JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MDAU: HARUSI ZIENDANE NA HALI HALISI YA MAISHA

Anasema Harusi nyingi huwa na hekaheka na kile alichodai ni 'usumbufu' mwingi kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki

Anashauri Familia zenye hali ya kati na chini kiuchumi kufanya Harusi zilizo ndani ya uwezo wao, akisisitiza ni wakati wa kubadilika na kuacha mazoea ya kizamani

Mjadala - https://jamii.app/MdauMichango
👍224💩1
Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga ameishauri Serikali kuongeza nguvu ya kutoa Elimu kwa jamii ili kupunguza tatizo la mimba za utotoni badala ya kuongeza nguvu katika ujenzi wa mabweni

> Amesema mimba za utotoni kwa Tabora ni 43%

Soma - https://jamii.app/ElimuYaMimba
👍5
ETHIOPIA: Zaidi ya Watu 100 wengi wao wakiwa ni kutoka jamii ya Amhara wameuawa katika shambulio linalodaiwa kufanywa na Wanamgambo wa OLA ktk eneo la Oromia

> Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amelaani na kuita tukio hilo ni la kikatili

Soma - https://jamii.app/MauajiEthiopia
👎42👍2😢2
MASHABIKI WA CHELSEA WAKASIRIKA LUKAKU KUJIPELEKA INTER

Baadhi ya mashabiki wamelaani kitendo cha Romelu Lukaku kupiga simu kwa Kocha wa Inter Milan kuomba amsajili

> Alifanya hivyo miezi miwili iliyopita Chelsea ikiwa bado mashindanoni

Soma - https://jamii.app/LukakuChelsea

#JamiiForums
😁16👍5
ZELENSKY: VITA YA URUSI IMEFANYA AFRIKA KUWA "MATEKA"

Akihutubia Umoja wa Afrika (AU), amesema inawezekana Vita inaendelea mbali na Mataifa ya Afrika, lakini ongezeko katika bei za Vyakula tayari limeileta Vita hiyo kwa Mamilioni ya Familia

Soma - https://jamii.app/ZelenskyAU
👍21👎14😁92
UNYANYASAJI WA KIJINSIA: KANUNI ZA MAADILI KWENYE USAFIRI WA UMMA ZAZINDULIWA KENYA

Hatua hiyo inakuja kufuatia malalamiko ya unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika kwa maneno au kimwili, ikielezwa Kanuni zinalenga kuhakikisha usalama

Unyanyasaji huo unatajwa kujidhihirisha mtu anapoguswa kwa namna isiyokubalika, kuangaliwa kwa matamanio na maoni/ucheshi uliochochewa kingono

Soma - https://jamii.app/KanuniMaadili
👍3👎2
Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2022/23 imeonesha kuwa mnamo mwezi Juni 2022, Serikali ilisaini mikataba ya kusambaza maji kwa Miji 28 kwa fedha za mkopo toka Exim Bank - India wenye thamani ya Tsh. 1,165,000,000,000

Soma - https://jamii.app/BajetiKuuTz

#BajetiKuu
🤔4👍1
TETESI: LIVERPOOL YAMUWANIA BARELLA

Inadaiwa Liverpool inataka kumsajili Kiungo wa Inter Milan, Nicolo Barella na ipo tayari kubadilishana na mchezaji wake, Naby Keita

Hata hivyo Inter inadaiwa kutaka Paundi Milioni 77 (Tsh. 218,680,000,000) ili kumuachia Barella

#JFSports
👍5
MAIMU NA WENZAKE WAFUTIWA MASHTAKA

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Ernest Maimu na wenzake wote wamefutiwa mashtaka yao yote baada ya DPP kukosa nia ya kuendelea na kesi yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu

Oktoba mwaka 2021, Maimu alifutiwa kesi moja ya Utakatishaji Fedha na kusalia na Mashtaka ya Uhujumu Uchumi, kuisababishia Serikali hasara na Matumizi mabaya ya Madaraka

Soma - https://jamii.app/MaimuKisutu
👍13👎4
SIMBA SC YAACHANA NA WAWA

- Pascal Wawa aliyeitumikia Simba kwa misimu minne, ataondoka klabuni hapo mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa Juni 2022

