JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UNAWEZAJE KUJIKINGA NA HOMA YA INI?

1) Usichangie matumizi ya vitu vyenye ncha kali vikiwemo viwembe

2) Kunywa Maji na kula Chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi na salama

3) Jua Afya yako kwa kufanya vipimo vya Homa ya Ini

4) Tumia Kinga kwa usahihi wakati wa kujamiiana

Fahamu zaidi > https://jamii.app/HomaIni2022

#WorldHepatitisDay2022 #JFAfya
👍5
LOLIONDO: Washtakiwa 3 kati ya 27 waliokuwa wanakabiliwa na makosa mawili likiwamo la mauaji ya Askari katika eneo la Loliondo, wamefutiwa kesi na kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha

> Wameachiwa baada ya DPP kukosa nia ya kuwashtaki

Soma https://jamii.app/KesiLoliondo
👍12😁3🥰1
#JFSHAIRI: Ukatili ni kitendo anachofanyiwa Mtu yeyote kwa lengo la kumdhuru au kumuumiza Kisaikolojia, Kimwili, Kiafya, Kingono na Kiuchumi

Jifunze kupitia Shairi hili kutoka kwa Mdau wa JamiiForums.com likizungumzia Ukatili unaofanyika kwenye Jamii

#JamiiForums #Violence #GBV
👍10
KENYA: Serikali imetaifisha takriban Tsh. Bilioni 3.9 za Rigathi Gachagua (Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Kenya Kwanza) kwa kushindwa kueleza jinsi alivyozipata kutoka kwa Mashirika ya Serikali

> Anashukiwa kuhusika na Utakatishaji Fedha

Soma https://jamii.app/UtaifishajiKenya

#Kenya2022
👍13😁2
#GUINEA: Maandamano dhidi ya Serikali ya Kijeshi na usimamizi wake wa mipango ya kurejesha Demokrasia yameripotiwa Jijini #Conakry

Inadaiwa, Utawala wa Kijeshi haupo tayari kufanya mazungumzo yatakayofafanua Kanuni za Kipindi cha Mpito

Soma https://jamii.app/GuineaProtests1

#Democracy
👍10
NIGERIA: Serikali imesema itaweka vikwazo kwa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na Trust TV kwa kutukuza Ugaidi baada ya vituo hivyo na kuonesha Filamu kuhusu Magenge ya Uhalifu ya Kaskazini Magharibi mwa Nchi hiyo

Soma https://jamii.app/NigeriaNaBBC
👍8
MSUMBIJI: Aliyekuwa Waziri wa Kazi, Maria Helena Taipo amehukumiwa kifungo cha Miaka 16 jela kwa Makosa ya Rushwa yanayohusisha kujipatia takriban Tsh. Bilioni 3.96 kutoka katika Fedha za Umma kati ya mwaka 2014-2015

Soma - https://jamii.app/WaziriUfisadi

#KemeaRushwa
👏7👍4
RUKWA: Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tanga, Emmanuel Jerome anadaiwa kumuua Mkewe, Lucy Nshoma kwa kumnyonga kisha na yeye kujiua kwa kujinyonga siku moja baadaye

> Emmanuel alimtuhumu mkewe kuwa na uhusiano na Wanaume wengine

Soma https://jamii.app/WanandoaWafariki

#JFMatukio
👍6🤔4👎1🎉1
UTOLEWAJI FEDHA PUNGUFU HUATHIRI UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI

Serikali Kuu ilipanga kutoa Tsh. Bilioni 928.05 ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hata hivyo, kiasi kilichotolewa ni Tsh. Bilioni 662.68, sawa na 71% ya Bajeti iliyopangwa

Kutolewa Fedha pungufu kwenye baadhi ya Halmashauri husababisha Halmashauri hizo zishindwe kutoa Huduma zilizopangwa kwa Wananchi

#JFUwajibikaji
👍3
Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji ni muhimu ili kuhakikisha Rasilimali za Umma zinatumika ipasavyo na Sera zinaundwa kwa maslahi ya watu

