JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
FRANCIS STOLLA (RAIS MSTAAFU WA TLS): Mahakama ni Mhimili unaojitegemea ukiachana na Teuzi

> Nchi yetu inapaswa ijengwe na Mifumo. Inabidi Tawala na Idara mbalimbali nchini zifanye kazi kimfumo

Soma - https://jamii.app/KongamanoTLS

#Democracy30 #30YrsOfMultipartism
👍5
ADO SHAIBU (ACT WAZALENDO): Vyama vya Siasa viwajibike kutengeneza mazingira bora ya Ushiriki wa Wanawake ktk Siasa

> Demokrasia isipoimairishwa, Siasa zikiendelea kuwa za piga ua, za baruti, za mabomu, za kukimbizana itawafanya Wanawake washindwe kushiriki Kisiasa

#Democracy30
👍2
USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU: UNAWEZAJE KUJILINDA MTANDAONI?

- Kuwa Makini na Urafiki wa Mitandaoni: Wahalifu hutumia Mitandao kujenga uaminifu

- Usiamini kila tangazo kirahisi: Wanaofanya Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu hutoa ahadi nono ambazo ni rahisi kumshawishi yeyote

Fahamu zaidi > https://jamii.app/HumanTRF2022

#EndHumanTrafficking
👍6
ALPHONCE SIMBU ASHINDA MEDALI YA FEDHA

Mwanariadha Mtanzania, Alphonce Felix Simbu ametwaa Medali ya Fedha baada ya kuibuka mshindi wa pili wa Mbio za Riadha katika Michezo ya Jumuiya ya Madola Jijini Birmingham, Uingereza

Simbu ametumia muda wa 2:12:29 huku Mshindi wa Kwanza, Victor Kiplagat ambaye ni Raia wa Uganda akitumia 2:10:55

#JFSports
👏19👍7
SENZO KUONDOKA YANGA, WAKILI SIMON PATRICK AKABIDHIWA MIKOBA

Klabu ya Yanga imetangaza kutomuongezea Mkataba Afisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingiza anayemaliza mkataba wake kesho Julai 31, 2022

Yanga imesema Senzo ndiye ameomba kutoongezewa mkataba kutokana na sababu za kifamilia. Wakili Simon Patrick ameteuliwa kukaimu nafasi

Soma - https://jamii.app/SenzoYangaApart

#JFSports
BONDIA MANDONGA APIGWA KWA KO

Bondia Karim Mandonga amepoteza dhidi ya Shabani Kaoneka, Raundi ya 4 kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea

Baada ya pambano Mandonga amesema: "Ni ajali kazini lakini nipo tayari kurudiana na mpinzani wangu."

Soma > https://jamii.app/MandongaApoteza

#JFSports
😁32👍6🔥3
KIDUNDA AMPIGA KATOMPA KWA POINTI

Bondia Mtanzania Selemani Kidunda ameshinda Mkanda wa WBF Inter Continental kwa pointi dhidi ya Eric Katompa wa DRC

Pambano lilikuwa la Super Middleweight Raundi 10 kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea

Soma > https://jamii.app/NdondiSongea

#JFSports
👍17👏5👎1
UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky ameamuru Raia waliopo katika Mji wa Donetsk kuondoka haraka kutokana na kuendelea kwa mapigano dhidi ya Vikosi vya Urusi

> Rais huyo amesema Serikali itawasaidia kwa Fedha wote wanaohamishwa

Soma https://jamii.app/KuhamaDonetsk

#RussiaUkraineWar
👍5😁2
MISRI: Wafungwa 7 wakiwemo Mwandishi wa Habari, Hisham Fouad pamoja na Mtafiti wa Masuala ya Binadamu (Anthropology), Ahmed Samir ambao walishtakiwa kwa Makosa ya Ugaidi wameachiwa huru

> Wameachiwa kwa msamaha wa Rais

Soma https://jamii.app/WafungwaWaachiwa

#JamiiForums
👍7
KAONEKA: KAMA NITARUDIA PAMBANO NA MANDONGA, SITAFANYA MAZOEZI

Bondia Shabani Kaoneka aliyempiga kwa TKO Karim Mandonga amesema yupo tayari kwa pambano la marudio

> Amesema hatafanya mazoezi ili kupambana na Mandonga kwa kuwa udhaifu wake anaujua

Soma https://jamii.app/BondiaKaoneka
😁37👍3👏1
NDEGE ZISIZO NA RUBANI ZA UKRAINE ZASHAMBULIA MELI ZA URUSI

