JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ripoti ya CAG 2020/21 imeonesha kumekuwepo na mianya ya uvujaji wa Mapato ambayo kama yangesimamiwa kwa umakini, yangeweza kuleta tija kwa Jamii

Mawakala kukusanya Mapato na kutoyawasilisha kwenye Halmashauri, ama Halmashauri kutokusanya Mapato kutoka vyanzo mbalimbali ni kiashiria cha Rushwa na Ubadhirifu wa Fedha za Umma

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji #KemeaRushwa
😁4πŸ‘2
Machache ambayo Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezungumza katika Uapisho wa Wakuu wa Mikoa leo Agosti 01, 2022

Soma - https://jamii.app/UteuziWateule

#Governance
πŸ‘6πŸ‘Ž1😁1
Nukuu za Rais Samia Suluhu Hassan leo baada ya Uapisho wa Viongozi Ikulu, Dar es Salaam

#JamiiForums #Governance
πŸ‘6
MALI YAISHUTUMU UFARANSA KWA UKOLONI MAMBOLEO

Rais Emmanuel Macron alikaririwa akisema Mataifa ya Kanda yalikuwa na jukumu la kuhakikisha Raia wa #Mali wanaweza kuonesha Nguvu ya Umma

Kauli yake ilitafsiriwa kuwa ya kichochezi na Jeshi la Mali

Soma https://jamii.app/ShutumaMali

#JFDiplomasia
πŸ‘10
AFRIKA KUSINI: Wanaume 82 wanashikiliwa kwa madai ya kubaka kundi la Wanawake waliokuwa wanarekodi video ya Muziki ktk eneo la Mgodi, Johannesburg

Raia wametoa wito wa kuhasiwa kwa kemikali watuhumiwa watakaopatikana na hatia

Soma - https://jamii.app/UbakajiWaMakundi

#UkatiliKijinsia
πŸ€”11πŸ‘4πŸ‘Ž1πŸ₯°1
MAMA ADAIWA KUMUUA MWANAYE WA MIAKA MITATU KWA FIMBO

Mtuhumiwa (27) alimchapa mwanaye sehemu mbalimbali za mwili, chanzo kikidaiwa ni mtoto kufungua bomba na kuchezea maji ya baridi

Jeshi la Polisi limesema Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea

Soma https://jamii.app/AmuuaMwanaye

#HakiMtoto
😒15πŸ‘Ž3πŸ‘2πŸ€”1
VIELELEZO VYA WIZI VYAIBWA KITUO CHA POLISI

Mali zilizokuwa Kituo Kidogo cha Polisi Uchira, Wilaya ya Moshi, Kilimanjaro kama vielelezo zimeibwa

Anayedaiwa kuiba ni mtuhumiwa wa kesi hiyo, alitaka kuharibu ushahidi wa kesi yake

Soma > https://jamii.app/TukioLaWizi

#JFMatukio
😁41πŸ‘5πŸ‘1
MAREKANI YAMUUA KIONGOZI WA AL QAEDA

Rais Biden amesema Ayman al-Zawahiri ameuawa kwa shambulio la 'Drone' Jijini Kabul Nchini Afghanistan. Inaelezwa, alihusika katika mashambulizi ya Septemba 11, 2001 yaliyoua takriban watu 3,000

Kifo chake kimetajwa kuwa pigo kubwa zaidi kwa Kundi hilo tangu kuuawa kwa Osama bin Laden mwaka 2011

Soma https://jamii.app/ZawahiriKilled
πŸ‘18😁2πŸ‘Ž1πŸŽ‰1
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA JAMII YENYE MTAZAMO HASI

- Jithamini ujue thamani yako

- Kipaumbele chako kiwe kutenda mema pasipo kujali mtazamo wa wengine

- Ishi kwa tahadhari hususan kwa watu wanaokuzunguka

- Fahamu aina ya watu wanaokuzunguka pamoja na mtazamo wao

- Kuwa mwepesi kusamehe

Msome > https://jamii.app/MaishaYaJamii

#JFMaisha
πŸ‘11
KENYA: Serikali imetangaza kufungwa ghafla kwa shule zote kuanzia Agosti 2, 2022 kabla ya Uchaguzi Mkuu na kufunguliwa Agosti 11, 2022

> Wanafunzi ambao tayari wameanza mitihani ya katikati ya Muhula wamebaki na sintofahamu

Soma - https://jamii.app/ShuleKenya

#Kenya2022
πŸ‘13πŸ€”3
RAIS WA ZAMBIA AWASILI TANZANIA

- Rais Hakainde Hichilema amewasili Nchini kwa ziara ya Kiserikali ya siku 1 na kupokelewa na Rais Samia Suluhu

- Ziara inakusudia kuimarisha zaidi mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Zambia na Tanzania

Fuatilia https://jamii.app/Hichilema-TZ

#JFSiasa
πŸ‘13
MDAU: WATANZANIA WANASTAHILI UFAFANUZI WA GHARAMA ZA INTANETI KUPANDA

Anasema Watu wengi hawaelewi na bado hawajapata ufafanuzi wa sababu zinazopelekea Vifurushi vya Intaneti kupanda mara kwa mara

Anaeleza, kupanda kwa gharama za Intaneti kuna athari mbalimbali kwa Wananchi ikiwemo kupunguza motisha ya kutafuta maarifa Mtandaoni

Soma - https://jamii.app/Vifurushi05

#DigitalRights
πŸ‘27πŸ‘Ž1
Ushiriki wa Umma katika masuala ya Kisiasa na Kidemokrasia ni sehemu muhimu ya Utawala wa Demokrasia

Wahusika wa mchakato wa Kusikiliza, Kuhoji, Kutafakari na Kufanya maamuzi yoyote katika Nchi ni Wananchi wenyewe

Zaidi, soma > https://jamii.app/UshirikiHuru

#Democracy #Governance
πŸ‘2
SERIKALI YAENDELEZA MARUFUKU YA β€˜LUMBESA’

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango amezuia vipimo visivyo rasmi ktk ununuzi wa mazao ikiwemo β€˜lumbesa’

Hii si mara ya kwanza β€˜lumbesa’ kuzuiwa. Waziri Mkuu Majaliwa aliizuia akisema inatumika kuwaibia Wakulima

Soma https://jamii.app/Mpango-lumbesa

#JFLeo
πŸ‘10
FEDHA ZA UMMA: USIMAMIZI DHAIFU HUPELEKEA MATUMIZI YASIYO NA TIJA

Ripoti ya CAG 2020/21 inaonesha udhaifu katika usimamizi wa matumizi ya Fedha za Umma

Hii imepelekea kuwepo matumizi nje ya Bajeti, matumizi yasiyo na tija na kufanyika malipo bila kudai risiti

#JFUwajibikaji
πŸ‘4