JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Profesa Mkumbo ameshauri Barabara ya Dar-Moro-Dodoma ipanuliwe ili kupunguza ajali kutokana na wingi wa magari yanayotumia njia hiyo

> Asema hayo akipotoa heshima za mwisho kwa Profesa Honest Ngowi na Innocent Mringo waliofariki kwa ajali

Soma https://jamii.app/DarDomBarabara
USA: Baada ya Mwigizaji, #WillSmith kumpiga kibao Mwigizaji mwenzake, #ChrisRock ktk Tuzo za #Oscar2022, Waandaaji wa tuzo hizo 'The Academy' wameanza rasmi mchakato wa kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yake

> Uamuzi rasmi utatolewa Aprili 18, 2022

Soma: https://jamii.app/Academy
RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA BARAZA LA MAWAZIRI

George Simbachawene atakuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera na Uratibu

> Damas Ndumbaro anakuwa Wizara ya Katiba na Sheria

> Pindi Hazara Chana anakuwa Waziri wa Maliasili na Utalii

#JamiiForums
Rais wa #Marekani, Joe Biden ametangaza kutoa pipa milioni 1 za mafuta kila siku kwa kipindi cha miezi sita ili kupunguza bei ya mafuta

> Baadhi ya Wataalamu wamesema mafuta hayo hayatapunguza vya kutosha athari za bei ghali kwenye Soko la Kimataifa

Soma https://jamii.app/MafutaMarekani
PAKISTAN: Upinzani umemtaka Waziri Mkuu, Imran Khan ajiuzulu wakati Bunge likisubiri Aprili 4, 2022 kupiga kura inayoweza kumtoa Madarakani

> Analaumiwa kwa kushindwa kusimamia Uchumi uliosababisha mfumuko wa bei na kupanda kwa nakisi ya bajeti

Soma - https://jamii.app/KhanImpeach
URUSI: Rais Vladmir Putin amesema atasitisha mikataba ya kusambaza Mafuta Barani #Ulaya, ikiwa Mataifa hayo yatakataa kununua bidhaa hiyo kwa fedha ya Urusi

> Pia, Putin ametaka malipo yote yafanyike kupitia Benki za Urusi

Soma https://jamii.app/UrusiMafuta

#RussiaUkraineConflict
Mdau ameandika sababu za Biashara ndogo kutofanya vizuri kuwa ni kutofanya utafiti wa soko, kukosa Muongozo bora wa Biashara, kuweka biashara sehemu isiyo sahihi

> Anasema sababu nyingine ni kutaka kujitanua kabla hujajitosheleza

Soma https://jamii.app/BiasharaNdogo

#JFUchumi
MDAU: UTARATIBU WA KISHERIA KUNUNUA ARDHI ILI KUEPUKA UTAPELI

Ardhi iliyosajiliwa: Mjue anayekuuzia, muulize maswali kuhusu umiliki wake, muombe Kivuli cha Hati (kopi) ujiridhishe umiliki na uhalali wa nyaraka, jadili masharti ya mauziano, andaa mikataba kabla ya kusaini na mshirikishe wakili, lipa na usaini

Ardhi isiyosajiliwa: Mjue anayeuza, ione ardhi, shirikisha Serikali za Mtaa, ukioneshwa ardhi rudi tena kwa muda wako, muhoji muuzaji kuhusu eneo, akuoneshe Nyaraka za Umiliki, uliza Maafisa Ardhi wa Wilaya, Saini Mkataba, mtumie Wakili

Soma - https://jamii.app/NunuaArdhiKisheria
KINANA ACHAGULIWA KUWA MAKAMU MWENYEKITI CCM BARA

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wamemchagua Abdulrahman Kinana kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwa kura za ndiyo 1,875

Wajumbe waliopiga kura ni 1,875, hakuna za hapana wala zilizoharibika

Soma - https://jamii.app/KinanaMKiti
#Siasa
Ukaguzi wa CAG ulibaini Mamlaka za Serikali za Mitaa 18 pamoja na baadhi ya Taasisi za Serikali hazina Sera na Mipango Mikakati ya Mifumo ya TEHAMA

