JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UMOJA WA ULAYA (EU) WAPIGA MARUFUKU NDEGE ZA URUSI

Hii inamaanisha Ndege za Urusi hazitoweza kutua, kuruka au kupita juu ya anga la Nchi yoyote ya Umoja huo

Pia, umepiga marufuku Vyombo vya Habari vya Sputnik na Russia Today

Soma https://jamii.app/EURussiaBan

#RussiaUkraineCrisis
#UPDATES - UKRAINE: Shirika la UNHCR limesema idadi ya wanaokimbia Vita Nchini #Ukraine imefikia Watu 368,000

Makadirio ya Jumamosi tu zaidi ya Watu 150,000 wamekimbilia #Poland, na Mataifa mengine ikiwemo #Hungary na #Romania

Soma https://jamii.app/RefugeesUkraine

#RussiaUkraineConflict
DR CONGO: Boti ya mizigo imewaka moto Bandarini na kuua watu 20, huku wengine 11 wakiungua vibaya

Serikali imepiga marufuku abiria kupanda boti za mizigo lakini wengi hutumia usafiri huo kutokana na Miundombinu duni ya Barabara

Soma - https://jamii.app/20DeadDRC

#JamiiForums
MICHEZO: Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeiamuru Urusi kucheza Mechi bila Bendera na Wimbo wa Taifa katika viwanja visivyoegemea upande wowote, ikionya huenda Nchi hiyo ikaondolewa kwenye mashindano ikiwa hali ya #Ukraine haitaimarika

Soma https://jamii.app/FIFARussia

#JFSports
MICHEZO: Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya Chelsea hawajakubali maombi ya Roman Abramovich kukabidhi majukumu ya kuiongoza timu kwa bodi hiyo huku yeye akibaki kuwa Mmiliki

> Inaelezwa, hofu ya Wajumbe hao ni kuonekana wanatumia klabu kwa malengo binafsi

Soma - https://jamii.app/31/Chelsea
UFAHAMU UGONJWA WA POLIO (1)

Unasababishwa na Kirusi cha #Polio kinachoambukizwa kutoka kwa mtu aliyeathirika kwa kunywa/kula Chakula au kinywaji kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya Ugonjwa

Unawaathiri zaidi Watoto chini ya Miaka 5

Soma - https://jamii.app/UgonjwaPolio
RUKWA: Watu saba wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi kwenye maeneo tofauti katika Wilaya za Nkasi na Sumbawanga mkoani Rukwa, Februari 26, 2022

> Matukio yote hayo yametokea wakati watu hao wakiwa shambani

Soma - https://jamii.app/32/RadiYaua

#JamiiForums #JFMatukio
WATALII TAKRIBAN 1,000 KUTOKA UKRAINE WADAIWA KUKWAMA ZANZIBAR

Leila Mohammed Musa, ambaye ni Waziri wa Utalii #Zanzibar amesema wanapanga kuwapeleka Nchi jirani ya #Poland

Taarifa zaidi zitatolewa pindi Balozi wa Ukraine atakapofika Zanzibar leo

Soma - https://jamii.app/WataliiUkraineZNZ
Benki Kuu ya Urusi imetangaza kuongeza kiwango chake cha riba kufikia 20% kutoka 9.5%, ili kukabiliana na hatari ya kushuka kwa thamani ya Fedha na mfumuko wa bei

Pia, imeamuru Kampuni kuuza 80% ya mapato yao ya Fedha za kigeni

Soma - https://jamii.app/RussiaRateSpike

#RussiaUkraineWar
Balozi Dkt. Wilbrod Slaa amekiri kuudhika na maneno 'Mbowe si Gaidi' yanayotolewa na baadhi ya Wananchi kuhusu kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe

> Amesema Wananchi wanatakiwa kuiachia Mahakama kutoa maamuzi

Soma - https://jamii.app/34/Mbowe

#JamiiForums
BULGARIA: Waziri Mkuu, Kiril Petkov asema atamfuta kazi Waziri wa Ulinzi, Stefan Yanev baada ya Kiongozi huyo kusita kuelezea uvamizi wa Urusi dhidi ya #Ukraine kama vita akisisitiza "Waziri wangu hawezi kutumia neno operesheni badala ya vita"

