JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#UKRAINE: Brent Renaud (50), Mwandishi wa Habari wa #Marekani aliyekuwa akifanyakazi nchini humo ameuawa kwa kupigwa risasi na Wanajeshi wa #Urusi Mjini Irpin

> Pia, Waandishi wa Hahari wengine wawili wamejeruhiwa akiwemo mmoja toka Italia

Soma https://jamii.app/BrentRenaud
#JFLeo
MDAU: KUMPA MTOTO UHURU WA KUJIELEZA KWENYE FAMILIA SIO UZUNGU

Ushiriki wa Mtoto kwenye masuala yanayomuhusu unapatikana pale anapopewa nafasi ya kutoa mawazo kuhusu maamuzi ya Maendeleo yake

Familia zinazowapa Watoto uhuru wa kujieleza na kutoa maoni yao kuanzia kwenye umri mdogo humuandaa Mtoto katika kutafuta Haki zake za Msingi mbele ya Jamii kubwa zaidi

Soma - https://jamii.app/FreeSpeecChild
#FreeSpeech
UPDATE: Watu wanne wamefariki dunia huku wengine 35 wakijeruhiwa katika ajali ya basi la Kilimanjaro Express lililopindukia korongoni eneo la Senjele Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe

Ajali hiyo imetokea baada ya Dereva kuwa kwenye mwendokasi

Soma - https://jamii.app/SongweAjali

#JFLeo
Ripoti ya Uwajibikaji Serikali Kuu na Mashirika ya Umma 2019-2020 imeonesha Miradi iliyosajiliwa na TIC (Kituo cha Uwekezaji) kwa Mwaka 2015/16 ni 420, wakati kwa Mwaka 2019/20 ilisajiliwa Miradi 219. Idadi hiyo imeshuka kwa asilimia 48

#JamiiForums #JFUwajibikaji #Accountability #WAJIBU
MDAU: WATOTO WENGI SIKU HIZI HAWALELEWI KATIKA MIKONO YA WAZAZI WAO

Anasema kwa Dunia ya sasa Watoto wengi siku hizi hawapati nafasi ya kukua wakiwa katika Mikono ya Wazazi wao. Wengi hupelekwa Shuleni mapema zaidi, wengine wakiwa hawajaweza hata kuongea vizuri

Anasema usimkimbize Mtoto Shuleni mapema akiwa bado haelewi wala hawezi kujisaidia kwa lolote. Mlee kwanza apate ufahamu wa kujitunza

Mjadala - https://jamii.app/ShuleWatoto5
#Malezi #Parenthood
👍1
NAPE: KULAZIMISHA WATUMISHI WA SERIKALI KUTUMIA TTCL HAIKUWA SAHIHI

Waziri wa Habari, Nape Nnauye amekosoa kulazimisha Watumishi wa Serikali kuwa na laini za TTCL, akisema Mtu anaweza kuwa na laini ya TTCL na asiitumie

Soma - https://jamii.app/KulazimishaLaini

#DigitalRights #JFLeo
SERIKALI: MUSWADA WA SHERIA YA ULINZI WA DATA UKO HATUA ZA MWISHO

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema “Hii ni Sheria muhimu vinginevyo uwekezaji utakuwa mgumu. Sio kwasababu kulikuwa na kurekodi rekodi Watu, hapana ni kwasababu ya kutunza Faragha.”

Soma - https://jamii.app/MuswadaFaragha
#DataProtection
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametangaza punguzo la ada ya Maombi ya Leseni ya Maudhui ya Mtandaoni kutoka Tsh. 100,000 hadi Tsh. 50,000 na ada ya Mwaka kutoka Tsh. 1,000,000 hadi Tsh. 500,000

Ameongeza "Tumeondoa Leseni kwa watoa maudhui kupitia Redio na Runinga pindi wakitaka kutoa Maudhui hayo hayo Mitandaoni"

Soma - https://jamii.app/LeseniMaudhui

#JamiiForums
MWANZA: RAIA WALALAMIKA KUTOPEWA AJIRA MRADI WA SGR

Wananchi wa Fela Wilayani Misungwi wamesimamisha msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kulalamikia kunyimwa ajira, na baadhi kuombwa rushwa katika Mradi wa Mwanza - Isaka

Soma - https://jamii.app/AjiraSGR

#JFLeo
PROF. MKUMBO: KILA RAIS HUTATUA CHANGAMOTO NA KUTENGENEZA NYINGINE

Mbunge wa Ubungo asema ni kawaida kwa Rais wa kutatua changamoto anazozikuta lakini huwa wanazitengeneza nyingine

