JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KILIMANJARO: Grace Pima anashikiliwa na Polisi akidaiwa kumchoma Moto Mtoto wake wa Miaka Mitano Mdomoni na Puani kwa kosa la kutukana

Alifanya unyama huo Februari 28 na kumfungia Mtoto ndani kwa Saa 48 akimtibu kwa Dawa za Asili.

Soma - https://jamii.app/MotoMtoto
#UkatiliMtoto
#ZANZIBAR: Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) imetangaza kuanzia Machi 9, Petroli itauzwa Tsh. 2,459, Dizeli Tsh. 2,500 na Mafuta ya Taa Tsh. 1,811 kwa Lita

Ongezeko limetokana na kupungua thamani ya Shilingi na tozo za Serikali

Soma https://jamii.app/MafutaZanzibar
UPDATE: Ofisi ya #HakiZaBinadamu ya Umoja wa Mataifa inasema Raia wa #Ukraine wapatao 474 wameuawa tangu uvamizi wa Urusi kuanza, lakini inahofiwa idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi

Ukraine imesema Vikosi vya Urusi vimeharibu takriban Hospitali 61

Soma - https://jamii.app/VifoUkraine
Mapungufu kadhaa kwenye ulipaji wa Mishahara kwa Watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliainishwa na CAG Mwaka 2019/20

Miongoni mwao ni Mamlaka 46 kushindwa kuwasilisha Makato ya Kisheria ya Mishahara yenye thamani ya Tsh. Bilioni 5.08 kwa Taasisi husika zikiwemo TRA (Tsh. Milioni 149.9) na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Tsh. Bilioni 3.92)

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji #Accountability
KAMPUNI ZAENDELEA KUSITISHA BIASHARA URUSI

Coca-Cola, Starbucks, Pepsi na McDonald's zasitisha Biashara kufuatia uvamizi wa #Ukraine

Kumekuwepo na shinikizo kutaka Kampuni za Biashara kuchukua hatua kama ishara ya kupinga mateso wanayopata Raia

Soma - https://jamii.app/BiasharaUrusi
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Hussein Kattanga amesema ili kuikuza #Teknolojia ktk Uchumi wa Kidigitali ni lazima kuwa na mazingira wezeshi

Amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapaswa kuwa Mlezi badala ya Mdhibiti/Ubabe

Soma - https://jamii.app/MleziTCRA

#DigitalRights
MDAU: TAIFA LINALOONGOZWA KIDEMOKRASIA LAZIMA LIFUATE MISINGI YAKE

Anasema Nchi inayoongozwa kwa Misingi ya Demokrasia inalazimika kutoa nafasi kwa Wananchi kumchagua Kiongozi wanayemhitaji bila udanganyifu wowote

Mihimili mikuu inayojenga Serikali inapaswa kufanya kazi kwa Uhuru bila kuingiliana kimajukumu

Soma - https://jamii.app/DemocracySOC

#StoriesOfChange
JE, WAJUA?: Kwenye Mgogoro wa #Ukraine na Urusi baadhi ya Watu wamebainika kuunga mkono vita kwa kutumia herufi ‘Z’ ikimaanisha ‘Za popedy’ yaani ushindi

Mwanariadha wa Kirusi, Ivan Kuliak anakabiliwa na kesi ya kinidhamu kwa kuonesha herufi hiyo

Soma - https://jamii.app/RussiaZ
SERIKALI YATOA TAHADHARI YA HOMA YA MANJANO

Waziri Ummy Mwalimu aagiza Maafisa wa Afya Mipakani kuhakikisha Wasafiri kutoka Nchi zenye Maambukizi wana vyeti vya Chanjo

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari na kujua dalili za Ugonjwa huo

Soma - https://jamii.app/HomaManjano

#JFLeo
RIPOTI: BELARUS YAENDELEZA UKANDAMIZAJI DHIDI YA WAPINZANI NA VYOMBO VYA HABARI

Ripoti hiyo ya UN inaweka wazi ukiukwaji unaofanywa kwa wanaojaribu kutekeleza Haki zao za Msingi, lakini pia inaonesha namna wahanga wanavyoshindwa kupata Haki zao

Soma - https://jamii.app/UNRipotiBelarus
MANENO GANI YA KIINGEREZA UMEYATAMKA VISIVYO KWA KIPINDI KIREFU?

