JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UPDATES: Mamlaka Nchini #Ukraine zinasema shambulio la Urusi limeua Wanajeshi wapatao 70 kwenye Kitengo cha Kijeshi huko Okhtyrka, Mji ulioko kati ya Kharkiv na Kyiv

Umoja wa Mataifa umesema idadi ya watu waliokimbia Ukraine imefikia 520,000

Soma - https://jamii.app/UrusiUkraine1
UFAHAMU UGONJWA WA POLIO (2)

Ugonjwa huu hauna tiba, na njia kuu ya kuuzuia ni kuwapatia watoto chanjo ya Polio ambayo hutolewa kwa Dozi Nne

Wataalamu wanasema ni muhimu Mtoto akamilishe ratiba ya Chanjo kama inavyotakiwa ili kupata kinga kamili

Soma - https://jamii.app/UgonjwaPolio
LINDI: MGANGA ATUHUMIWA KUMBAKA MWANAFUNZI

Jeshi la Polisi Mkoani humo linamtafuta Mganga wa Kienyeji Juma Salumu maarufu 'Juma Kipanya' anayekabiliwa na tuhuma za kubaka na kumpa ujauzito Mwanafunzi (15) wa Darasa la Saba

Soma - https://jamii.app/LindiMganga
#HumanRightsViolations
URUSI: Kocha wa Klabu ya Lokomotiv Moscow, Markus Gisdol (52), amejiuzulu akipinga uvamizi wa Urusi kwa Ukraine

Asema β€œSiwezi kuwa kwenye uwanja wa mazoezi huko Moscow kufundisha wachezaji wakati umbali wa Kilomita chache yanatolewa maagizo yanayoleta mateso kwa watu”

#JFSports
GENEVA: Zaidi ya Wajumbe 140 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo Machi 1, 2022 walitoka nje ya ukumbi wakikataa kusikiliza hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov

> Wanapinga uvamizi wa Urusi Nchini Ukraine

Soma - https://jamii.app/UNRussia
ADIDAS YAVUNJA USHIRIKIANO NA URUSI

Adidas imesimamisha ushirikiano na Chama cha Soka cha Urusi baada ya nchi hiyo kuvamia Ukraine

Adidas ambayo ni Kampuni ya 2 kwa ukubwa kwa utengenezaji wa vifaa vya michezo, imesitisha udhamini wa jezi za Urusi ulioanza mwaka 2008

#JFSports
GHANA: Kundi la kwanza la Raia wa Ghana wakiwemo Wanafunzi limewasili Accra Nchini humo toka Ukraine ambapo kuna machafuko ya kushambuliwa na Urusi

> Inaelezwa kuwa, wengi wa Raia hao wanaelekea Slovakia, Hungary, Romania na Poland

Soma - https://jamii.app/GhanaUkraine
UTEUZI: Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Yusuph Juma Mwenda kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB). Uteuzi wake unaanza leo Machi 01, 2022

Kabla ya kuteuliwa na Rais Mwinyi, Mwenda alikuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Soma - https://jamii.app/UteuziZRB
MDAU: WAZAZI HUCHANGIA KUHARIBU NDOA ZA WATOTO WAO

Anasema Ndugu/Wazazi wanapokuja kukaa kwa Mtoto wao mwenye Ndoa huwa na Mitazamo tofauti ya namna wanavyotegemea Ndoa iwe na huweza hata kuleta mfarakano na kuharibu Uhusiano uliopo

Ikiwa Ndugu wanakuja kuishi nanyi ni vema kuwe na sababu zinazochangia kukaa na nyie ikiwemo Ugonjwa au Maisha magumu. Lakini kama Mzazi ana nguvu na anaweza kufanya kazi zake za kawaida ni makosa kuishi kwa Mwanao aliyeoa/aliyeolewa

Msome - https://jamii.app/WazaziNdoaMtoto
#Maisha #Mapenzi
πŸ‘1
VISA NA MASTERCARD ZAFUNGIA TAASISI ZA FEDHA ZA URUSI

- Zimezifungia Taasisi hizo kutumia mifumo ya huduma zake ikiwa ni sehemu ya vikwazo kwa Urusi

- Pia, zimeahidi kutoa Dola za Kimarekani Milioni 2 kila moja kwa ajili ya kusaidia Ukraine

