JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#UGANDA: Mahakama imetoa hati ya kumkamata Mwandishi wa Vitabu, Kakwenza Rukirabashaija kwa kutofika Mahakamani

Alitoroka Nchi baada ya kushtakiwa kwa makosa ya kumtusi Rais Yoweri Museveni na mwanaye, Jenerali Muhoozi Kainerugaba

Soma - https://jamii.app/KakwenzaLawsuit
#FreeSpeech
#UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky ameomba watu Duniani kuandamana kupinga Operasheni ya #Urusi Nchini Ukraine iliyoanza Februari 24, 2022

> Zelensky amesema kuunga mkono Ukraine ni kuunga mkono Uhuru na Maisha

Soma https://jamii.app/WorldProtest
#JamiiForums #RussiaUkraineConflict
MODERNA KUOMBA KUTUMIKA KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 6

Itawaomba wadhibiti wa Marekani na Ulaya, kuidhinisha dozi 2 ndogo kwa Watoto chini ya Miaka 6

Watoto milioni 18 Nchini Marekani walio chini ya Miaka 5, ndio kundi la umri ambalo halijapata Chanjo

Soma https://jamii.app/ModernaBabies
BOTSWANA YAKATAA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI NA TANZANIA

Chama cha Soka cha Botswana (BFA) kimesema Tanzania iliomba kucheza Michezo 3 huku viwango vya FIFA vikiwa ni michezo 2

> BFA imesema mchezo huo wa 3 usingekuwa na umuhimu kwao

Soma > https://jamii.app/TFFFIFA
#Sports
πŸ‘1
BELEDWEYNE, SOMALIA: Shambulio la Bomu la kujitoa mhanga la Wanamgambo wa Al-Shabaab limesababisha vifo vya watu 15 akiwemo Mbunge, Amina Mohamed Abdi

> Baadhi ya ripoti zinaonesha idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa kuliko inayotajwa sasa

Soma https://jamii.app/BomuMhanga
#JamiiForums
KENYA: Wizara ya Afya nchini humo imetangaza kuisha kwa muda wa matumizi kwa zaidi ya dozi 800,000 za #COVID19 aina ya #AstraZeneca

> Wizara hiyo imesema kuanzia sasa itakuwa inapokea dozi zenye miezi 4 kabla ya muda wa kuisha matumizi

Soma https://jamii.app/Kenya800k
#JamiiForums
#GHANA: Rais Nana Akufo-Addo na Mawaziri wake wamepunguza mishahara yao kwa 30% ili kupunguza matumizi ya Serikali

Safari za nje kwa Maafisa wa Serikali na uagizaji wa Magari umesitishwa ili kupambana na athari za vita ya Urusi na #Ukraine

Soma - https://jamii.app/30Mishahara
#JFLeo
UNCTAD ilikadiria #Uchumi wa Dunia kukua kwa 3.6% Mwaka 2022 ila kutokana na vita ya Urusi na #Ukraine Uchumi utapungua kwa 2.6%

Ripoti inasema kiwango cha uharibifu wa Kijeshi kutadhoofisha afueni iliyoanza kupatikana baada ya #COVID19

Soma - https://jamii.app/VitaUchumi
#Economy
πŸ‘1
MICHEZO: Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Yusuph Singo amesema Serikali ina imani na Bondia Twaha Kiduku ktk pambano lake na Alex Kabangu wa DRC litakalofanyika Machi 26, 2022 Mkoani Morogoro

Soma https://jamii.app/KidukuMach26
#JFSports
Msanii wa Filamu, Steven Mengele (Steve Nyerere), leo Machi 25, 2022 ametangaza kujiuzulu nafasi ya Usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT)

Amesema β€œNimejiuzulu kwasababu sioni kama hizi kelele zina tija kwa Taifa. Nimeamua kuachia”

Soma - https://jamii.app/SteveResigns
#Sanaa
Je, Unafahamu kwanini Kwenye usafirishaji haramu wa Binadamu wasafirishaji huwapeleka mbali waathirika ikiwemo kuwavukisha mipaka ya Mkoa au Nchi?

