JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KUFUTWA KWA VAT KATIKA MAFUTA YA KULA

Waziri wa Fedha amependekeza kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa 0% kwa Wazalishaji wa Mafuta Kula hapa Nchini

Lengo ni kuchochea uzalishaji wa mafuta hususan wakati huu ambao bei imepanda katika Soko la Dunia

Soma - https://jamii.app/BajetiKuuTz

#Bajeti2022 #BajetiKuu
👍23
Katika mwaka 2022/23, Serikali inapanga kutumia Tsh. Trilioni 41.48 kwa Matumizi ya Kawaida na Maendeleo

Kati ya kiasi hicho, Trilioni 26.48 (sawa na 63.8% ya Bajeti) zimetengwa kwa matumizi ya kawaida. Matumizi ya Maendeleo yanatarajiwa kuwa Tsh. Trilioni 15.0 (36.2% ya Bajeti)

#Bajeti2022
👍7
USHURU WA NYWELE BANDIA NA MAJI KUTOKA NJE YA NCHI KUPANDA

Serikali imesema Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka 25% hadi 35% kwenye bidhaa za nywele bandia

Pia, imependekeza kutoza Ushuru wa Forodha wa 60% badala ya 35% kwa mwaka mmoja kwenye maji ya kunywa (Mineral Water)

Soma - https://jamii.app/BajetiKuuTz

#Bajeti2022 #BajetiKuu
👍16
USHURU WA VIFUNGASHIO, NA MABASI YA MWENDO YA MWENDOKASI KUSHUKA

Serikali inatoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa 'Duty Remission' kutoka 25% au 10% hadi 0% kwa mwaka mmoja katika karatasi zinazotumika kama malighafi ya kutengeneza vifungashio

Soma - https://jamii.app/BajetiKuuTz

#Bajeti2022 #BajetiKuu
SERIKALI KUKOPA TSH. TRILIONI 5.78

Dkt. Mwigulu amesema Misaada na Mikopo ya Masharti Nafuu kwa Serikali inatarajiwa kuwa Tsh. Trilioni 4.65 sawa na 11.2% ya bajeti yote huku ikitarajia kukopa Tsh. Trilioni 5.78 kutoka Soko la Ndani

Pia, amesema kuwa Serikali imetenga Tsh. Trilioni 11.31 ya ulipaji wa Deni la Serikali, Tsh. Trilioni 9.83 kwa ajili ya Mishahara na Tsh. Trilioni 5.34 za matumizi mengineyo

Soma - https://jamii.app/BajetiKuuTz

#Bajeti2022 #BajetiKuu
👍13👎3😢2😁1
PAKISTAN: WANANCHI WASHAURIWA KUPUNGUZA KUNYWA CHAI

Waziri Ahsan Iqbal ametoa wito huo akisema, "Tunakopa ili kuagiza Chai, kunywa vikombe vichache kutashusha gharama kubwa za uagizaji"

Akiba ya Fedha za Kigeni ya #Pakistan inaendelea kushuka kwa kasi hivyo kuilazimu Serikali kupunguza gharama kubwa za uagizaji

Soma - https://jamii.app/ChaiPakistan
👍9😁4🤔4🔥1
JamiiForums inatangaza nafasi 10 za Wasimamizi wa Maudhui (Content Managers)

MAJUKUMU: Kusimamia Maudhui ya JamiiForums.com na kuhakikisha Wanachama wanazingatia Miongozo wanaposhiriki Mijadala mbalimbali

Je, unadhani unafaa? Tuma Maombi yako kupitia vacancies @ jamiiforums.com kabla ya kesho Juni 16, 2022.

Kwa Maelezo zaidi - https://jamii.app/NafasiKaziJF
👍5
DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Baadhi ni kutoka damu ukeni baada ya kujamiiana, kutoka damu wakati ambao siyo wa hedhi, kutoka maji yenye harufu mbaya sehemu za siri, maumivu wakati wa kujamiiana, haja ndogo na kubwa kutoka ovyo

Soma - https://jamii.app/SarataniYaKizazi
👍7
Ukatili dhidi ya Wazee unatajwa kuwa tatizo kubwa duniani, na kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, Mtu 1 kati ya 6 mwenye umri wa miaka 60 na kuendelea amepitia aina fulani ya ukatili mwaka uliopita

Jitihada kubwa zinahitajika kutatua changamoto zinazowakibili Wazee, zikiwemo zile zinazokiuka #HakiZaBinadamu

Soma - https://jamii.app/WazeeUkatili
👎3👍2🤔1
Ukatili dhidi ya Wazee unaweza kutokea kwa aina mbalimbali ikiwemo;

> Kisaikolojia: Inahusisha udhalilishaji, vitisho, matusi na kutopewa nafasi ya kuamua

> Kimwili: Wanaofanyiwa ukatili huu wanaweza kupigwa na kufanyiwa vitendo vingine kama hivyo vinavyoweza kuwaumiza

