JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NIGERIA: Watu waliojihami wamelishambulia kwa risasi treni iliyokuwa na abiria 1,000 ktk Jimbo la Kaduna na kuwateka baadhi ambao idadi haijafahamika

> Watu wengi wanatumia treni baada ya mashambulio kuwa mengi kwa njia nyingine za usafiri

Soma https://jamii.app/TreniNigeria
Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais Uhuru Kenyatta ameidhinisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa Mwanachama wa EAC

> Maamuzi hayo yamefikiwa Machi 29, 2022 ktk Mkutano wa 19 wa Wakuu wa Nchi Wanachama

Soma https://jamii.app/DRCinEAC
Jeshi la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya #Congo limesema limewakamata wanajeshi wawili wa #Rwanda waliohusika na shambulizi lililofanyika na Waasi wa M23

> UN imekuwa ikishutumu Rwanda na #Uganda kwa kuunga mkono M23 ingawa Serikali zote zinakanusha

Soma https://jamii.app/RwandaDRC
#SOMALIA: Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa tishio la baa la njaa nchini humo lililosababishwa na ukame linaweza kusababisha vifo 330,000 vya watoto walio chini ya miaka mitano

> Hii ni kutokana na vipindi vitatu vya mvua kupita bila mvua

Soma https://jamii.app/UkameSomalia
SHINYANGA: Imeripotiwa, Watoto 10 wenye umri wa miaka 6-12 toka Kata ya Mhongolo, Ngogwa na Wendele wamebakwa, kulawitiwa na wengine wakiliwa na fisi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita

> Hayo yalitokea walipoagizwa dukani nyakati za usiku

Soma - https://jamii.app/Ukatili
ZANZIBAR: Makamu wa Kwanza wa Rais, Othman Masoud Othman amesema Sheria ya Uchochezi inatoa fursa ya kutumika vibaya na Vyombo vinavyosimamia Sheria

> Ameongeza, wakati wa kuifanyia mapitio ili kulinda Uhuru wa Kujieleza na wa Habari nchini umefika

Soma https://jamii.app/Uhuru
NAIROBI: Kupanda kwa bei ya mafuta ya kupikia na viazi mviringo kumefanya Wafanyabiashara waache kuuza chipsi kutokana na kupata hasara

> Nchi nyingi za Afrika zinakumbana ongezeko la bei linalotokana na Vita ya #Ukraine na #Urusi

Soma https://jamii.app/NairobiChipsi
MAREKANI: Serikali imewatahadharisha raia wake walioko #Urusi kufuata Sheria za nchi hiyo au kuondoka mapema iwezekanavyo kutokana na vitisho vya kunyanyaswa au kutengwa na Jeshi la Urusi

Soma https://jamii.app/WamarekaniOnyo

#JamiiForums #RussiaUkraineConflict
LIBYA: VISA VYA UKIUKWAJI HAKI VYASHAMIRI TANGU OKTOBA 2021

Matukio yaliyoshamiri ni vitisho dhidi ya Wanaharakati, mashambulizi dhidi ya Mawakili na Majaji na ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu dhidi ya Wahamiaji, Wanawake na Wafungwa

Soma https://jamii.app/LibyaCrisis
#Democracy
SERIKALI: Kuna ongezeko la watu wenye dalili za homa, kukohoa, mafua, kubanwa kifua na maumivu ya mwili kuanzia Desemba 2021 hadi Machi 25, 2022 na ongezeko hili limetokea kwa kipindi kama hiki kwa kwa miaka 3 mfululizo

Aidha, kuna uwepo wa Mafua Makali (Influenza), utafiti umefanyika katika Hospitali 18 za Mikoa 14 na 3% ya sampuli zilionekana kuwa na Virusi vya Influenza A vinavyosababisha Mafua Makali na Nimonia (Pneumonia)