Soma - https://jamii.app/BulgariaMD
SERIKALI YAONDOA TOZO YA TSH. 100 KWENYE MAFUTA

Tozo hiyo kwa kila Lita ya Dizeli, Petroli na Mafuta ya Taa yaondolewa kulinda Wananchi na athari za mabadiliko ya Bei za Mafuta

Bei zimepanda kutokana na sababu kadhaa ikiwemo vita ya Urusi & Ukraine

Soma https://jamii.app/TZTozoMafuta
#BELARUS: RAIS LUKASHENKO AJIONGEZEA MUDA WA KUKAA MADARAKANI

Tume ya Uchaguzi imesema 65% ya Watu waliopiga kura wameridhia mabadiliko ya #Katiba

Mabadiliko yanampa Rais Lukashenko aliyeiongoza tangu 1994 muda zaidi Madarakani na kinga ya Maisha

Soma - https://jamii.app/LukashenkoPower
UKRAINE YASAINI MAOMBI YA KUJIUNGA UMOJA WA ULAYA (EU)

Pia, Rais Volodymyr ameomba Umoja huo uiruhusu #Ukraine ipate Uanachama mapema iwezekanavyo, chini ya Utaratibu Maalum wakati ikijilinda dhidi ya mashambulizi ya Urusi

Soma - https://jamii.app/UkraineEU

#RussiaUkraineCrisis
URUSI YAENDELEA KUISHAMBULIA UKRAINE LICHA YA MAZUNGUMZO

Makombora yaua watu kadhaa #Kharkiv, na ving'ora vya mashambulizi ya anga vimesikika tena katika Mji Mkuu, #Kyiv

Rais Volodymyr asema shambulio la Urusi huko Kharkiv ni uhalifu wa kivita

Soma - https://jamii.app/RussiaAttacks
#BURKINAFASO: JESHI LAIDHINISHWA KUONGOZA KWA MIAKA MITATU

Mkutano wa Kitaifa umepitisha Mkataba utakaoruhusu Utawala wa Kijeshi kuongoza kipindi hicho

Mkutano huo uliidhinisha Hati ambayo baadaye ilisainiwa na Luteni Kanali Henri-Paul Damiba

Soma - https://jamii.app/Jeshi3BurFaso
AFGHANISTAN: Marufuku ya kusafiri nje ya Nchi imetolewa na Serikali ya #Taliban ikilenga kuwakinga Waafghanistan na ugumu wa Maisha nje ya Taifa hilo

Familia ambazo zinahitaji kuondoka zinahitaji kuwa na sababu muhimu kwa Mamlaka ya Uhamiaji

Soma - https://jamii.app/TravelBanTaliban
#HumanRights
Nguvu ya #Demokrasia halisi hutegemea Uhuru na Haki fulani za kimsingi. Uhuru na Haki hizi lazima vilindwe ili kuhakikisha Demokrasia inafaulu

Katika Nchi nyingi Haki za Msingi zinapatikana na kulindwa na #Katiba. Katiba huelezea Miundo na kazi za Serikali pamoja na kutoa Miongozo ya kuunda #Sheria nyingine

Kwa kawaida, Katiba inatakiwa kulindwa dhidi ya kufanyiwa marekebisho na Vigogo wa Serikali pasipo kuwasilisha mabadiliko yoyote kwa Wapigakura kupitia Kura ya Maamuzi/Maoni

#JamiiForums #Democracy
MDAU: OFISI ZA SERIKALI ZIWE NA KIBAO CHA KURIPOTI UZEMBE KWENYE UTOAJI HUDUMA

Apendekeza kuwe na kibao kwenye kila Taasisi inayohudumia Wananchi chenye namba za kuripoti kukitokea Ucheleweshwaji wa Huduma bila sababu za Msingi, Urasimu, na Uzembe wowote ule

Anasema hii itasaidia kuwa na Taasisi zinazofanya Kazi kweli na Wafanyakazi watakuwa hawana longo longo kwenye Utoaji huduma.

Msome - https://jamii.app/UzembeHuduma
#StoriesOfChange #Accountability