JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UKRAINE: Rais Volodymyr Zelensky ameagiza wanaume nchini humo wenye umri wa miaka 18-60 kuilinda nchi yao

> Taarifa zinasema Majeshi ya Urusi yameshauteka Uwanja wa Ndege wa Jeshi la Ukraine pamoja na Kinu cha Nyuklia cha Chernobil

Soma https://jamii.app/WanaumeUkraine
Ukraine: Watu zaidi ya 137 wahofiwa kufariki baada ya mlipuko uliosikika katika Mji Mkuu wa Nchi hiyo, Kyiv

Majeshi ya Urusi yameonekana kuendelea na mashambulizi mbali na kuwekewa vikwazo na Marekani na Ulaya

#JamiiForums #RussiaUkraineConflict
GEITA: AUAWA KWA TUHUMA ZA KUJARIBU KUMBAKA MWANAFUNZI

Kijana mwenye umri kati ya miaka 18 - 22 ameuawa na kuchomwa moto akidaiwa kujaribu kubaka Mwanafunzi aliyekuwa akielekea Shuleni

M/kiti wa Mtaa anashikiliwa na Polisi kusaidia kubaini wahusika

Soma https://jamii.app/GeitaAuawa
1
#UPDATES: Mashirika ya Ndege ya Uingereza yamepigwa marufuku kutua katika Viwanja vya Ndege vya Urusi pamoja na kupita kwenye Anga lake

Uamuzi huo unafuatia uamuzi wa Uingereza kupiga marufuku Shirika la Ndege la Urusi, #Aeroflot kutua Nchini Uingereza.

#RussiaUkraineConflict
👍1
UEFA: FAINALI YA KLABU BINGWA ULAYA HAITAFANYIKA URUSI

- UEFA imehamisha fainali ya Klabu Bingwa Ulaya kutoka St. Petersburg, Urusi kwenda Paris, Ufaransa

- Fainali hiyo itakayochezwa Mei 28, 2022 itachezwa katika uwanja wa Stade de France badala ya Gazprom Arena

#JFSports
👍1
SERIKALI: WATANZANIA WALIO UKRAINE WAWE WATULIVU

Wizara ya Mambo ya Nje imesema hakuna Mtanzania aliyepata madhara hadi sasa

Serikali imewashauri Watanzania wafuate maelekezo ya #Ukraine, na kuwasiliana na Ubalozi

Soma - https://jamii.app/UkraineWatanzania

#RussiaUkraineConflict
UKRAINE YAOMBA MSAADA WA MAJESHI YENYE NGUVU

Rais wa #Ukraine, Volodymyr Zelensky amelalamika Mataifa yenye nguvu kuwaacha wajipambanie huku wakitazama kwa mbali

> Amesema vikwazo vilivyowekwa havijamshawishi Rais Vladimir Putin kuacha mashambulizi

Soma https://jamii.app/UkraineYaombaMsaada
KIGOMA: MGANGA ATUHUMIWA KUMUUA MTEJA ALIYETAKA KUZIKA FEDHA ZA BIASHARA

Dereva wa Pikipiki na Mganga wa Kienyeji wanatuhumiwa kumuua na kisha kumfukia Mwanamke aliyekuwa ameenda kuzindika Fedha za Biashara kiasi cha Tsh. Milioni 9

Soma - https://jamii.app/MtejaKifoZindiko
#HumanRights
MAREKANI: ASKARI 3 WANAOTUHUMIWA KUMUUA GEORGE FLOYD WAKUTWA NA HATIA

Maafisa hao wa zamani wa #Minneapolis walishtakiwa kwa kumnyima Floyd Haki yake ya matibabu wakati Afisa Derek Chauvin alipomkandamiza kwa goti shingoni mnamo Mei 25, 2020

Soma - https://jamii.app/FloydCaseGuilt
#UKRAINE YATAKA MAZUNGUMZO NA URUSI

Rais Volodymyr Zelensky ametaka mazungumzo na Rais Vladimir Putin ili kunusuru Raia wasio na hatia