Soma - https://jamii.app/HomaMafua
#JamiiForums #Afya
CAG: Hadi kufikia Juni 30, 2021, Deni la Serikali lilikuwa Tsh. 64.52 trilioni ikilinganishwa na Tsh. 56.76 trilioni mwaka uliopita hivyo kuna ongezeko la Tsh. 7.76 trilioni, sawa na 13.7%

> Deni la Serikali bado ni himilivu

#JamiiForums #RipotiYaCAG #CAG
Dkt. Charles Kichere (CAG): Kwa Vyama vya Siasa ADC, CHAUMA, TLP, UMD walipata Hati Mbaya huku CUF, UDP, SAU wakipata Hati Zenye Shaka

> Demokrasia Makini na AFP tulishindwa kutoa maoni

Soma - https://jamii.app/CAGReport

#JamiiForums #RipotiYaCAG #CAG
RAIS SAMIA: Kama kuna Waziri ambaye anaendesha Wizara ambayo Mashirika yake hayana bodi, sitomwelewa

> Rais ameongea hayo wakati anapokea Ripoti ya CAG na Ripoti ya TAKUKURU kwa mwaka 2020/2021, leo Machi 30, 2022 Ikulu Chamwino, Dodoma

#JamiiForums #RipotiYaCAG #CAG
Rais Samia: Serikali za Mtaa bado kuna upotevu mkubwa wa Mapato, endelea kusimamia. Kuna watu wamefariki, walifukuzwa au kuacha kazi lakini inaonyesha wanalipwa

> Inno (Innocent Bashungwa) usione shida kufukuza walioiba, usiwalee. Ukiwaonea huruma utalia wewe

#RipotiYaCAG #CAG
CAG alibaini tangu lilipoanza zoezi la utolewaji wa Vitambulisho vya Taifa 2012/13, ni Wananchi 5,621,350 tu ndio waliopata vitambulisho sawa na asilimia 26 ya Wananchi 21,692,122 walioandikishwa NIDA hadi kufikia Juni, 2020.

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #WAJIBU
Rais Samia: Tozo ya Tsh. 100 iliyokuwa imeondolewa kwenye mafuta irejeshwe kwa sababu hesabu zake tayari zilikuwa zimepigiwa kwenye bajeti

> Kwa mwenendo wa upandaji wa Bei ya Mafuta Duniani, kuondoa tozo hiyo ni kuikosesha Serikali mapato

Soma - https://jamii.app/Tozo

#JamiiForums
Rais Samia: Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani bado hakiko vizuri, ndio sababu ya CAG kukutana na matatizo mengi

> Baadhi ya Wakaguzi wa Ndani hushirikiana na Watu wa Manunuzi ili kujua mbinu za kuchepusha fedha za Serikali

Soma https://jamii.app/InternalAudits

#JamiiForums #RipotiYaCAG #CAG
DR-CONGO: Waasi wa M23 waiangusha Helkopta ya Umoja wa Mataifa Wilayani Rutshuru-Kivu Kaskazini na kusababisha vifo vya Wanajeshi Walinda Amani 8

> M23 wamelilaumu Jeshi la DRC kwa kuwashambulia ndipo wao walipojibu wakaiangusha helkopta hiyo

Soma https://jamii.app/WalindaAmani
TAKUKURU: Kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka tumetaifisha mali zenye thamani ya Tsh. bilioni 1.2, tumeweka zuio la fedha kiasi cha Tsh. milioni 495.5 na mali zenye thamani ya Tsh. bilioni 2.6

> Pia, tumefanikiwa kuokoa Tsh. bilioni 29.3

Soma https://jamii.app/Takukuru
NAIBU WAZIRI (KATIBA NA SHERIA): Watanzania waipe muda Katiba iliyopo iangaliwe maeneo yanayokera ili iimarishwe, haina tatizo lolote isipokuwa wanaoitafsiri hutoa maana tofauti

> Amesema Katiba hii ni kama Kitabu cha Dini, kila mmoja anatafsiri yake

Soma https://jamii.app/Katiba