JamiiForums
βœ”
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FAIDA ZA STRAWBERRY MWILINI

- Husaidia kuimarisha uwezo wa Ubongo katika kuweka na kutunza kumbukumbu

- Yana kiwango kikubwa cha Madini ya Zinc ambayo husaidia kuimarisha #Afya ya Uzazi kwa Mwanaume
-
- Matunda haya yana Vitamini E ambayo hunyoosha mikunjo ya Ngozi na kupunguza mchakato wa kuzeeka

Soma - https://jamii.app/StrawberryFaida

#JFAfya
πŸ‘15πŸ₯°1
CHINA YARUSHA MAKOMBORA KARIBU NA TAIWAN

Imerusha Makombora kufuatia ziara ya Spika wa Bunge la Marekani, Nancy Pelosi ktk kisiwa hicho

#Taiwan inadai Makombora yalikuwa 11, pia kulikuwa na Ndege za kijeshi zilizoonekana kuzunguka eneo

Soma https://jamii.app/MakomboraYaChina
#JamiiForums
πŸ‘12
RWANDA YATUHUMIWA KUWASAIDIA WAASI WA M23 NCHINI #DRC

Kwa mujibu wa ripoti ya Baraza la Usalama la UN, #Rwanda imefanya uingiliaji wa Kijeshi katika Ardhi ya Congo tangu Novemba 2021

Pia, ilitoa Wanajeshi kwaajili ya operesheni za M23

Soma - https://jamii.app/RWDM23UN
πŸ‘8
SUDAN KUSINI: SERIKALI YA MPITO KUBAKI MADARAKANI KWA MIAKA MIWILI ZAIDI

Sudan Kusini ilipaswa kufanya Uchaguzi Februari 2023, lakini hadi sasa Serikali hiyo imeshindwa kutimiza masharti muhimu ya makubaliano ikiwemo kuandaa #Katiba mpya

Soma - https://jamii.app/SudanMpito2

#Democracy
Ukatili/Uonevu Mtandaoni hupenya katika kila nyanja ya maisha ya Mwathirika, na unaweza kusababisha matatizo ya Kisaikolojia na Kijamii

Kuwa "Raia bora wa Mtandaoni" (Good Netizen) ni pamoja na kujua kile kinachofaa kufanya katika mazingira ya Mtandaoni

#JamiiForums #DigitalRights #CyberBullying
Mara baada ya kujifungua, Mama na Mtoto wagusane Ngozi kwa Ngozi ili kusaidia Maziwa kutoka

Virutubisho vilivyomo kwenye Maziwa ni:
Maji 87%
Wanga 7%
Mafuta 4%
Protini 1%
Vingine 1% (Vitamini, Madini, Kingamwili, Vimeng'enya, Kiinitete)

Soma > https://jamii.app/KunyonyeshaMtoto

#WBW2022
πŸ‘9
#JFDATA: Matumizi ya Intaneti Duniani yaliongezeka maradufu kutokana na Mlipuko wa COVID-19 uliopelekea wengi kuitumia kwa Kazi, Masomo, Huduma muhimu na Mawasiliano

Mwaka 2020, Watumiaji wa Intaneti waliongezeka kwa 10.2% ambayo inatajwa kuwa idadi kubwa zaidi katika kipindi cha miaka 10. Kwa Mwaka 2021, ongezeko hilo lilifikia 5.8%

Fahamu zaidi - https://jamii.app/DataInternet
πŸ‘5πŸŽ‰1
SENEGAL: Serikali imetia saini Mkataba wa Amani na Waasi wa Chama cha Movement of Democratic Forces of Casamance (MFDC) wanaotaka kujitenga

Mkataba huo unatajwa kuweza kumaliza mzozo uliodumu tokea Mwaka 1982 Nchini humo

Soma https://jamii.app/AmaniSenegal

#Governance
πŸ‘5
Mdau anasema kuficha wazo la #Biashara na huku ukiwa huna mtaji si ufahari ila ni kuendeleza Umasikini

Ameshauri kuwashirikisha Wadau wa maendeleo ili kupata msaada wa hali na mali wa utekelezaji wa wazo hilo na kulipa uhai

Msome - https://jamii.app/BusinessIdea

#JFBiashara
πŸ‘4
MDAU: NAWEZAJE KUTUMIA KOMPYUTA KUINGIZA KIPATO?

