JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MDAU: TAKA NGUMU ZICHAKATWE KUWA MBOLEA ASILIA KUOKOA MAZINGIRA

Anasema tatizo la taka ngumu ni kubwa, na jitihada za Mamlaka pamoja na wadau mbalimbali bado hazijakidhi ukubwa wa tatizo lililopo

Anashauri maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kutupa taka ngumu kuwekwa viwanda vya mbolea, malighafi ya chuma na plastiki badala ya kuchoma moto taka na kusababisha uchafuzi wa mazingira na athari za Kiafya

Soma - https://jamii.app/TakaNgumuSOC

#StoriesOfChange
Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani (Machi 8, 2022), inaelezwa Wanawake na Wasichana wanakumbana na athari kubwa zaidi za Mabadiliko ya TabiaNchi, kwani yanazidisha ukosefu wa #UsawaWaKijinsia

Kukosekana Usawa wa Kijinsia ni miongoni mwa changamoto kubwa inayohitaji suluhisho la haraka, na ni wakati wa kuchukua hatua

Soma - https://jamii.app/UsawaWanawake

#IWD2022
NAMIBIA: Wanafunzi 23 wamefanikiwa kurejeshwa Nchini humo kutoka #Ukraine na Wizara ya Elimu imewataka kujiunga na Vyuo vya ndani ili kuendelea na Masomo

Wanafunzi takribani 13,000 wa #Ghana, Somalia na #Nigeria wamekwama Mjini Sumy

Soma - https://jamii.app/WanafunziNamibia

#RussiaUkraine
MTWARA: ATUHUMIWA KUUA MKE NA KISHA KUMZIKA KWENYE SHIMO

Shaibu Kauselela anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumuua Amina Mtausi (40) kwa kumpiga na kitu kizito, baadaye kumzika kwenye Shamba na kupanda Mpunga ili kupoteza ushahidi

Soma - https://jamii.app/Mtwara

#GBV
URUSI: Baadhi ya raia wameingia Mitaani kupinga hatua ya Nchi yao kuishambulia #Ukraine wakitoa maneno ya β€˜No to War’

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema takriban Watu 3,500 wamekamatwa katika Miji 56 kwa kufanya maandamano

Soma - https://jamii.app/ProtestersRussia
#RussiaUkraineConflict
KUNYIMWA KUJIELEZA NI KUNYIMWA HAKI YA KUSHIRIKI KATIKA MAENDELEO

Ripoti iliyotolewa na Taasisi ya Article 19 Mwaka 2021 inaonesha hali ya #UhuruWaKujieleza/kutoa mawazo binafsi imekuwa ikidorora katika maeneo mengi duniani

Bila Uhuru wa Kuzungumza haiwezekani kamwe kutatua matatizo ambayo yanahitaji kutatuliwa

Soma - https://jamii.app/UhuruKujieleza
ETHIOPIA: Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) limeripoti machafuko ya #Ethiopia kusababisha Watu milioni 2 kukimbia Makazi yao

> Mapigano ya #Tigray yamezibomoa hata kambi za Wakimbizi zilizokuwa Nchini #Eritrea

Soma https://jamii.app/EthiopiaMachafuko

#JFLeo
UPDATES: Serikali ya #Ukraine imependekeza vikwazo vya kibiashara vya kimataifa dhidi ya Urusi ikiwemo kuzuia mafuta ya Taifa hilo ikisema 'Vita viwalishe'

Vikosi vya Moscow vinaushambulia Mji wa #Mariupol na Raia 300,000 wanasubiri kuondolewa

Soma - https://jamii.app/MafutaUrusi
SIMIYU: WATENDAJI WA SERIKALI WAKAMATWA KWA WIZI WA CHUPA ZA DAWA

Watu 12 wakiwamo Watendaji wa Serikali za Mtaa wamekamatwa wakidaiwa kuiba Chupa 434 za Dawa za kuua wadudu wa Pamba zilizotolewa na Serikali kwa Wakulima Wilayani Bariadi

Soma - https://jamii.app/WiziSimiyu

#JFLeo
URUSI YATOA MASHARTI YA KUACHA KUISHAMBULIA UKRAINE

Imeitaka Ukraine kuitambua #Crimea kama sehemu ya #Russia, na Donetsk and Luhansk kama Mataifa huru

