JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MFAHAMU SADIO MANE WA SENEGAL, LIVERPOOL

Alipokuwa mdogo alitamani kuwa kama El Hadji Diouf na Ronaldinho hivyo akiwa na miaka 16 alitoroka nyumbani Bambali kwenda Dakar ili akacheze mpira

Kabla ya #AFCON2021 kuanza alitamani Senegal icheze Fainali na Misri au Guinea na jambo hilo lilitimia kwani walicheza dhidi ya Misri

Soma - https://jamii.app/SadioMane

#JFSports
DAR: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni imetoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani Paul Makonda na kuubandika wito huo ktk Makazi yake ya Dar na Koromije

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Saed Kubenea imeahirishwa hadi Machi 2, 2022

Soma https://jamii.app/KesiMakonda

#JFUwajibikaji
DODOMA: Akishiriki Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema "Sasa hivi kuna biashara za mtandao nyingi zinafanyika hazilipi Kodi na hatuzijui. Utakapoingia Mfumo huu tutawajua"

Soma - https://jamii.app/RaisMfumoAnwani

#JFSiasa
Katika kuadhimisha #SaferInternetDay, changamoto kama unyanyasaji Mtandaoni hupewa umuhimu kwani siku hii hulenga kuongeza ufahamu kuhusu masuala ya Mtandao

Kaulimbiu ya Mwaka 2022 ni "Pamoja kwa Mitandao bora"

Soma - https://jamii.app/MitandaoSalama

#SaferInternetDay2022 #DigitalRights
NINI HUFANYA MTU KUWA KWENYE HATARI YA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU?

Umasikini: Wasafirishaji hulenga jamii masikini na zilizotengwa na kuwapa watu fursa za uongo. Kundi hili lina uwezekano mkubwa wa kuhatarisha maisha yao ili kuhudumia familia zao

Afya ya Akili: Watu walio na matatizo ya afya ya akili hukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo uwezo mdogo wa kutathmini hatari. Wasafirishaji haramu wana ujuzi wa kugundua udhaifu huu na kuutumia kwa manufaa yao

Soma - https://jamii.app/HumTrafficking

#EndHumanTrafficking
WATU MILIONI 13 KWENYE PEMBE YA AFRIKA WANAKABILIWA NA NJAA

Ukame umepelekea mazao kuharibika, mifugo kufa na watu wapatao Milioni 13 ktk Nchi za Kenya, Ethiopia na Somalia kukumbwa na njaa

> Uhaba wa chakula unalazimu Familia kuacha makazi yao

Soma - https://jamii.app/UhabaNjaaWFP

#HumanRights
WATU 2,117,387 WAMEPATA DOZI KAMILI DHIDI YA #COVID19

Kuanzia Januari 29 - Februari 6, 2022 visa vipya 252 vilibainika kati ya watu 8,529 waliopimwa. Dar yaongoza ikiwa na maambukizi 184

Watu 792 wamepoteza maisha tangu mlipuko uanze

Soma https://jamii.app/DataUvikoTz

#UVIKO3 #JFAfya
CCM YAMPITISHA ZUNGU KUGOMBEA U-NAIBU SPIKA

- Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu imempitisha Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu kuwa Mgombea wa Kiti cha Naibu Spika wa Bunge

Soma https://jamii.app/ZunguCCM-NSpika

#Democracy
Aliyewahi kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Benedict wa 16 amekiri makosa katika kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia alipokuwa Askofu Mkuu wa Munich, na kuomba msamaha

Mawakili wake wanadai hakuwa wa kulaumiwa moja kwa moja

Soma - https://jamii.app/PapaBenRadhi

#Accountability
SERIKALI YAFUTA KIFUNGU CHA SHERIA CHA KUWALINDA POLISI

Muswada huo uliopelekwa Bungeni kwa hati ya dharura uliibua sintofahamu kwa Wananchi huku wakihoji mantiki ya kuwakingia kifua Polisi endapo watafanya jinai na kuhalalisha mauaji ya raia

Soma - https://jamii.app/KifuaPolisi

#JFUwajibikaji #JFSheria
#TUNISIA: Chama cha Majaji kimetoa wito wa kusitishwa kwa shughuli zote za Mahakama kuanzia Februari 9 ili kupinga hatua ya Rais Kais Saed ya kulivunja Baraza la Mahakama ya Juu

Awali Rais huyo aliwafuta kazi Mawaziri na kutwaa Mamlaka yote

Soma - https://jamii.app/MgomoJajiTunis

#Governance
EU YAIONDOLEA BURUNDI VIKWAZO VYA KIUCHUMI

Ni kutokana na mazingira ya Amani ya Kisiasa pamoja na Maendeleo kwenye masuala muhimu ikiwemo #HakiZaBinadamu

Vikwazo viliwekwa baada ya Pierre Nkurunziza kuamua kugombea Urais kwa Muhula wa 3

Soma - https://jamii.app/BurSanctionsEU

#JFUchumi
MDAU: Ili kupunguza uhalifu utokanao na wivu wa mapenzi, Elimu ya mahusiano itolewe na pia Viongozi wa Dini na Serikali washirikishwe

> Anaongeza, uwepo wa Wanasaikolojia unahitajika kwa ukubwa sana kama huduma ya matibabu mengine

Soma https://jamii.app/UhalifuSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
Nukuu ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame

#Governance
MAANA YA R KWENYE FILAMU/MOVIE

Filamu yenye R (Restricted) ni ile iliyozuiliwa kutazamwa na Watoto walio chini ya miaka 17

Huwa na Maudhui ya Watu wazima ikiwemo Lugha ya Matusi, Vurugu kali, Utupu/Ngono na Dawa za Kulevya

Soma - https://jamii.app/PGMovies

#JFMaarifa
Uonevu au Unyanyasaji kupitia Teknolojia unaweza kutokea kwenye Mitandao ya Kijamii. Ni tabia ya kujirudia inayolenga kumtisha, kumdhalilisha au kumkasirisha mlengwa

Umewahi kuwa mhanga wa uonevu wa mitandaoni? Ulichukua hatua gani?

Soma - https://jamii.app/UonevuMitandao

#CyberBullying #DigitalRights
KUKAGUANA/KUCHUNGUZANA KIDEMOKRASIA NDIKO HULETA UWAJIBIKAJI NA MABADILIKO

Wananchi wanatarajia Serikali zao kutoa Huduma za Umma kwa ufanisi mkubwa ambao utakidhi mahitaji yao na kutambua Haki zao kama Binadamu. Pia, kupewa Uwezo wa kusema Kero zao na kuweza kusikilizwa na Mamlaka husika

Utafiti unaonesha Nchi zenye viwango vya chini vya Utoaji wa Huduma hazina #Sheria au zina Sheria dhaifu katika kuwapa adhabu wanaofanya vibaya (International IDEA 2013a).

Soma - https://jamii.app/KukaguanaDemokrasia
#Accountability
RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA UFARANSA NA UBELGIJI

Akiwa Ufaransa Rais atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani

Vilevile, atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa

Soma - https://jamii.app/RaisKaziZiara

#Governance
SIHA: MGANGA MFAWIDHI ASHUSHWA CHEO KWA HUDUMA MBOVU

Naibu Waziri wa #Afya, Dkt. Godwin Mollel amemshusha Cheo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha baada ya Wananchi kulalamikia huduma mbovu na Mgonjwa kuachwa zaidi ya Saa 1 bila huduma

Soma - https://jamii.app/MgangaOutSiha

#JFUwajibikaji