Ushiriki wa Wananchi huwawezesha kuwajibisha Mamlaka na kukemea Ubadhirifu, Ufisadi na Rushwa

Soma https://jamii.app/UwaziSerikali

#Accountability #Transparency #JFUwajibikaji
👍8
Ili kuweza kuona fursa hizi na nyingine nyingi za Ajira, tembelea > https://jamii.app/NafasiAjira

#JamiiForums
👍3
WAZIRI WA AFYA: Tangu Julai 18, 2022 hadi sasa hakuna maambukizi mapya ya Homa ya Mgunda na Wagonjwa 17 wameruhusiwa kwenda nyumbani

> Waliofariki kwa Homa hiyo ni 3 huku Watu 15 waliochangamana na Wagonjwa wamekutwa hawana maambukizi

Soma https://jamii.app/HomaYaMgundaUpdates

#JFAfya
👍10
SERIKALI: UPANDISHAJI MISHAHARA UNAANGALIA HALI YA UCHUMI

Akizungumza kuhusu Nyongeza ya Mishahara, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema katika mchakato ya upandishaji Mishahara, Serikali inaenda kwa kuangalia Hali ya Uchumi wa Nchi ili kutokwama katika mambo mengine

Amefafanua, "Tunaangalia gurudumu hili tunavyolipeleka sisi wenyewe tusije tukalikimbiza likatukwamisha, tukafika mahali tumegota tukashindwa kwenda. Mwenendo huu wa kiuchumi sisi ndio tunaushikilia, tunausimamia na tunautekeleza"

Soma - https://jamii.app/NyongezaMishahara
👍10😁4🤯2👎1
MAJALIWA: WANAOSEMA TUMEONGEZA 20,000 NI WENYE MISHAHARA MIKUBWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wanaosema kuhusu ongezeko dogo la mishahara ni wale ambao wana mishahara mikubwa na ambao unatosha

Ameeleza, "Ni kweli 23% iliyotamkwa haijalipa watu wote, na hii ni kwasababu ya Formula inayotumika katika kutamka viwango vya Mshahara. Inapotamkwa wanaonufaika si wote mpaka wa mishahara mikubwa, bali ni wale wa kada ya chini"

Soma - https://jamii.app/PMMishahara
👍17😁4🤯3👏2🤔2💩1
Mdau wa JamiiForums.com anasema miongoni mwa vitu unavyotakiwa kujua mapema katika maisha ni kutoruhusu mazoea na kila mtu

Anashauri usipende kusema mipango yako kwani Watu hawapo vile unavyowaona/wanavyojionesha, na pia waepuke watu wanaopenda kuomba omba Msamaha, wakiuchukulia kuwa ni kitu rahisi

Msome zaidi > https://jamii.app/MdauMaisha

#JFMaisha
👍71👏1
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa aliyewahi kuwa Waziri wa Usalama wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Nourredine Adam kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa Mapinduzi ya mwaka 2013

Soma - https://jamii.app/WaasiCAR
👍8
RUTO: KENYATTA, ACHA KUNIONGELEA NA KUTISHA WAKENYA

Amemjibu Rais Uhuru Kenyatta akisema kama hamuungi mkono, amuache

Amesisitiza "Tafadhali Rais, hutakiwi kuwa chanzo cha vitisho. Kazi yako ni kuhakikisha Wakenya wote wakae pamoja"

Soma - https://jamii.app/KenyattaRutoSaga

#Kenya2022 #Democracy
👍15🤔2👎1
IRAN: MAFURIKO YA SIKU MBILI YAUA WATU 53

Mbali na vifo, taarifa rasmi ya Serikali imesema Watu wengine 16 hawajulikani walipo

Mafuriko hayo yameathiri Watu 400 katika Vijiji 18 na kusababisha Miundombinu mingi kuharibika

Soma - https://jamii.app/MafurikoIran
👍4😢4