JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#DigitalRights: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imewaonya wanaofanya vitendo vya udhalilishaji kwa Wanawake Mitandaoni, ikisema kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria za Nchi na kunaweza kusababisha kutozwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja

Soma > https://jamii.app/TCRA
DODOMA: Rais Samia amesema kwa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23, Serikali itaongeza fedha kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ili wapunguze muda wanaotumia ktk Shughuli za Uzalishaji kwa kuwa shughuli hizo zinapunguza muda wa Shughuli za Medani

Soma https://jamii.app/UzalishajiMajeshi
RAIS SAMIA: HATUWEZI KUAJIRI WATU WAPYA KILA MWAKA

Amesema β€œHaina maana kama Mtu ana cheo akabaki Ofisini hana kazi. Nina hakika kuna Watu wanazurura kwenye korido za Ofisi hawana kazi"

Ameongeza β€œMsitulazimishe kuajiri Watu wapya kwasababu Watu wengi wamepanda vyeo vinginevyo mtanifanya sasa nisipandishe”

Soma - https://jamii.app/SamiaKaziMwaka
Rais Samia Suluhu amelitaka Jeshi la Magereza kulinda maeneo yake ili kuepuka migogoro na amekosoa tabia ya Askari Magereza kugawiana maeneo kiholela

> Pia, amelitaka Jeshi hilo kutenga maeneo yatakayotumika kama zawadi kwa Wastaafu wa Magereza

Soma https://jamii.app/ArdhiMagereza
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Misamaha ya Wafungwa huenda kwa matukio maalum, ukitoa misahama mingi Magereza yatakosa nguvukazi

> Asema ni vyema nguvu ielekezwe kwny kupunguza Mahabusu kwa kuwa hawafanyi kazi na wako idadi sawa na Wafungwa

Soma https://jamii.app/MisamahaWafungwa
AQABA, JORDAN: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa ktk Mkutano wa Kujadili Usalama eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika amesema Tanzania itaendelea kuisaidia Msumbiji kupambana na Ugaidi

> Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Samia kwenye mkutano huo

Soma - https://jamii.app/TZUgaidi
DAR: Wafanyakazi wa Kiwanda cha Pepsi (SBC LTD) Dar es Salaam, wameiomba Serikali kusimamia maslahi yao wakidai kuwepo kwa madhila ikiwemo kufanya kazi bila mikataba, udhalilishaji kazini na dhuluma ya maslahi

Soma - https://jamii.app/AjiraTZ
#JamiiForums #Ajira
πŸ‘1
MDAU: MTOTO WA KIUME NAYE ANA HISIA, ACHA KUMKATAZA KULIA

Tabia hii inawafanya Watoto wakue ktk misingi ya kuamini Watoto wa kiume hawatakiwi kulia/kuumia

Wanapokua hujikuta wakibeba mambo mengi Moyoni na kushindwa kuhimili Msongo wa Mawazo

Soma https://jamii.app/CryingBoys
#Malezi
ULAYA YAKATAA KUNUNUA GESI KWA FEDHA YA KIRUSI

Rais wa #Ufaransa, Emmanuel Macron amepuuzia takwa la Urusi kutaka Mataifa ya Ulaya kununua Gesi kwa Fedha ya Kirusi

Amesema Urusi inafanya hivyo ili kukwepa vikwazo kutokana na uvamizi wake #Ukraine

Soma - https://jamii.app/UrusiGesi
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA WAZO LA BIASHARA

1. Chagua wazo unalolipenda na kulimudu: Kanuni mojawapo ya kufanikiwa ni kupenda kile unachokifanya

2. Zingatia upatikanaji wa Fedha: Hakikisha wazo unalolichagua utaweza kupata Fedha za kutosha ili kulitekeleza

3. Angalia uhitaji wa Soko: Unapoangalia uhitaji wa soko utachagua Biashara ambayo itauzika

Soma - https://jamii.app/BiasharaWazo
#Business
JE, WAJUA KUHUSU β€˜SAA YA DUNIA’?