Aidha, #Ukraine imetakiwa kubadili Katiba na kukataa kuingia katika kambi yoyote kama NATO

Soma - https://jamii.app/UrusiMasharti
WANAFUNZI WA KITANZANIA WATOKA SALAMA UKRAINE

Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula amesema Wanafunzi wapatao 150 wamevuka salama na kukimbilia nchi za Poland, #Hungary, Romania na #Denmark. 23 wamefanikiwa kurejea Tanzania

Soma - https://jamii.app/WatanzaniaSalama

#JFLeo
#BURUDANI: Watu wengi hasa Vijana wanapenda kuangalia Filamu (#Movies). Filamu hizi huburudisha, huchangamsha na kutoa mafunzo kwa Jamii

Je, ni Filamu gani uliyowahi kuangalia zaidi ya mara moja na bado huichoki?

Mjadala - https://jamii.app/FilamuBurudani

#Entertainment #JamiiForums
SERIKALI: WATU 8 WAFARIKI DUNIA KWA #COVID19 NDANI YA MWEZI MMOJA

Visa vipya 290 viliripotiwa kuanzia Februari 5 - Machi 4, 2022. Wagonjwa 136 walilazwa na 128 kati yao hawakupata chanjo

Idadi ya waliopata dozi kamili ya chanjo Nchini ni 2,664,373

Soma https://jamii.app/8COVID19
#UKRAINE YATAKA ZELENSKY NA PUTIN KUFANYA MKUTANO

Taifa hilo linataka mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Rais Volodymyr Zelensky na Rais wa #Russia, Vladimir Putin likisema linatambua maagizo yote yanatoka kwa Kiongozi huyo

Soma - https://jamii.app/ZelenskyPutin

#RussiaUkraineWar
Machi 8 ni Siku ya Wanawake Duniani

> Tunaungana na Watu wote kuadhimisha Siku hii, na tunawatakia Maadhimisho mema ya Siku ya Wanawake Duniani

#JamiiForums #IWD2022 #InternationalWomensDay
πŸ‘1
Takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zimeonesha idadi ya Vifo vilivyotokana na #COVID19 vimefikia 5,999,158

Nchi nyingi zimelegeza masharti huku Safari na #Biashara zikianza kurejea. Aidha, kupata chanjo bado kunasisitizwa

Soma - https://jamii.app/COVID19Duniani

#UVIKO3
#UGANDA: Gabriel Rwotomiya amefariki kwa kupigwa risasi wakati Polisi wakituliza vurugu za Wanafunzi wa Sekondari Gulu baada ya kuzuiwa kutazama Mechi ya Man City na Man U, Machi 6

Wanafunzi wamerejeshwa Nyumbani na Shule kufungwa kwa muda

Soma - https://jamii.app/Uganda

#JFLeo
Katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipata taarifa za makusanyo ya Mapato katika Halmashauri 135

Alibaini Bilioni 18.77 zilikusanywa kutoka vyanzo mbalimbali, lakini hakuna ushahidi Mapato hayo yaliwasilishwa Benki

#JamiiForums #WAJIBU #JFUwajibikaji #Accountability
Katika kuadhimisha #InternationalWomensDay ni muhimu kuangazia changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuhamasisha jitihada za kukomesha ukosefu wa #UsawaWaKijinsia

Leo, tunasherehekea na kutambua Uongozi, nguvu, uwezo, ujasiri na mchango walionao Wanawake wote katika Jamii

Maadhimisho ya Mwaka 2022 yanabeba Kaulimbiu isemayo, "Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu"

#JamiiForums #BreakTheBias #IWD2022
MDAU: WATUMISHI WAFUNDISHWE NAMNA BORA YA KUTUMIA MIKOPO WANAYOCHUKUA

Anasema Watumishi wa Serikali huvutiwa huchukua Mikopo wakiamini ni ya gharama nafuu hali inayowafanya wawe na madeni hadi wanastaafu

Ameshauri kiundwe chombo maalum cha kudhibiti usimamizi na uendeshaji wa Taasisi zote za Kifedha. Sheria ya Mafao iboreshwe ili kuwezesha Watumishi wanapostaafu wawe wanajengewe Nyumba za Makazi

Soma - https://jamii.app/WatumishiMadeni

#StoriesOfChange