JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Tume ya Utumishi wa Walimu Wilayani Geita imewafukuza kazi Walimu wawili wa Shule ya Sekondari Kivukoni na 6 wa Shule za Msingi za Nyantorotoro, Kivukoni, Lubanda, Mtakuja na Mkoani kwa utoro kazini

> Wanadaiwa kujihusisha na Mtandao wa Q-Net

Soma - https://jamii.app/UtoroWalimu
😁11👍2👏1😢1
James Januari (4) aliyejeruhiwa katika tukio la mauaji ya Watu 6 wa familia moja ktk Kijiji cha Kiganza, Wilayani Kigoma amefariki usiku wa kuamkia leo Julai 5, 2022

> Mtoto huyo amefariki akiwa Morogoro njiani kuelekea Hospitali ya Muhimbili

Soma - https://jamii.app/MtotoKufariki

#JamiiForums
😢13👍5
SIERRA LEONE: TIMU ZAFUNGANA 95-0, 91-1

Kahunla Rangers imeishinda Lumbelu United magoli 95-0, huku Gulf FC ikishinda 91-1 dhidi ya Koquima Lebanon

Matokeo hayo ya mechi za Daraja la Kwanza yanachunguzwa na Mamlaka za Soka

Soma - https://jamii.app/MatokeoYaAjabu

#JFSports
😁45👍10🔥3👏3🌚1
UINGEREZA: KASHFA ZA SERIKALI ZAPELEKEA MAWAZIRI 2 KUJIUZULU

Rishi Sunak amesema Umma unatarajia Serikali kuendeshwa kwa umakini

Sajid Javid asema Kura ya Imani kwa Waziri Mkuu ilikuwa wakati wa mwelekeo mpya, lakini ni dhahiri hali haitobadilika

Soma - https://jamii.app/2MinistersResign

#Accountability #Democracy
👍11
#TWITTER YAISHTAKI SERIKALI YA INDIA

Kampuni hiyo inapinga baadhi ya maagizo ya kuzuia 'Tweets' na Akaunti ikisema ni ukiukwaji wa #UhuruWaKujieleza

Idadi kubwa ya Akaunti na Tweets hizo zinadaiwa kukosoa Sera za Serikali

Soma - https://jamii.app/TwitterIndiaGovt

#DigitalRights
👍9
KISWAHILI SOMO LA LAZIMA MSINGI, SEKONDARI UGANDA

#Uganda imepitisha #Kiswahili kuwa Lugha rasmi Nchini humo

> Maamuzi hayo yamefikiwa ili kutekeleza mapendekezo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayotaka Wanachama kutumia Lugha hiyo

Soma - https://jamii.app/KiswahiliUG
👍26👏4
BEI ZA PETROLI, DIZELI ZAPANDA

Bei mpya kwa Dar: Petroli ni Tsh. 3,220, Dizeli ni Tsh. 3,143, Arusha: Petroli Tsh. 3,271, Dizeli 3,207

> Dodoma: Petroli Tsh. 3,279, Dizeli Tsh. 3,202, Mwanza: Petroli Tsh. 3,370, Dizeli Tsh. 3,293

Soma - https://jamii.app/BeiMpyaMafuta

#JamiiForums
👎24👍7
INDIA: VIVO YATUHUMIWA KUTAKATISHA FEDHA, OFISI ZAKE ZAPEKULIWA

Maafisa wamepekua Ofisi kadhaa za Kampuni ya Kielektroniki ya #Vivo kutoka China kufuatia shutuma za utakatishaji Fedha

Mapema mwaka huu, upekuzi wa aina hiyo pia ulifanywa kwa Xiaomi na #Huawei. Uhusiano wa India na #China umeonekana kuwa mbaya tangu mwaka 2020

Soma - https://jamii.app/VivoIndia
👍2👎1👏1
PWANI: Mtoto wa kike (5) amejeruhiwa na 'Dada wa Kazi za Ndani' kwa kumwagiwa mafuta ya moto sehemu mbalimbali za mwili wake kisha mtuhumiwa huyo kutoroka

> Polisi inamshikilia Baba wa Mtoto aliyejeruhiwa kwa madai ya kumsaidia Mtuhumiwa kutoroka