Tangu 2007 Dunia hutumia Jumamosi ya Mwisho ya Machi kuadhimisha Saa ya Dunia, ambapo taa za umeme huzimwa kwa saa 1 kuanzia Saa mbili na nusu hadi saa tatu na nusu usiku

> Hii hufanywa kutambua umuhimu wa Asili

Soma https://jamii.app/EarthHour
TWAHA KIDUKU AMTWANGA MKONGO, ALEX KABANGU

Bondia wa Tanzania, Twaha Kassim amempiga kwa point Bondia wa DR-Congo, Alex Kabangu katika pambano la round nane

> Kwa Ushindi huo, Twaha amejitwalia mkanda wa UBO-Super Middle Weight ambao ulikuwa wazi

Soma https://jamii.app/TwahaVsKabangu
UKRAINE: Waandishi wa Habari 12 wamefariki na 10 kujeruhiwa Nchini humo tangu kuzuka kwa Vita mwezi mmoja uliopita

Hadi sasa karibu Wawakilishi wa Vyombo vya Habari 56 wameshambuliwa ikiwa ni pamoja na Vyombo 15 vya kigeni

Soma - https://jamii.app/MediaDeathUkr
#RussiaUkraineWar
KENYA: Rais Uhuru Kenyatta amesema Naibu wa Rais, William Ruto alikuwa akimuhujumu na kusimamia mipango ya kumfanyia hujuma ili ashitakiwe

> Kenyatta amesisitiza Raila Odinga ndiye mtu sahihi kwa Nafasi ya Urais ktk uchaguzi wa mwaka huu

Soma - https://jamii.app/Kenyatta
UFARANSA: Wanafunzi Mjini Paris, wameandamana wakipinga Ujenzi wa Bomba la Mafuta la #Tanzania na #Uganda wakisema ni uharibifu wa mazingira

> Omar Elmawi ambaye ni Raia wa Kenya ameonekana kuwa kinara wa kampeni hiyo ya #StopEACOP

Soma https://jamii.app/BombaLaMafuta
BIDEN ATOA KAULI KALI KWA PUTIN, IKULU YAINGILIA KUPOZA MAKALI

Rais wa Marekani, Joe #Biden amesema Rais Putin hatakiwi kuendelea kuwepo Madarakani

Ikulu ya Marekani imefafanua kuwa Biden hakumaanisha kushawishi mabadiliko Urusi

Soma - https://jamii.app/PutinBiden

#JamiiForums
UNYANYASAJI WAFANYAKAZI PEPSI: UCHUNGUZI WAANZA

Serikali imekiri kutambua taarifa za madai ya unyanyasi na madhila kwa wafanyakazi wa Kiwanda cha #Pepsi (SBC LTD) Jijini Dar

Ukaguzi na uchunguzi unaendelea kiwandani hapo

Soma - https://jamii.app/UtuKazini
#JamiiForums #HumanRights
#KENYA: WASIOJULIKANA WAZIDI KUUA, IDADI YAFIKA 29

Miili miwili iliyopatikana ikielea Mto Yala imefikisha idadi ya Maiti za Watu 29 wanaodaiwa kuuawa tangu Oktoba 2021

Mwili mmoja umetobolewa Macho huku mwingine ukiwa umefungwa mfuko Kichwani

Soma - https://jamii.app/KenyaMauaji
#Iraq imejenga ukuta kwenye mpaka wake na #Syria ili kuzuia wanajihadi wa kundi la Islamic State kuingia

Ukuta umejengwa Ninawi, eneo la #Sinjar na una urefu Kilometa 12 na Mita 3.5 kwenda juu. Ujenzi ulianza 2018 na haitambuliki lini utakamilika

Soma - https://jamii.app/UkutaIS
πŸ‘1
TANZIA: PROF. NGOWI AFARIKI DUNIA

Prof. Honest Ngowi ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe akiwa na Dereva wake wamefariki kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Mlandizi, Pwani wakiwa njiani kuelekea Morogoro

> Ajali imetokea Machi 28, 2022 asubuhi

Soma https://jamii.app/ProfNgowi
πŸ‘1