JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SHINYANGA: ASKARI ANAYEMLINDA MWEKEZAJI ADAIWA KUUA RAIA KWA RISASI

Cosmas Hamis Kusililwa (25) aliyekuwa akichimba Madini Kijiji cha Mwang’holo, anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi wanaolinda eneo la Kampuni ya El-Hillal Minerals Ltd

Soma - https://jamii.app/PoliceShy
MDAU: KABLA HAUJAPIGA PICHA YA UTUPU, FIKIRIA MADHARA YAKE

Ameshauri Watu kufikiria madhara ya picha hizo kabla ya kupiga na kuzisambaza akisema ni muhimu kutumia Maendeleo ya #Teknolojia kujijenga kiuchumi badala ya kuchapisha picha mbaya

Soma - https://jamii.app/UtupuPicha
#JFLeo
Rais Samia amewataka watanzania washughulike na masuala ya unyanyasaji kuanzia ngazi za familia

> Ametaja changamoto iliyopo ni watu kuongea na kumaliza suala la unyanyasaji kifamilia hali inayofanya unyanyasaji kuendelea kwa Watu wenye Ulemavu

Soma https://jamii.app/Unyanyasaji
Jamii Forums inakualika kushiriki kwenye Mazungumzo ya Demokrasia Nchini #Tanzania kupitia Digitali. Mazungumzo yatafanyika Machi 17, kuanzia saa 3 asubuhi yakiongozwa na Balozi wa #Sweden, Anders SjΓΆberg

Lengo ni kujenga na kubadilishana uzoefu kati ya Viongozi Wakuu kama Wanasiasa, Watumishi wa Umma, Wawakilishi wa Mashirika ya kiraia kuhusu #Demokrasia ya Kidigitali kama njia ya kuimarisha Maendeleo

Ungana nasi kupitia Kurasa zetu za Mitandao ya Kijamii ikiwemo Twitter, #Facebook, Instagram na #Telegram kufuatilia yatakayojiri.

#JamiiForums #Democracy
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii kuweka mkazo katika kushughulikia changamoto za Watu wenye Ulemavu

> Amesema Maafisa hao wanashughulikia Mirathi na migogoro ya Ndoa kwa kuwa shauri likiisha watu hutoa chochote

Soma https://jamii.app/UstawiJamii

#JFLeo
Mazungumzo haya yanatoa fursa ya mjadala wa Umma kuhusu namna #Teknolojia za Kidigitali zinavyoweza kupanua fursa kwa Watanzania kushiriki ipasavyo katika Utawala wa Nchi na jinsi Serikali inavyoweza kutoa motisha kufikia Azma hiyo

Dhana ya Mazungumzo ya #Demokrasia ni juhudi za kufanya Demokrasia kuwa thabiti, na kuchangia katika Malengo ya Maendeleo Endelevu.

#JamiiForums #Democracy #HumanRights
HAITI: Madaktari, Wauguzi na Wahudumu wengine wa Sekta ya #Afya wamefanya mgomo kupinga wimbi la Utekaji nyara uliokithiri kwa Watu wa Sekta hiyo

Waliotekwa 2021 ni 655, ambapo Serikali inasema idadi inaweza kuwa kubwa zaidi

Soma - https://jamii.app/DrsStrikeHaiti
#HumanRightsViolations
KIGOMA: Kituo cha Sheria na #HakiZaBinadamu (LHRC) kimelaani mauaji ya Juma Ramadhan (35) aliyepigwa risasi na Askari wakati vurugu zikidhibitiwa Uwanja wa Lake Tanganyika

Kimetoa wito wa kuundwa Tume Huru ya uchunguzi

Soma - https://jamii.app/KgmPolice

#HumanRights #JamiiForums
HANDENI, TANGA: AJALI YAUA WATU WANNE NA KUJERUHI 37

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema Basi dogo la Abiria aina ya Coaster iligonga Toyota Hiace na watembea kwa miguu na kusababisha vifo vya watu wanne na majeruhi 37

Soma - https://jamii.app/TangaAjali

#JFLeo
Tanzania ni miongoni mwa Nchi zinazokua kwa kasi katika Masoko ya Kidigitali Barani Afrika. Idadi ya Watumiaji wa Huduma za Intaneti imeongezeka kutoka milioni 28 Machi 2021 hadi milioni 30 Februari 2022, sawa na ongezeko la asilimia 7.1.

Mazungumzo ya Machi 17, 2022 kuhusu Demokrasia ya Kidigitali Nchini #Tanzania yanalenga kutoa Jukwaa kwa Watendaji wa Serikali na wasio wa Serikali ili kuonesha mwelekeo wa Demokrasia kupitia #Teknolojia na changamoto zake

#JamiiForums #Democracy #HumanRights
ULIPOKUWA MTOTO ULITAKA KUFANYA KAZI GANI?

Swali 'Unataka kufanya kazi gani?' ni la kawaida kuulizwa ukiwa Mtoto, na wakati mwingine unaweza kuwa na ndoto za kuwa fulani Maishani mwako

Ukiwa Mtoto ulitaka kazi gani, na sasa unafanya nini?

Mjadala > https://jamii.app/KaziMtoto
Jopo la Wazungumzaji litahusisha hadhira inayowakilisha Serikali, Mashirika ya kiraia na Wabunifu.

Wadau wakuu watazungumza kuhusu hali ya sasa ya Demokrasia ya Kidigitali Nchini #Tanzania pamoja na matarajio yake. Kuangazia mafanikio yaliyopatikana na changamoto kupitia #Teknolojia za Kidigitali ili kukuza Serikali iliyo wazi na ushiriki hai wa Wananchi.

#JamiiForums #Democracy #DigitalSpaces
KUMBUKIZI YA MWAKA MMOJA YA KIFO CHA MAGUFULI

Hayati John Pombe Magufuli alifariki Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo β€˜Atrial Fibrillation’ ktk Hospitali ya Mzena, Dar es Salaam

> Rais Samia Suluhu ataongoza shughuli ya Kumbukizi ya Mwaka 1 itakayofanyika Chato, Mkoani Geita
Yanayojiri katika Mazungumzo ya Demokrasia Nchini Tanzania kupitia Digitali yanayoendelea hivi sasa

Mazungumzo haya yanaongozwa na Balozi wa Sweden hapa Nchini, Anders SjΓΆberg

Fuatilia > https://jamii.app/DemocracyTalk

#DemocracyTalkTz
Ungana nasi katika Mazungumzo ya Demokrasia Nchini #Tanzania kupitia Digitali yanayolenga kujenga na kubadilishana uzoefu kuhusu #Demokrasia ya Kidigitali kama njia ya kuimarisha Maendeleo

Zaidi, tembelea > https://jamii.app/DemocracyTalk

#DemocracyTalkTz