JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KAMATI YAUNDWA KUCHUNGUZA MADAI YA SAMAKI KUFA KWA SUMU MTO MARA

Ni baada ya picha zinazodaiwa kuwa ni za Mto Mara zikionesha Samaki waliokufa kusambaa Mitandaoni, huku ikielezwa hali hiyo ni kutokana na kemikali za sumu zinazotoka Migodini

Soma - https://jamii.app/SumuMara
#JFLeo
KOREA KUSINI: MPINZANI ACHAGULIWA KUWA RAIS

Yoon Suk-yeol amemshinda mpinzani wake, Lee Jae-myung wa Chama cha Demokrasia kwa chini ya 1%

Waliojitokeza kupiga kura ni 77% ya wanaostahili. Wagombea wote walionekana kutopendwa muda wa kampeni

Soma - https://jamii.app/RaisKoreaKusini
KAYA 86 ZILIZO TAYARI KUHAMA NGORONGORO ZAJITOKEZA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea majina 453 toka Kaya 86 zilizokubali kuondoka hifadhini

> Amesema Serikali imetenga Kilometa za Mraba 400,000 Wilayani Handeni kwaajili ya zoezi hilo

Soma https://jamii.app/NgorongoroHiari
NDUGULILE: KUTOZA KODI BIASHARA ZA MTANDAONI MAPEMA KUTAUA AJIRA NYINGI

Mbunge wa Kigamboni, amesema Tanzania iko nyuma ktk biashara mtandao hivyo ni muhimu kuzilea

> Amesema hayo baada ya mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira kusema biashara zenye mauzo zaidi ya Tsh. Milioni 4 zitozwe kodi

Soma https://jamii.app/ecommerceTax
πŸ‘1
UPDATES: Serikali ya #Ukraine imesema Raia wa Mji wa #Mariupol wameshindwa kuondoka baada ya Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda kushindwa kutekelezwa

Jitihada za kupelekea Chakula, Maji na Dawa kwenye Mji huo zimeshindikana

Soma - https://jamii.app/RaiaMariupol

#JFLeo
Kampuni ya Meta inayomiliki Mtandao wa Kijamii wa #Facebook na #Instagram imelegeza sera yake ili kuruhusu maneno ya chuki dhidi ya Urusi

Wataruhusu sentensi za chuki kama β€˜Death to Russian Invaders’ lakini hawataruhusu chuki dhidi ya raia

Soma - https://jamii.app/FacebookPolicy
#JFLeo
Kumekuwa na mapungufu mbalimbali katika Utekelezaji wa Bajeti. Taasisi mbalimbali za Serikali zilifanya matumizi nje ya Bajeti Mwaka 2019/20

Matumizi ya Fedha za Umma nje ya Bajeti yanapelekea uwezekano wa kuwepo Ubadhirifu na vitendo vya Rushwa

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji #Accountability
TRA: TUNAWAFUATILIA WATEJA WA WANAOFANYA BIASHARA MTANDAONI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wanaofanya Biashara Kidigitali wafike Ofisini kujisajili

Yasema kuna wenye Maghala makubwa ya bidhaa ila hawana Maduka na TIN

Soma - https://jamii.app/DigitalBusiness
#DigitalRights
MAREKANI YAOMBWA KUTOWEKA VIKWAZO KWA WATOA HUDUMA YA INTANETI URUSI

Asasi za Kiraia zimesema hatua ya Kampuni zinazotoa huduma ya Intaneti kuondoka Nchini Urusi kutokana na vikwazo inaweza kuathiri wenye Mawazo na Misimamo tofauti

Soma - https://jamii.app/InternetRussia
#DigitalRights
Wizara ya Afya Nchini #Kenya imelegeza masharti ya kupambana na #COVID19 ikiwemo kuondoa ulazima wa kuvaa Barakoa kwenye maeneo ya umma