Lengo la kufanya hivi ni ili kumtenganisha Mwathirika na Mazingira aliyoyazoea. Ni vigumu kwa Waathirika kutafuta msaada kama hawajui Jiografia, Lugha, Utamaduni na mpangilio wa Mazingira mapya ili waendelee kunyonywa

Soma - https://jamii.app/BoardersHumanTraff
#HumanTrafficking
#DigitalRights: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imewaonya wanaofanya vitendo vya udhalilishaji kwa Wanawake Mitandaoni, ikisema kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria za Nchi na kunaweza kusababisha kutozwa faini, kufungwa jela au vyote kwa pamoja

Soma > https://jamii.app/TCRA
DODOMA: Rais Samia amesema kwa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23, Serikali itaongeza fedha kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ili wapunguze muda wanaotumia ktk Shughuli za Uzalishaji kwa kuwa shughuli hizo zinapunguza muda wa Shughuli za Medani

Soma https://jamii.app/UzalishajiMajeshi
RAIS SAMIA: HATUWEZI KUAJIRI WATU WAPYA KILA MWAKA

Amesema β€œHaina maana kama Mtu ana cheo akabaki Ofisini hana kazi. Nina hakika kuna Watu wanazurura kwenye korido za Ofisi hawana kazi"

Ameongeza β€œMsitulazimishe kuajiri Watu wapya kwasababu Watu wengi wamepanda vyeo vinginevyo mtanifanya sasa nisipandishe”

Soma - https://jamii.app/SamiaKaziMwaka
Rais Samia Suluhu amelitaka Jeshi la Magereza kulinda maeneo yake ili kuepuka migogoro na amekosoa tabia ya Askari Magereza kugawiana maeneo kiholela

> Pia, amelitaka Jeshi hilo kutenga maeneo yatakayotumika kama zawadi kwa Wastaafu wa Magereza

Soma https://jamii.app/ArdhiMagereza
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Misamaha ya Wafungwa huenda kwa matukio maalum, ukitoa misahama mingi Magereza yatakosa nguvukazi

> Asema ni vyema nguvu ielekezwe kwny kupunguza Mahabusu kwa kuwa hawafanyi kazi na wako idadi sawa na Wafungwa

Soma https://jamii.app/MisamahaWafungwa
AQABA, JORDAN: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa ktk Mkutano wa Kujadili Usalama eneo la Kusini Mashariki mwa Afrika amesema Tanzania itaendelea kuisaidia Msumbiji kupambana na Ugaidi

> Waziri Mkuu amemuwakilisha Rais Samia kwenye mkutano huo

Soma - https://jamii.app/TZUgaidi
DAR: Wafanyakazi wa Kiwanda cha Pepsi (SBC LTD) Dar es Salaam, wameiomba Serikali kusimamia maslahi yao wakidai kuwepo kwa madhila ikiwemo kufanya kazi bila mikataba, udhalilishaji kazini na dhuluma ya maslahi

Soma - https://jamii.app/AjiraTZ
#JamiiForums #Ajira
πŸ‘1
MDAU: MTOTO WA KIUME NAYE ANA HISIA, ACHA KUMKATAZA KULIA

Tabia hii inawafanya Watoto wakue ktk misingi ya kuamini Watoto wa kiume hawatakiwi kulia/kuumia

Wanapokua hujikuta wakibeba mambo mengi Moyoni na kushindwa kuhimili Msongo wa Mawazo

Soma https://jamii.app/CryingBoys
#Malezi
ULAYA YAKATAA KUNUNUA GESI KWA FEDHA YA KIRUSI

Rais wa #Ufaransa, Emmanuel Macron amepuuzia takwa la Urusi kutaka Mataifa ya Ulaya kununua Gesi kwa Fedha ya Kirusi

Amesema Urusi inafanya hivyo ili kukwepa vikwazo kutokana na uvamizi wake #Ukraine

Soma - https://jamii.app/UrusiGesi