Soma https://jamii.app/VisaMastercard-Ur

#JFLeo
FC SPARTAK MOSCOW: TUMETOLEWA EUROPA KWA SABABU ZISIZO ZA KIMICHEZO

Klabu hiyo ya Urusi iliyotolewa Ligi ya Europa kutokana na Urusi kuvamia Ukraine, imesema hatua hiyo inasikitisha

Imesema β€œTunaamini michezo hata kwenye wakati mgumu inatakiwa kujenga madaraja na si kuyaunguza”

#JFSports
MAHAKAMA YA ICC KUCHUNGUZA UHALIFU WA KIVITA UKRAINE

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imesema ktk uchunguzi wa awali imeridhika kuna sababu za msingi za kuamini madai ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya Binadamu umefanyika Nchini Ukraine

Soma https://jamii.app/ICCUkraine
RAIS BIDEN: PUTIN ALIKATAA DIPLOMASIA, HAJUI KILICHOPO MBELE

Asema Vita dhidi ya #Ukraine ilipangwa bila kuchochewa, na Rais Putin alifikiri Nchi za Magharibi hazitojibu

Marekani itapiga marufuku Ndege za Urusi kwenye Anga lake

Soma - https://jamii.app/BidenPutin

#RussiaUkraine
LEO NI JUMATANO YA MAJIVU. KWARESMA KUANZA

- Siku ya kwanza ya Kwaresma huitwa Jumatano ya Majivu kutokana na tendo la kupakwa Majivu

- Kwaresma ni siku 40 za kufunga, kusali, kutafakari Neno la Mungu na kufanya matendo ya huruma

Kwa Historia, soma - https://jamii.app/Kwaresima
JE, WAJUA?: Chupa moja ya Damu inaweza kuokoa Maisha ya Watu Watatu. Mwanamke anaweza kuchangia Damu kila baada ya Miezi 4 na Mwanaume anaweza kuchangia kila baada ya Miezi Mitatu

Kila unapotoa Damu unafanyiwa uchunguzi mdogo wa #Afya. Damu inayochangiwa huchunguzwa Virusi vya UKIMWI, Kaswende na Homa ya Ini (Hepatitis B&C). Matokeo ya uchunguzi hayatolewi hadharani, bali ni mtoaji tu ndiye atakayepewa.

#JamiiForums #BloodDonation #DidYouKnow
MDAU: UTHUBUTU NI SILAHA YA MAFANIKIO

Anasema woga wa kufanya makosa ni tabia iliyowafungia wengi nje ya fursa nono, ikiwapotezea muda na ujasiri. Hatua mojawapo kutoka kwenye umasikini na unyonge ni kutoogopa gharama za makosa

Soma - https://jamii.app/UthubutuSOC

#StoriesOfChange
Kampuni ya kutengeneza Ndege ya Marekani ya #Boeing (BA.N) imesitisha usambazaji wa Vifaa, matengenezo na usaidizi wa kiufundi kwa Mashirika ya Ndege ya Urusi kama sehemu ya vikwazo vilivyowekwa kutokana na uvamizi wake #Ukraine

Soma - https://jamii.app/BoeingRussia
#RussiaUkraineWar
Kuelekea Siku ya Usikivu Duniani (Machi 03, 2022), Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema zaidi ya Watu Bilioni 1 Duniani wapo katika hatari ya kupoteza uwezo wa kusikia kutokana na mazoea ya kusikiliza muziki kwa sauti kubwa, na kwa muda mrefu

Soma - https://jamii.app/WHD2022
NJOMBE: WANANCHI WALIOIBIWA MASUFURIA YA WALI WAITWA POLISI

Wananchi #Njombe wameitwa kituoni kutambua mali zilizokamatwa wakati wa doria ya Polisi

Baadhi ya mali ni magodoro, pikipiki, sufuria, mitungi ya gesi, jiko, laptop na TV

Soma - https://jamii.app/SufuriaNjombe
#JamiiForums
APPLE YASITISHA KUUZA BIDHAA URUSI

Kampuni hiyo kubwa ya Teknolojia pia imesema huduma nyingine zikiwemo Apple Pay na Apple Maps zitadhibitiwa kufuatia uvamizi uliofanywa na Urusi dhidi ya #Ukraine, na kupekelea maelfu kukimbilia Mataifa jirani

Soma - https://jamii.app/AppleUrusi