> Kifedha: Fedha au mali zao kutumiwa vibaya au kuibwa

Soma zaidi - https://jamii.app/WazeeUkatiliw
👎3👍1
SRI LANKA: Kutokana na hofu ya uhaba wa Chakula, Serikali imeridhia Watumishi wa Umma kutoenda kazini siku ya Ijumaa kwa miezi mitatu ijayo kuwahamasisha kulima

Aidha, uamuzi huo unalenga kuwasaidia wanaopata shida kufika kazini kutokana na uhaba wa Mafuta

Soma - https://jamii.app/SriLankaChakula
👍5🤔1
MSUMBIJI: Umoja wa Mataifa (UN) umesema watu 10,000 wamekimbia makazi yao kutokana na machafuko eneo la Cabo Delgado lenye utajiri wa gesi

Watu saba wameuawa katika ghasia za hivi karibuni kwenye Jimbo hilo ambalo limekuwa na machafuko tangu 2017

Soma - https://jamii.app/MsumbijiMachafuko
👍9👎1
Unapoibiwa au kupoteza simu inashauriwa kutoa taarifa kwa Mtoa Huduma wako

Vilevile, ni muhimu kuwapa taarifa watu wako wa karibu ili kuepuka utapeli unaoweza kufanywa

Zaidi, soma - https://jamii.app/HatuaWiziSimu

#JamiiForums
👍2
KINACHOTOKEA MTANDAONI KILA SEKUNDE 60

Utafiti uliofanywa mwaka 2021 unaonesha ndani ya sekundi 60 kuna wastani wa mambo mengi yanayofanyika Mtandaoni yakiwemo:

> Maudhui ya saa 500 yanaingizwa YouTube. Meseji Milioni 21.1 zinatumwa. Barua Pepe Milioni 197.6 zinatumwa

> Tweets 200,000 zinapostiwa, Stori 695,000 zinapostiwa Instagram, Video 5,000 zinapakuliwa TikTok na Watu Milioni 1.4 wanaperuzi Facebook

#JamiiForums #JFData
👍5
MOROGORO: Daudi Senyagwa amefariki kwa kuteketea na moto huku ufunguo wa nyumba yake ukikutwa nje, usiku wa kuamkia leo Juni 15, 2022 ktk Mtaa wa Seminari, Kata ya Kingolwila

> Uchunguzi wa awali umeonesha kuna viashiria vya mlipuko wa mtungi wa gesi

Soma - https://jamii.app/AfaKwaMoto
😢6👍3👎1
NGORONGORO: Baadhi ya Wakazi toka Hifadhi ya Ngorongoro wameomba kukutana na Serikali ili kutatua changamoto zinazokabili hifadhi hiyo kwa lengo la kuboresha mpango wa matumizi ya hifadhi hiyo

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella alisema Kaya 296 zimejiandikisha ili kuondoka katika eneo hilo leo

> Alisema "Awamu ya kwanza itahusisha mifugo, mali na wao wakazi husika, Kuhusu makazi yao ya Ngorongoro hatutayagusa, watabomoa wao wenyewe kwa hiyari yao"

Soma - https://jamii.app/SakataLaNgorongoro
👎12👍5
MDAU: Kuna Watu wengi ambao wamepata mafanikio ktk fani ambazo hawakuwahi kuzisomea au haikuwa ndoto yao kufanya kazi hizo

> Je, kufanya kazi tofauti na ulichosomea ni matokeo ya maamuzi mabovu kwenye uchaguzi wa kozi (Course)?

Soma - https://jamii.app/KaziUliyosomea

#JFAjira
👍7
YANGA SC BINGWA LIGI KUU TANZANIA BARA 2021/22

Ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Coastal umeifanya Yanga kuwa Bingwa ikiwa imefikisha alama 67 zisizoweza kufikiwa na timu nyingine

Yanga imetwaa Ubingwa ikiwa imebakiza kucheza michezo mitatu

Soma - https://jamii.app/YangaBingwa

#JFSports
👍36💩15👏65🔥3😢1
UN YASHAURI UHAMISHO WA WAMASAI NGORONGORO KUSITISHWA

Wataalamu wa Masuala ya Haki za Binadamu Umoja wa Mataifa (UN) wametoa wito kwa Serikali ya Tanzania kusitisha Mipango ya kuwahamisha Watu waishio Loliondo na eneo la Hifadhi la Ngorongoro

Wameshauri Serikali kuanza mazungumzo ili kutambua changamoto zilizopo na misingi bora ya utatuzi wake

Wametoa rai kwa Mamlaka kuonesha uwazi kwa kukubali maombi ya uchunguzi kutoka nje

Soma - https://jamii.app/UNTanzania
👍30👏1
CHINA YAAHIDI KUENDELEA KUIUNGA MKONO URUSI

Rais wa China, Xi Jinping ametoa ahadi hiyo baada ya kuwasiliana na Rais wa Urusi, Vladimir Putin kwa njia ya simu

> Xi amesema wataunga mkono Urusi katika masuala ya Uhuru na Usalama

Soma - https://jamii.app/ChinaRussia

#JamiiForums
👍23🔥3🤔3👏2👎1