Amesema Rais Samia ametatua changamoto ya Kidiplomasia na Uwekezaji

Soma https://jamii.app/MatatizoRais
PROF. KITILA: CHANGAMOTO YA ELIMU NI KUTENGENEZA WAHITIMU WASIOAJIRIKA

Asema Elimu ya sasa inatengeneza Wahitimu ambao hawawezi kutengeneza Ajira na wanakosa Stadi za Ufundi

Ameeleza, ni muhimu Mwanafunzi kuwa na Taaluma, Stadi na Maarifa ya Msingi

Soma https://jamii.app/MatatizoRais
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amteua Humphrey Polepole kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Malawi

Shamsi Vuai Nahodha ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la JMT na Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe

Wataapishwa Ikulu Dodoma Machi 15, 2022

Soma https://jamii.app/BaloziMalawi
#JFLeo
NEHEMIA MCHECHU ARUDISHWA NHC

- Rais Samia amemteua Nehemia Mchechu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba ya Taifa (NHC)

- Mchechu aliondolewa katika nafasi hiyo Juni 2018 ikielezwa ni kutokana na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili

Soma https://jamii.app/NehemiaNHC

#JFLeo
PROF. KITILA: SUALA SIO KATIBA MPYA BALI LINI TUTAREJEA MCHAKATO

Amesema Nchi ilishapiga hatua kwani ilishakubaliana Mwaka 2014 na kuunda Tume ya #Katiba Mpya

Asema swali la kujiuliza ni lini mchakato utarejea kwani Rasilimali nyingi zimetumika

Soma - https://jamii.app/Katiba2014
JE, NI RAHISI WANAWAKE KUSAMEHE USALITI KULIKO WANAUME?

Wadau ndani ya JamiiForums.com wanasema mara nyingi ni rahisi Mwanamke kumsamehe Mwanaume kosa la usaliti kuliko Mwanaume kumsamehe Mwanamke

Nini mawazo yako kwenye hili?

Mjadala zaidi - https://jamii.app/UsalitiMapenzi
UJERUMANI: SAFARI ZA NDEGE ZAFUTWA KWA MGOMO WA WAFANYAKAZI

Wafanyakazi wa Usalama wamefanya mgomo wa kudai nyongeza ya mishahara

Mgomo huo unafanyika wakati Mashirika ya Ndege yakiyumba kutokana na vita ya #Ukraine na ongezeko la Bei ya Mafuta

Soma - https://jamii.app/FlightsCancelGRM
MSAIDIZI WA SABAYA ADAI ALIKUWA ANAISHI KAMA MATEKA

Watson Mwahomange ambaye ni Mtuhumiwa katika Kesi ya Uhujumu Uchumi amesema alipigwa kila alipotuhumiwa kitu

Asema Sabaya ni mtu hatari na kuomba Mahakama impe ulinzi atakaporudi Mahabusu

Soma - https://jamii.app/SabayaHatari
Ripoti ya CAG ya 2019/20, inaonesha kuongezeka kwa idadi ya mapendekezo yanayotolewa na CAG kwa Miaka mitatu mfululizo kutoka 4,282 Mwaka 2016/17 hadi kufikia 5,483 kwa 2018/19

Mwaka 2018/19 mapendekezo yaliyotekelezwa kikamilifu yalikuwa 1,608 (28%), Mwaka 2017/18 yaliyotekelezwa kikamilifu ni 1,474 (31%) na Mwaka 2016/17 yaliyotekelezwa ni 1,459 (3%).

#JamiiForums #Accountability #JFUwajibikaji #WAJIBU
Rais Samia Suluhu Hassan leo, Machi 15, 2022 amewaapisha Humphrey Polepole kuwa Balozi wa #Tanzania Nchini #Malawi na Waziri Kindamba kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe

Hafla ya uapisho imefanyika Viwanja vya Ikulu, Chamwino, Dodoma

Soma - https://jamii.app/UapishoPolepole
#JFLeo
UN: VITA YA URUSI NA #UKRAINE INAWEZA KUSABABISHA UHABA WA CHAKULA DUNIANI

Umoja wa Mataifa umesema Nchi nyingi Afrika zinategemea ngano kutoka Mataifa hayo, na vita itasababisha uhaba

Tayari Burkina Faso, Somalia na Yemen zinahangaika kulisha Raia

Soma https://jamii.app/NganoUN