JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Rais Samia Suluhu Hassan leo, Machi 15, 2022 amewaapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa #Tanzania Nchini #Malawi na Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe

Hafla ya uapisho imefanyika Viwanja vya Ikulu, Chamwino, Dodoma

Soma - https://jamii.app/UapishoPolepole
#JFLeo
UN: VITA YA URUSI NA #UKRAINE INAWEZA KUSABABISHA UHABA WA CHAKULA DUNIANI

Umoja wa Mataifa umesema Nchi nyingi Afrika zinategemea ngano kutoka Mataifa hayo, na vita itasababisha uhaba

Tayari Burkina Faso, Somalia na Yemen zinahangaika kulisha Raia

Soma https://jamii.app/NganoUN
BIASHARA: MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUTOA HUDUMA NZURI KWA WATEJA

1. Mthamini Mteja kuliko Pesa: Pesa ni ujira anaopewa Mtu baada ya kutatua tatizo la Mteja

2. Elewa hitaji la Mteja: Mteja anapofika katika Biashara yako hakikisha unafahamu na kuelewa vyema anahitaji nini (kuwa Msikivu)

3. Jifunze Lugha nzuri kwa Mteja: Usijibu Wateja kwa lugha ya mkato au kukejeli. Kuwa na utulivu unapozungumza na Mteja na mpe ufafanuzi anaohitaji.

Soma - https://jamii.app/HudumaWateja
#Biashara
MALEZI: MAMBO YANAYOWEZA KUATHIRI MAENDELEO YA MTOTO KIMASOMO

1. Matatizo ya Kisaikolojia: Matatizo haya hutokana na kubakwa, kulawitiwa, kupigwa, kunyimwa Chakula

2. Matatizo ya Kifamilia: Kuna Familia ambazo kila siku ni Ugomvi, fujo za Ulevi, au hata Unyanyasaji mwingine kama Utumikishaji wa Watoto pamoja na Mazingira Duni ya kuishi

Soma - https://jamii.app/MasomoWatoto
#Malezi #Parenthood
USHAURI: NAMSAIDIAJE MTOTO WANGU KUACHA TABIA YA WIZI?

Mdau anasema Mtoto wake yuko Darasa la 6 na ana tabia ya Wizi uliokithiri

Ameshamwadhibu ila haijasaidia. Anaiba Nyumbani, Shuleni, kwa Majirani na hata kwa Wageni wanaofika Nyumbani

Anauliza: Je, anakosea wapi kwenye Malezi? Atumie mbinu gani kumsaidia Mtoto?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/MtotoMwizi
#Malezi
KIGOMA: SHABIKI WA MPIRA AFARIKI BAADA YA KUPIGWA RISASI NA ASKARI

Kamanda wa Polisi Mkoani humo, James Manyama amesema tukio hilo lilitokea Machi 14, 2022 kufuatia vurugu katika mchezo wa soka, ambapo Askari alifyatua risasi wakati akijihami

Soma - https://jamii.app/PoliceKgm
#YEMEN: Mashirika ya Misaada ya Umoja wa Mataifa yamesema Watu wapatao 160,000 wamo hatarini kukabiliwa na uhaba mkubwa wa Chakula

Hali ni mbaya Nchini Yemen kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu 2014 Waasi wa Kihouthi walipoteka Mji Mkuu

Soma - https://jamii.app/Njaa160kYemen
πŸ‘1
Ili kuweza kutuma Maombi ya nafasi hizi tembelea - https://jamii.app/NafasiAjira
#JamiiForums
URUSI: Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa #Canada, Melanie Joly na Waziri wa Ulinzi wa Canada, Anita Ananda hawataruhusiwa kuingia #Urusi

> Katazo limeandikwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Urusi

Soma https://jamii.app/MawaziriCanada
#KENYA: Wajumbe wa Chama cha UDA wamemuidhinisha Naibu Rais, William Ruto kuwania kiti cha Urais ktk Uchaguzi Mkuu Agosti 2022

Ruto atamenyana na Kiongozi wa Muungano wa Azimio la Umoja, Raila Odinga anayeungwa Mkono na Rais Uhuru Kenyatta