- Wawa ni mchezaji wa 3 kuagwa na #SimbaSC baada ya Bernard Morrison na Rally Bwalya

Soma > https://jamii.app/WawaSimba

#JFSports
👍14
MALI: Serikali imesema raia 132 wameuawa baada ya Vikundi vya Waasi ambao ni Wanachama wa kundi lenye silaha la Katiba Macina kuvamia Vijiji ktk Mji wa Mopti na kushambulia

> Kundi hilo linatajwa kuwa na uhusiano na Kundi la Al-Qaeda

Soma - https://jamii.app/Watu100Wauawa

#JamiiForums
👍6😢3👎2
Bajeti ya Serikali ya 2022/23 imependekeza taarifa zilizopo kwenye Kitambulisho cha NIDA zitumike kutengeneza Leseni za Udereva

> Dereva akifuzu mafunzo atoe Namba ya NIDA halafu TRA na Polisi waoanishe taarifa na wamtumie mhusika Leseni kwa simu

Soma - https://jamii.app/BajetiKuuTz
👍22😁5
#BURKINAFASO: Jeshi limewataka raia kuondoka katika maeneo yanayotajwa kuwa na maslahi ya kijeshi kabla ya oparesheni zinazolenga kudhibiti ghasia kuanza

Mashambulizi yameendelea licha ya ahadi ya kuimarisha Usalama baada ya Mapinduzi ya Kijeshi

Soma - https://jamii.app/JeshiRaisBF
👍13🔥1
#DIGITALSECURITY: Tumia USB zisizoruhusu taarifa kuhama kutoka kwenye simu yako kwenda kwenye chombo kingine

> Ukitumia USB inayoweza kuhamisha mafaili chagua "Option" ya "Charge Only" na uifunge simu yako ili kuzuia uhamishaji wa data zako

Soma - https://jamii.app/PersonalDataProtection
👍17
ARUSHA: Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Dkt. John Pima (44) pamoja na wenzake 4 wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na mashtaka mengine ya Uhujumu Uchumi ikiwemo ya Utakatishaji Fedha

Soma - https://jamii.app/KesiDktJohnPima

#JamiiForums
👍6🤔1
VIPINDI VYA BARIDI KUENDELEA KWA BAADHI YA MIKOA

Viwango vya chini vya Joto katika Mikoa ya Njombe na Mbeya vinatabiriwa kuwa 5°C, Iringa 11°C, Tabora 12°C, Arusha 14°C, Mwanza na Dodoma 16°C

Aidha, upepo mkali unatarajiwa katika baadhi ya maeneo

Soma - https://jamii.app/MikoaBaridi
👍17
WANASHERIA 5,065 WALIOKOPESHWA KUANZA KULIPA

Walikopeshwa zaidi ya Tsh. Bilioni 10.6 wakiwa Wanafunzi wa Law School of Tanzania (2008-2015)

> Watarejesha kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kuanzia Julai Mosi, 2022

Soma - https://jamii.app/MikopoSheria
👍11😢1
KENYA: Mgombea Urais, Raila Odinga ameendelea kuongoza kwa 50% katika umaarufu huku nafasi ya pili ikishikwa na Naibu Rais, William Ruto aliyepata 25%

> Profesa George Wajackoyah amepata 7%, zilizobaki zimeenda kwa wagombea wengine

Soma - https://jamii.app/UraisKenya

#JamiiForums
🥰8👍2😁1
RWANDA: Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unafanyika Jijini Kigali baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na COVID-19

> Viongozi na Wawakilishi toka Mataifa 54 wanashiriki mkutano huo kuanzia Juni 20 hadi Juni 25, 2022

Soma - https://jamii.app/MkutanoRwanda
👍8
Mwandishi wa Habari wa Urusi, Dmitry Muratov ameuza medali yake ya Amani ya Nobel kwa Dola Milioni 103.5 (Tsh. Bilioni 239.2) ili kusaidia Watoto wa Ukraine walioathiriwa na vita

> Amesema fedha hizo zitapitia katika Akaunti ya UNICEF

Soma - https://jamii.app/AuzaTuzo

#JamiiForums
👍22