JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MSUMBIJI: TOVUTI ZA SERIKALI ZADUKULIWA

Wadukuzi wa 'Yemen Hackers' wamedai kudhibiti tovuti 34 za Serikali ya Msumbiji na wanataka wapewe takriban Tsh. Milioni 46

Wametaka Fedha ndani ya saa 24 au watavujisha taarifa za siri

Soma - https://jamii.app/WadukuziMsumbiji

#DigitalSecurity
HOJA: UNATUMIA MBINU GANI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIMALEZI?

Mdau ametolea Mfano changamoto za Mtoto kutokupenda kula, kwenda Shuleni, kuchanganyika na wenzake, Uwezo mdogo Kimasomo, Utundu kupita kiasi na mengineyo

Anauliza umewahi kukumbana na tatizo gani la kimalezi na ulitatua vipi na kufanikiwa?

Mjadala - https://jamii.app/ChangamotoMalezi

#Malezi
UKRAINE YATANGAZA HALI YA HATARI

Bunge limethibitisha hali ya hatari kwa siku 30. Mamlaka zinaweza kuzuia raia kutembea na mikutano kwa maslahi ya Taifa

> Pia Serikali imetangaza huduma ya lazima ya kijeshi kwa wanaume waliofikia umri wa kupigana

Soma https://jamii.app/StateOfEmergency
UN YAITAKA URUSI KUONDOA WANAJESHI #UKRAINE

Katibu Mkuu wa UN, Antonio Guterres amesema wengi wameshapoteza maisha, na ni wakati wa kuipa nafasi Amani

Rais wa Marekani, Joe Biden asema Urusi itabeba lawama kwa yatakayotokea

Soma https://jamii.app/UrusiUN

#RussiaUkraineConflict
PAPA FRANCIS ATANGAZA MACHI 2 KUWA SIKU YA KUFUNGA NA KUIOMBEA #UKRAINE

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ametoa wito kwa watu kutumia Siku ya Jumatano ya Majivu kuiombea Ukraine baada ya ripoti za Urusi kuanza mashambulizi

Soma https://jamii.app/PapaUkraine

#RussiaUkraineConflict
MDAU: MAKOSA YA KIFEDHA YANAYOFANYWA NA VIJANA WENGI

1. Kutumia Fedha uliyoipata kabla ya kuweka Akiba: Msemo wa 'Ponda Mali kufa kwaja' hupelekea Vijana wengi kufanya Matumizi yasiyo na ulazima na kukosa Akiba

2. Kutupa Risiti (Stakabadhi za Malipo): Unaweza kudhani risiti za vitu unavyonunua hazina umuhimu kwako lakini hukusaidia kutambua tabia/mwenendo wa Matumizi yako

Soma - https://jamii.app/MoneyMistakes

#Maisha
PUTIN: ATAKAYEINGILIA MZOZO WA UKRAINE ATAPATA PIGO LA KIHISTORIA

Baada ya milipuko kuripotiwa Mji wa #Kyiv, Rais wa Urusi asema, "Yeyote atakayeingilia kutoka Mataifa ya Magharibi, atakutana na matokeo ambayo hajakutana nayo"

Soma - https://jamii.app/OnyoPutin

#RussiaUkraineCrisis
#UPDATES: Takriban Watu 6 wameripotiwa kupoteza Maisha katika shambulio la Bomu llililofanywa na vikosi vya Urusi Nchini #Ukraine

Maafisa wanasema shambulio dhidi ya kambi ya Jeshi ya #Podilsk, nje ya Mji wa #Odessa limesababisha Watu wengine saba kujeruhiwa, na 19 hawajulikani walipo.

#RussiaUkraineConflict #JamiiForums
MALEZI: MTENGENEZEE MTOTO MAZINGIRA YA KUJISOMEA NYUMBANI

1. Kama inawezekana ni vema kuwe na chumba/sehemu maalumu isiyokuwa na usumbufu kwaajili ya Mwanafunzi kujisomea

2. Hakikisha una ratiba ya Masomo kwa Siku, Wiki na kwa Mwezi. Kwenye ratiba kuwe na muda wa kujisomea vitabu vya ziada

3. Tunza Mitihani yote ya Mtoto iliyopita ili kutathmini Maendeleo yake. Mwanafunzi awe na ratiba maalumu ya kuangalia TV au kutumia Vifaa vya Kieletroniki.