Soma - https://jamii.app/RutoUrais
#JFLeo
Mwaka 2019/20, CAG alikagua Taasisi 263 ambazo ni Wizara, Idara na Wakala wa Serikali Kuu na kutoa Hati za Ukaguzi 260 ikilinganishwa na 294 kwa Mwaka 2018/19

Kupungua kwa Hati za Ukaguzi ni kutokana na CAG kushindwa kufanya ukaguzi kwa Balozi na Misheni 43 kutokana na Ugonjwa wa UVIKO-19

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #WAJIBU
TANGA: AJALI YAUA, MASHUHUDA WA AJALI NAO WAGONGWA

Watu kadhaa wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali iliyotokea Sindeni, Wilayani Handeni Mkoani humo Machi 16, 2022

DC wa Handeni, Siriel Mchembe amethibitisha kutokea ajali hiyo

Soma > https://jamii.app/TangaAjali
Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema Rais wa Marekani, Joe Biden na Maafisa wengine 12 wamepigwa marufuku kuingia Nchini humo

Vikwazo hivyo pia vitamuhusu Katibu Mkuu Kiongozi, Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi, Lloyd Austin

Soma - https://jamii.app/RussiaSanctionBiden
#RussianUkraineWar
JE, WAJUA: MSANII HUTAKIWA KULIPA TSH. 50,000 AKIENDA NJE YA NCHI KWA KAZI ZA SANAA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema Sheria zinawataka Wasanii kulipa Tsh. 50,000 kupata Kibali kila wanapoenda nje ya Nchi kufanya kazi za kisanaa

Soma https://jamii.app/KibaliSanaa

#Burudani
Zaidi ya Wanajeshi 10 wa #Kenya ambao ni sehemu ya kikosi cha Walinda Amani wa AU wameuawa kwa kilipuzi kilichotegwa eneo la Gedo karibu na mpaka wa Kenya na #Somalia

Vilipuzi vimedaiwa kuwekwa na kundi la Al-Qaeda lenye uhusiano na Al-Shabaab

Soma - https://jamii.app/KenyaWanajeshi
πŸ‘1
SHINYANGA: ASKARI ANAYEMLINDA MWEKEZAJI ADAIWA KUUA RAIA KWA RISASI

Cosmas Hamis Kusililwa (25) aliyekuwa akichimba Madini Kijiji cha Mwang’holo, anadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na Polisi wanaolinda eneo la Kampuni ya El-Hillal Minerals Ltd

Soma - https://jamii.app/PoliceShy
MDAU: KABLA HAUJAPIGA PICHA YA UTUPU, FIKIRIA MADHARA YAKE

Ameshauri Watu kufikiria madhara ya picha hizo kabla ya kupiga na kuzisambaza akisema ni muhimu kutumia Maendeleo ya #Teknolojia kujijenga kiuchumi badala ya kuchapisha picha mbaya

Soma - https://jamii.app/UtupuPicha
#JFLeo
Rais Samia amewataka watanzania washughulike na masuala ya unyanyasaji kuanzia ngazi za familia

> Ametaja changamoto iliyopo ni watu kuongea na kumaliza suala la unyanyasaji kifamilia hali inayofanya unyanyasaji kuendelea kwa Watu wenye Ulemavu

Soma https://jamii.app/Unyanyasaji
Jamii Forums inakualika kushiriki kwenye Mazungumzo ya Demokrasia Nchini #Tanzania kupitia Digitali. Mazungumzo yatafanyika Machi 17, kuanzia saa 3 asubuhi yakiongozwa na Balozi wa #Sweden, Anders SjΓΆberg

Lengo ni kujenga na kubadilishana uzoefu kati ya Viongozi Wakuu kama Wanasiasa, Watumishi wa Umma, Wawakilishi wa Mashirika ya kiraia kuhusu #Demokrasia ya Kidigitali kama njia ya kuimarisha Maendeleo

Ungana nasi kupitia Kurasa zetu za Mitandao ya Kijamii ikiwemo Twitter, #Facebook, Instagram na #Telegram kufuatilia yatakayojiri.

#JamiiForums #Democracy
Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii kuweka mkazo katika kushughulikia changamoto za Watu wenye Ulemavu

> Amesema Maafisa hao wanashughulikia Mirathi na migogoro ya Ndoa kwa kuwa shauri likiisha watu hutoa chochote

Soma https://jamii.app/UstawiJamii

#JFLeo