China imesema Urusi ipo tayari kwa mazungumzo baada ya Rais Putin kuongea na Rais Xi Jinping

Soma https://jamii.app/Mazungumzo

#RussiaUkraineConflict
#KENYA: MWANAFUNZI AFUNGWA KWA VIFO VYA MOTO SHULENI

Msichana (18) amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 jela kwa kuua bila kukusudia kufuatia kuwasha Moto katika Bweni la Shule na kuua wenzake tisa

Alitenda kosa hilo 2017 ktk Shule ya Wasichana ya Moi

Soma - https://jamii.app/JelaMotoShule
AFYA: 43% YA CHUMVI NCHINI HAICHANGANYWI NA MADINI JOTO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi amesema 43% ya chumvi ni hatari kwa Afya kwa kuwa hazichanganywi na madini joto

Athari zake ni Magonjwa kama Goita na kujifungua Watoto Njiti

Soma - https://jamii.app/ChumviHatari
TONY RASHID AMKALISHA BONGANI MAHLANGU

Bondia wa #Tanzania, Tony Rashid arejesha ubingwa wa ABU-Super Bantam Weight baada ya kumpiga kwa point bondia wa Afrika Kusini, Bongani Mahlangu(Profesa) kwenye pambano la Marudio

Soma https://jamii.app/TonyRashid
#JFSports
#UKRAINE: MBUNGE ASEMA WANAWAKE WATAPIGANIA NCHI

Kira Rudik amechapisha picha akiwa ameshika bunduki na kusema anajifunza kuitumia ili kutetea ardhi yake dhidi ya Urusi

Amesema Wanawake watatetea Nchi yao kama Wanaume

Soma - https://jamii.app/WanawakeUkraine

#RussiaUkraineConflict
RAIS WA UKRAINE AVAA GWANDA NA KUINGIA VITANI

Rais Volodymyr Zelensky ameingia "Uwanja wa Vita" kutetea Nchi yake

Awali, kulikuwa na tetesi Rais huyo amekimbia Nchi. Alijitokeza na kuomba Wananchi wapuuzie taarifa hizo

Soma - https://jamii.app/GwandaUkraine

#RussiaUkraineConflict
MAREKANI: RAIS BIDEN ATEUA MWANAMKE MWEUSI KUWA JAJI WA MAHAKAMA YA JUU

Ketanji Jackson anakuwa Mwanamke wa kwanza Mweusi kwenye Mahakama ya juu kabisa ambayo awali ilitangaza hastahili kupata Uraia wa Marekani kutokana na rangi ya Ngozi yake

Soma https://jamii.app/KentanjiSupreme
#JFLeo
RELI, DARAJA VYASOMBWA NA MAJI. ABIRIA WAKWAMA MOROGORO

Mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Morogoro zimesababisha uharibifu wa Miundombinu ya Reli ya kati na Barabara ambapo Daraja la Kidete limekatika na kupelekea Treni kusimamisha safari zake

Soma - https://jamii.app/AbiriaKilosa
URUSI: Mtandao wa #Facebook unaomilikiwa na Kampuni ya Meta umezuiwa Nchini Urusi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kupishana ktk Masharti ya vitu vya kuweka Mitandaoni wakati huu wa vita na #Ukraine

Soma - https://jamii.app/FBBanRussia

#DigitalRights #RussiaUkraineConflict #PressFreedom
RAIS SAMIA AKUTANA NA MTAWALA WA DUBAI

Rais Samia amezungumza na Makamu wa Rais ambaye ni Waziri Mkuu wa UAE na Mtawala wa Dubai, Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum

> Ni baada ya kuhutubia katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 Mjini Dubai

Soma https://jamii.app/RaisSamiaDubai

#JFLeo
POLAND KUKATAA KUCHEZA NA URUSI MECHI YA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

- Poland imesema itakataa kucheza mchezo huo wa Machi 25, 2022 baada ya Urusi kuivamia Ukraine

- Pia itakuwa mwenyeji wa michezo yote ambayo Ukraine ilitakiwa kuwa mwenyeji ila itashindwa kutokana na vita

#JFSports