Soma - https://jamii.app/MtotoAjeruhiwa
😢7👍6🤔6👎1
RAIS SAMIA KUHUDHURIA MKUTANO SENEGAL

Rais Samia Suluhu Hassan ameondoka Nchini leo Julai 6, 2022 kuelekea Dakar, Senegal kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA Summit for Africa)

Tangu kuingia Madarakani Machi 2021, Rais Samia pamoja na Viongozi wengine wamekuwa wakihudhuria Mikutano mbalimbali Nje ya Nchi ili kuimarisha Diplomaisha na uhusiano wa Tanzania na Mataifa mengine

Soma - https://jamii.app/RaisSamiaDakar
👍11😁8👎51
Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema amefikia makubaliano na Kiongozi wa Sudan ili kusuluhisha kwa Amani mzozo wa mpaka ambao umesababisha mapigano hivi karibuni

> Sudan iliishutumu Ethiopia kwa kuua Wanajeshi wake, Ethiopia ilikanusha madai hayo

Soma - https://jamii.app/MakubalianoYaAmani
👍5😁5
NIGERIA: Watu wenye silaha za moto wameshambulia msafara wa Timu ya Walinzi na Maafisa wa Itifaki wa Vyombo vya Habari wa Rais Muhammadu Buhari katika Mjini wa Katsina na kujeruhi Watu wawili kabla ya Watu hao kudhibitiwa na Jeshi

Soma - https://jamii.app/BuharisConvoyAttacked

#JamiiForums
🔥9😱5👍4
Utumiaji holela wa Dawa za Kuzuia Mimba (P2) na za Kuongeza Nguvu za Kiume (Viagra) umedaiwa kuongezeka na kufanya jamii kuwa katika hatari ya kupata madhara kiafya

> TMDA imesema inafanyia utafiti dawa hizo na kutoa Elimu kuhusu matumizi yake

Soma - https://jamii.app/DawaKuchunguzwa

#Afya
👍15
HUKUMU YA KINA MDEE YAAHIRISHWA

Mahakama Kuu imeahirisha kutoa hukumu ya maombi ya Halima Mdee na wenzake 18 kuhusu kufukuzwa uanachama CHADEMA

> Uamuzi utatolewa Julai 8, 2022, Msajili amesema uamuzi haujakamilika

Soma - https://jamii.app/MdeeHukumu
👍7👎6🤯6
NJOMBE: Mahakama Kuu Kanda ya Iringa imewahukumu Elias Jackson Mwenda (31), Hussein Khamis (31) na Orestus Mbawala (51) kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya James Kaengesa

> Walitenda kosa hilo Juni 2016 ambapo pia walimpora James pikipiki yake

Soma - https://jamii.app/HukumuNjombe

#JamiiForums
👍12
SINGIDA: Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Singida, Thomas Ngiracha amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kujihusisha kimapenzi na Mwanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule hiyo

> Mwanafunzi aliwasilisha barua ya malalamiko akielezea usumbufu anaoupata

Soma - https://jamii.app/TuhumaKwaMwalimu
👍16👏2👎1
ETHIOPIA: Afisa wa Wilaya ya Konso amethibitisha vifo vya Watoto 13 kutokana na njaa akisema idadi ya Watoto wenye utapiamlo inaongezeka na zaidi ya Watoto 240 wamelazwa

> Ukame katika eneo hilo umesababisha takriban Wakazi Milioni 18 kukosa chakula

Soma - https://jamii.app/NjaaEthiopia
😢9👍5👎21
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
Fanya vitu kwa ajili yako, sio kufurahisha wengine. Simama imara siku zote ili kesho yako iwe bora kuliko jana!

#JamiiForums
👍9🔥9👏43🤯1
ZAMBIA: Nahodha wa Timu ya Taifa ya Wanawake ameondolewa kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufeli 'Vipimo vya Ustahiki wa Jinsia'

> Hii ni kutokana na kiwango chake cha Homoni za Testosteroni kuwa juu kupita kiasi

Soma - https://jamii.app/ZambiaWAFCON

#JFSports
😢15👍7🤔5
Tunawatakia Watanzania wote Maadhimisho mema ya Siku ya Sabasaba

#Sabasaba2022 #JamiiForums
👏16👎5🙏4👍31