Pia, Sera na Mipango Mikakati iliyopo haiendani na Kanuni za Fedha katika Taasisi zilizokaguliwa

#JamiiForums #Accountability
KENYA: Mahakama imetangaza kuwa mabadiliko ya Katiba yaliyopendekezwa kabla ya Uchaguzi Mkuu ni kinyume cha Sheria

> Mahakama imesema, ikithibitika kuwa Rais hakuwa na ushawishi ktk mapendekezo hayo Bunge linaweza kuyawasilisha tena

Soma https://jamii.app/KatibaYazuiliwa
#JFSiasa
URUSI: Gavana wa Jimbo la Belgorod, Vyacheslav Gladkov ameishutumu #Ukraine kushambulia ghala la mafuta la Belgorod na kujeruhi Watu wawili

> Hii ni mara ya pili kwa eneno hilo kupata shambulio ambapo awali Ghala la Silaha lililipuliwa

Soma https://jamii.app/GhalaUrusi
#JamiiForums
UNFPA: NUSU YA MIMBA DUNIANI HAZIKUTARAJIWA

Inakadiriwa, kila mwaka mimba milioni 121 hupatikana Duniani kote

> 60% ya mimba hizo zinatolewa huku 45% ya zinazotolewa, zikitolewi katika njia zisizo salama na zinasababisha vifo kwa 5% hadi 13%

Soma https://jamii.app/RipotiMimbaDuniani
DAR: WANAOTUMIA MJAMZITO FEKI KUIBA PIKIPIKI WAKAMATWA

Watuhumiwa hao 8 hushirikiana, 1 hujifanya mjamzito na kukodi pikipiki kuelekea kwa wengine 3 ambao hupora

> 1 hung'oa GPRS na wengine 3 hutengeneza na kudurufu kadi, kisha kuuza pikipiki

Soma https://jamii.app/MtandaoBodaboda
DROO YA KOMBE LA DUNIA: UHISPANIA, UJERUMANI KUNDI MOJA

Droo ya kupanga Makundi ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 imefanyika leo huko Doha, Qatar

Katika droo hiyo, Senegal imewekwa Kundi moja na Uholanzi huku Morocco ikiwa Kundi moja na Ubelgiji na Croatia

#JFSports #WC2022
Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limetoa wito kwa #Ukraine kuanzisha uchunguzi wa uhalifu wa kivita, baada ya kuibuka mkanda wa video unaowaonesha Wanajeshi wakiwapiga risasi miguuni wafungwa 3 wa kivita wa Urusi

Soma - https://jamii.app/UhalifuKivitaUkr
#HumanRights
RAIS SAMIA: Tunasifiwa kwamba maboresho tuliyoyafanya Awamu ya Tano yamekuza heshima ndani ya Utumishi wa Umma. Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na 'Simba wa Yuda' ambaye ulikuwa ukimgusa sharubu anakurarua

Soma - https://jamii.app/SamiaHeshimaWoga

#JFSiasa
HIFADHI YA MAFUTA: Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji imesema kiasi cha mafuta kilichopo kuanzia Aprili 1, 2022 ni lita za Petroli zinazotosha kwa siku 27, Dizeli kwa siku 19, Mafuta ya Taa kwa siku 108 na Mafuta ya Ndege kwa siku 35

Soma - https://jamii.app/MafutaEwura
UFARANSA: Rais Emmanuel Macron ameahidi kutoa Euro bilioni 20 sawa na Tsh. Trilioni 51 ili kudhibiti ongezeko la bei ya umeme na gesi

> Ameahidi kuwapatia marupurupu yasiyokatwa kodi watumishi wa umma na kupambana na mfumuko wa bei

Soma https://jamii.app/BeiUfaransa
#Ukraine imetangaza kuchukua udhibiti wa eneo zima la #Kyiv baada ya Wanajeshi wa Urusi kuondoka ktk baadhi ya Miji ya karibu

Watu 280 walizikwa kaburi la pamoja katika Mji wa #Bucha huku Watu 200 wakiuawa katika Mji wa #Irpin

Soma - https://jamii.app/KyviRescue
#RussiaUkraineWar