Mdau wa JamiiForums.com anaomba ushauri akisema ameshawahi kuitumia kwenye shughuli za Stationery na ana uwezo wa β€˜Video production’

Je, umewahi kuingiza kipato kupitia Kompyuta? Mshauri Mdau anavyoweza kujiajiri

Mjadala - https://jamii.app/ComputerKujiajiri

#Maisha #JFBiashara
πŸŽ‰2πŸ”₯1πŸ₯°1
KENYA: Serikali imesema madai ya Naibu Rais, William Ruto kuhusu kuzima Umeme na Mtandao ili kutekeleza wizi wa Kura ni kejeli

Imesisitiza, hakuna nia ya kuingilia mitambo na huduma zinazosaidia uendeshaji wa Uchaguzi

Soma - https://jamii.app/InterntShutdown

#KenyaDecides #DigitalRights
πŸ‘3
MOROCCO: Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, Aziz Akhannouch anakabiliwa na Shinikizo la kujiuzulu kutokana na kupanda kwa gharama za mafuta

Raia wanadai Kiongozi huyo ni sehemu ya tatizo kwani anamiliki moja ya Kampuni kubwa ya Mafuta Nchini humo

Soma https://jamii.app/WaziriMorocco

#Governance
πŸ‘1
MABONDIA 19 WA AFRIKA KUPIGANA NUSU FAINALI YA JUMUIYA YA MADOLA

Mabondia hao wanatarajiwa kupanda ulingoni Agosti 6, 2022

Mtanzania Kassim Mbundwike atapigana na Tiago Muxanga wa Msumbiji. Mtanzania Yusuf Lucasi Changalawe atazichapa na Sean Lazerini

Soma https://jamii.app/BoxingInUK

#JFSports
πŸ‘6❀2πŸ‘1
USHAURI WA MDAU KUHUSU MAMBO YA KUMFUNDISHA MTOTO WAKO

1) Mkumbushe Wivu utamfanya amchukie Mtu ambaye alipaswa ajifunze kutoka kwake. Mkumbushe Msaada sio Haki yake, asipopewa asinung'unike atafute chake

2) Tumeona mazuri kwa Watu waliokuwa wakiitwa wabaya na tumeona mabaya kwa Watu waliokuwa wakiitwa wazuri, aishi na kila Mtu kwa akili

Soma zaidi - https://jamii.app/JumbeMwanao

#Maisha #JFMdau
πŸ‘17πŸ‘6
MDAU: MAJINA YETU YA ASILI YAMEPOTEZA MVUTO AU TUNAONA AIBU KUYATUMIA?

- Anasema kwa sasa Watanzania wengi wana majina ya kisasa zaidi na tumebakisha majina ya mwisho kuwa ya asili ila ya mwanzo wengi ni ya Kizungu ama Kiarabu

- Je, majina yetu ya asili yamepoteza mvuto ama tunajisikia wa kale pale tunapoyatumia majina hayo?

Mjadala - https://jamii.app/MajinaAsili
#Maisha #JFMdau
πŸ‘12😁2
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
Wikiendi hii iwe njema kwako na kwa wote uwapendao

Asante kwa kuwa sehemu ya Familia ya JamiiForums!
πŸ‘26❀10
Ripoti ya CAG 2020/21 ilibaini Matumizi ya bila nyaraka stahiki na toshelezi yalifanywa na Taasisi 48

Ili kuondoa matumizi yasiyo na tija kwa Serikali, Taasisi ya #WAJIBU inashauri Maafisa waliohusika kufanya matumizi hayo kwenye Taasisi za Umma wawajibishwe

#JFUwajibikaji
πŸ‘1
JAJI MKUU: MAJAJI WAPANGIWE IDADI YA KESI KWA MWAKA

Prof. Ibrahim Juma ametoa ushauri huo akisema utaratibu ambao unatumika ni wa mwaka 1979

Lengo ni Shauri moja liwe Mahakamani ndani ya siku 350 ili kupunguza mrundikano

Soma > https://jamii.app/KesiMahakamani

#JamiiForums
πŸ‘12
SUDAN KUSINI: Rais Salva Kiir amewafukuza kazi Waziri wa Fedha, Agak Achuil Lual pamoja na Gavana wa Benki Kuu, Moses Makur. Sababu za uamuzi wake hazijawekwa wazi

Gavana wa zamani, Dier Tong ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha

Soma - https://jamii.app/SiasaSudanKusini

#Governance
πŸ‘8
UCHAGUZI KENYA: Jane Kibe (48) na Peris Wanjiru (35) wamenusurika kifo baada ya kuchomwa visu na kijana mmoja (17) kwa madai ya kukataa kumuunga mkono Baba yake anayegombea Ubunge

Mtuhumiwa ni rafiki wa karibu wa mtoto wa Wanjiru

Soma https://jamii.app/ShambulioVisu

#Democracy
πŸ‘Ž9πŸ‘5