Pia, Wagonjwa wasio na dalili hawatatengwa na hakutakuwa na ulazima wa kukaa Karantini kwa wenye virusi

Soma - https://jamii.app/COVID19Mask
#UVIKO3
JE, WAJUA? - KUTUMIA UGONJWA KUOMBA FEDHA BILA KIBALI NI KOSA KISHERIA

Wakili wa Kujitegemea, Justine Kaleb anasema Mgonjwa akitaka kuombaomba Mtaani lazima apate kibali maalum cha Serikali au Taasisi zinazotambua Ugonjwa wake

Kufanya tofauti na hivyo adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya Tsh. milioni tano au vyote kwa pamoja

Soma - https://jamii.app/Ombaomba
#JFLeo
TANZIA: RAIS RUPIAH BANDA AFARIKI DUNIA

> Aliyewahi kuwa Rais wa #Zambia, Rupiah Banda amefariki dunia akiwa na miaka 85. Aligundulika kuwa na saratani ya utumbo

> Banda ni Rais wa 4 wa Zambia aliyechaguliwa kidemokrasia na aliongoza kuanzia mwaka 2008 hadi 2011

Soma https://jamii.app/RupiaBanda

#RIPBanda
SERIKALI YAPENDEKEZA BAJETI YA TSH. TRILIONI 41 MWAKA 2022/23

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tsh. Trilioni 28, sawa na 70% ya Mapato itatokana na makusanyo ya ndani

Bajeti itagusa Maendeleo ya Jamii hususani Sekta ya Kilimo

Soma - https://jamii.app/MapendekezoBajeti

#JFLeo
UNHCR: WATU MILIONI 12.5 WAMEATHIRIKA NA MZOZO WA #URUSI NA #UKRAINE

Shirika la Umoja wa Mataifa Linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) limeripoti watu zaidi ya milioni 4.4 wamelazimika kuhama makazi yao

> Walioathirika zaidi ni Wazee, Watoto na Wanawake

Soma https://jamii.app/AthariMzozo
CCM: MWENENDO WA JESHI LA POLISI UCHUNGUZWE

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM imeagiza Serikali ilichunguze Jeshi la Polisi baada ya Wananchi kupoteza imani nalo

> Imedaiwa, Polisi hutenda majukumu bila kufuata Mwongozo wa Kisheria (PGO)

Soma https://jamii.app/PolisiCCM
RAIS SAMIA AAGIZA KANUNI ZA MIKUTANO YA SIASA KUANDALIWA

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge kwa kushirikiana na TLS pamoja na ZLS kuandaa Kanuni zitakazoelekeza namna ya kufanya mikutano ya hadhara ya Vyama vya Siasa

Soma - https://jamii.app/AgizoMikutanoSiasa

#JFLeo
MAKONDA: KUNA BAADHI YA MAAFISA WA POLISI WANALIPAKA TOPE JESHI LA POLISI

Aliyekuwa RC wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema baadhi ya Polisi hulinda Wafanyabiashara wakubwa wanaodhulumu mali za watu

> Ameunga mkono mienendo ya Polisi kuchunguzwa

Soma https://jamii.app/MakondaPolisi
MAKONDA: GHALIB USINILAZIMISHE KUSEMA UOZO WENU. WALIO NYUMA YENU NAWAJUA

Kauli hiyo ya Paul Makonda ni baada ya Wakili wa Ghalib Said Mohamed (GSM) kuweka vielelezo vinavyoonesha Ghalib ndiye Mmiliki wa kiwanja kilichopo Regent Estate Kinondoni

Soma - https://jamii.app/JFSiasa
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
DAR: KIWANDA CHA GSM CHAWAKA MOTO

> Kiwanda cha kutengeneza magodoro kinachomilikiwa na Kampuni ya GSM kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kimeungua moto

Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana kwa sasa

Soma - https://jamii.app/MotoGSM

#JamiiForums #JFLeo