Mashambulizi hayo yametokea katika Bandari ya Crimea na kujeruhi Watu watano

> Wakazi wa eneo hilo wametakiwa kubaki ndani kwa sababu za kiusalama

Soma https://jamii.app/RussianFleetAttacked

#RussiaUkraineWar
👍13
MDAU: JITIHADA HUAMUA KUFANIKIWA AU KUFA KWA BIASHARA

Amefafanua kuwa, kila biashara au fursa ina uwezo wa kutengeneza faida kubwa ikiwa tuu nguvu, ubunifu na mtaji stahiki vitawekezwa kwa wakati sahihi

Soma - https://jamii.app/JitihadaBiashara

#JFBiashara
👍7🥰1
UTEUZI WA DKT. CHEGENI WATENGULIWA

Rais Samia ametengua uteuzi wa Dkt. Raphael Masunga Chegeni na kumteua Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara

Meja Jenerali Mzee alikuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP)

Soma - https://jamii.app/UteuziMara

#Governance
👍14😁6
RONALDO AONDOKA OLD TRAFFORD MECHI IKIENDELEA

Cristiano #Ronaldo ameichezea Manchester United mechi ya kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano, alitolewa wakati wa mapumziko, akaondoka mechi ikiendelea

> Matokeo ya mchezo huo yalikuwa 1-1

Soma https://jamii.app/CR7Exit

#JFSports
😁17👍4👎3🤔2
MYANMAR: Kiongozi wa Kijeshi, Min Aung Hlaing ameongeza muda wa hali ya hatari kwa Miezi 6 huku akisema ni juhudi za kutekeleza mpango wa amani

Jeshi lilitangaza hali ya hatari Februari 2021 baada ya mapinduzi ya Kijeshi

Soma https://jamii.app/HatariMyanmar

#JFDemokrasia
🤔4
KENYA: Siku 10 baada ya Serikali kushusha bei ya Unga wa Mahindi kuwa Ksh. 100 (Tsh. 1,960) toka Ksh. 200 (Tsh. 3,920) kwa Kilogramu 2, uhaba wa bidhaa hiyo umekuwa mkubwa Madukani

- Serikali imewaonya wanaoficha na kutangaza msako kuanzia Agosti Mosi

Soma - https://jamii.app/UngaWaUgaliKE
👍5
MDAU: WATOTO WANAHITAJI ULINZI KIPINDI HIKI CHA LIKIZO YA SENSA

- Anasema Mitaani pamefurika kila aina ya Makundi na Watu wa rika tofauti. Huu ni muda wa Wazazi/Walezi kuchukua tahadhari ya kulinda Watoto wanapocheza

- Anashauri Wazazi kupangilia muda wao vizuri kwaajili ya usalama wa Watoto, ama kuwakabidhi sehemu salama pindi wasipokuwepo

Soma - https://jamii.app/WatotoSensa

#Malezi #Parenting
👍15
FAIDA ZA 'KIWIFRUIT' KIAFYA

1. Huimarisha Kinga na kuzuia Magonjwa: Kiwifruit moja huzalisha karibu 80% ya Vitamini C inayohitajiwa na Mwili kwa siku

2. Husaidia kuondoa Shinikizo la Damu na kuboresha Afya ya Moyo: Linaweza kupunguza hatari ya Kiharusi na Ugonjwa wa Moyo

Soma - https://jamii.app/BenefitsKiwi

#JFAfya #Health
👍12
Mdau wa JamiiForums.com anasema Watu wengi wenye #Biashara na Kampuni hawaajiri Vijana kwa kuhofia kuhujumiwa na huishia kuajiri Watu wa makamo wakiamini hawana Tamaa kama Vijana

Unakubaliana kwa kiasi gani na hoja hii?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/VijanaSokoAjira

#JFMaisha
👍19👎4
MDAU: FANYA YAFUATAYO KUWAEPUSHA WATOTO WAKO NA JANGA LA AJIRA

1. Tutambue Vipaji na Vipawa vya Watoto mapema na kuviendeleza. Wafundishe Wanao kile ulichonacho. Ikiwa ni Mfanyabiashara anza kumzoesha kusimamia na kuijua #Biashara yako

2. Wakati wa likizo jaribu kumshikiza Mwanao katika maeneo yatakayomsaidia kuwa na ujuzi na Maarifa mbalimbali. Usikomae na 'tuition' tu ikiwa maendeleo yake sio mabaya.

Soma zaidi - https://jamii.app/UjuziWatoto

#Ajira #JFMdau #Maisha
👍15