Soma - https://jamii.app/MasomoNyumbani
#Malezi
SHINYANGA: WATUMISHI 6 WAFUKUZWA KAZI KWA UTORO, KUGHUSHI NYARAKA

Baraza la Madiwani Wilaya ya Shinyanga limewafukuza kazi Watumishi hao kutoka Idara ya Afya na Idara ya Utawala

Watumishi wengine 2 watakatwa 15% ya Mishahara yao kwa Miaka mitatu

Soma - https://jamii.app/WafukuzwaUtoro
KISUTU, DAR: MADABIDA NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Aliyekuwa M/kiti wa CCM - Dar, Ramadhani Madabida na wenzake 5 walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kusambaza makopo 7,776 ya Dawa Bandia za kufubaza VVU (ARV) aina ya Antiretroviral.

Soma - https://jamii.app/MadabidaFree
MTWARA: MWANAFUNZI AANDIKA BARUA KWA MWALIMU MKUU KUKATAA SHULE

Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Madimba ameandika barua kwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kukataa kuendelea kusoma, akisema Masomo yamemshinda

Soma - https://jamii.app/ShuleBasiUvuvi

#JFLeo
NAIROBI, KENYA: MUSWADA WA KUDHIBITI KAMARI WAANDALIWA

Muswada huo utafanya Michezo ya kubeti na kamari Jijini #Nairobi iwe inachezwa kwenye Hoteli zenye hadhi ya Nyota Tano na Casino tu, huku muda wa kucheza ukiwa saa 2 usiku hadi 12 alfajiri

Soma - https://jamii.app/BettingGambling
UKRAINE: RAIS KUMPATIA SILAHA KILA RAIA ANAYETAKA KUIPIGA URUSI

Rais Volodymyr Zelensky amewahamasisha Raia kupigania Nchi yao, na kusema silaha zitatolewa

Kufuatia Urusi kuivamia, #Ukraine imesitisha uhusiano wake wa Kidiplomasia na Taifa hilo

Soma - https://jamii.app/SilahaUkraine
WANAOVUJISHA MIAMALA YA WATEJA KUCHUKULIWA HATUA

Waziri wa Sheria, George Simbachawene ameagiza Kampuni za Mawasiliano kuchunguzwa na hatua kuwachukuliwa dhidi ya Watumishi ambao wanavujisha Taarifa za Miamala ya Wateja kwa wahalifu wa Mitandaoni

Soma - https://jamii.app/WatejaTaarifa
SCHALKE O4 KUONDOA NEMBO YA KAMPUNI YA URUSI KWENYE JEZI

- Klabu hiyo ya Ujerumani imethibitisha kuondoa kwenye jezi zake nembo ya mdhamini mkuu wa Klabu, Kampuni ya Gazprom inayomilikiwa na Urusi

- Imesema sehemu ilipokuwa inakaa nembo yatawekwa maneno β€˜Schalke 04’

#JFSports
TANESCO: KUANZIA JULAI, UMEME UTAINGIA BILA KUANDIKA TOKEN KWENYE MITA

Kuanzia Julai, Smart Meters zitaanza kutumika. Umeme utawaka moja kwa moja kama ilivyo huduma za king'amuzi

Suala la Token liliwahi kulalamikiwa kupitia #StoriesOfChange ya JF

Soma - https://jamii.app/SmartMeters
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
#UPDATES: Takriban Raia 10 na Wanajeshi 40 wa #Ukraine wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya Anga yaliyofanywa na Urusi leo Februari 24, 2022 katika Mji wa #Odessa

Taarifa ya Vifo hivyo imetolewa na Msaidizi wa Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alipozungumza na Waandishi.

#RussianInvasion #RussiaUkraine
MDAU: VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUHAMIA DAR

Anashauri wanaotaka kuhamia Dar wahakikishe wana Ujuzi na Nidhamu ya Fedha

Asema si tatizo Kijana wa Mkoani kuja Dar, lakini ni muhimu kujiuliza; Mambo yakienda tofauti utafanyaje?

Soma - https://jamii.app/DarKuhamia

#StoriesOfChange