Wadau wa Jukwaa la Lugha ndani ya JamiiForums.com wametolea Mifano maneno ambayo wameyatamka visivyo kwa muda mrefu yakiwemo; Entrepreneur, Advertisement, Schedule, Determine, Mishandle na Frying Pan

Maneno gani ya Kiingereza yamewahi au yanaendelea kukusumbua hadi sasa?

Mjadala zaidi > https://jamii.app/ManenoEnglish
MBEYA: KIJANA AKAMATWA NA POLISI AKISAFIRISHA VIPODOZI VYENYE SUMU

Polisi wanamshikilia Emmanuel Msigala (42) kwa kusafirisha vipodozi vyenye viambata Sumu vilivyopigwa marufuku

Mtuhumiwa ni mnunuzi, msafirishaji na muuzaji wa bidhaa hizo

Soma - https://jamii.app/Vipodozi
#Afya
LINDI: Mama mmoja Mkazi wa Ruangwa anatuhumiwa kumuua Mwanaye wa Mwaka mmoja kwa kumnywesha sumu ya kuua Magugu

Alifikia hatua hiyo baada ya Mama mkwe wake kukataa kukaa na Mtoto akimwambia bado mdogo, anastahili kuendelea kunyonya

Soma - https://jamii.app/SumuMtoto
#UkatiliWatoto
UKRAINE: Hospitali ya Wajawazito ya Mariupol imeshambuliwa na Wanajeshi wa #Urusi katika shambulio la anga na kusababisha majeruhi 17

> Inaelezwa kuwa, waliojeruhuwa ni Wafanyakazi na Wajawazito huku Watoto wakiwa salama

Soma https://jamii.app/17Wajeruhiwa
#RussiaUkraineCrisis
Leo Machi 10, 2022 ni Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani, inayolenga kuongeza ufahamu kuhusu Afya ya Figo ili kuziba pengo la uelewa wa Ugonjwa wa Figo. Mwaka huu, Kaulimbiu ni "Afya ya Figo kwa Wote"

Zipo njia mbalimbali za kupunguza hatari ya kupata Ugonjwa wa Figo zikiwemo kufanya mazoezi, kuzingatia Lishe na Mitindo bora ya Maisha

Soma - https://jamii.app/WKD22

#WorldKidneyDay2022
MAREKANI: Rais Joe Biden atasaini agizo la Serikali la kutaka utafiti ufanyike dhidi ya Crypto-Currency ili kubaini madhara yake kwny uchumi na usalama kwa wanaowekeza kwenye fedha hizo

> 16% ya Wamarekani wamewekeza katika Crypto-Currency

Soma https://jamii.app/CryptocurrencyMarekani
MBEYA: Jeshi la Polisi linamshikilia Daniel William (Diwani wa Kata ya Iganzo) kwa tuhuma za kumshambulia kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili Shadrack Zacharia ambaye ni Mpigapicha, akimtuhumu kumpiga picha bila idhini yake

Soma - https://jamii.app/DiwaniPolisi

#JamiiForums
MDAU: UELEWA WA JAMII NI KIKWAZO KWA WATANZANIA KUCHEZA SOKA LA KULIPWA

Anasema Jamii haielewi umuhimu wa Michezo na kupeleka kutokuwa na Mazingira wezeshi

Kuna uhaba wa vituo vya kulea vipaji na kusababisha kuwa na Wachezaji wachache Kimataifa

Soma - https://jamii.app/SokaChangamoto
Kutotayarisha Hesabu na kuziwasilisha kwa CAG kwa Ukaguzi ni uvunjifu wa Kifungu cha 25 cha Sheria ya Fedha za Umma No. 21 ya Mwaka 2001

Mwaka 2019/20 Mashirika ya Umma 11 hayakuwasilisha Hesabu kwa CAG kwa ajili ya Ukaguzi

#JamiiForums #WAJIBU #Accountability #JFUwajibikaji
UKRAINE: WATU WAZIKWA KWENYE KABURI LA PAMOJA

Jiji la Mariupol limechimba mfereji wa mita 22 na kuzika maiti zikiwa ktk mifuko ya plastik. Idadi kamili ya waliouawa haijafahamika

> Tangu Jumanne raia hawana huduma ya maji wala umeme.

Soma https://jamii.app/KaburiMoja