JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS SAMIA: KUNA UZEMBE, UFUJAJI FEDHA NA MIVUTANO MINGI MKOANI MARA

Asema Fedha zinafujwa kwenye Miradi licha ya kuwepo Wakaguzi wa Ndani Mkoani humo

Amesema, "Wakaguzi wa Ndani nanyi ni sehemu ya wafujaji wa Fedha hizo, ndiyo maana hamsemi"

Soma - https://jamii.app/MiradiFedhaMara

#JFUwajibikaji
RAIS SAMIA: WANANCHI ACHENI KUFANYWA NGAZI

Amesema, "Hawa watu wanakuja na maneno mazuri wanawafanya kuwa ngazi mnainama wanapanda. Wakifika wanapotaka, hamna maana"

Asema Miradi inayoletwa ni ya Wananchi hivyo waifuatilie na ikiwa haiendi waseme

Soma - https://jamii.app/WananchiRaisMara

#JFSiasa
Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika umeridhia na kupitisha ombi la #Tanzania la kutaka #Kiswahili kuwa lugha ya Kazi ktk Umoja huo

Kiswahili kinakadiriwa kuwa na Wazungumzaji takribani milioni 100 Barani Afrika

Soma - https://jamii.app/KiswahiliAU

#JFLugha
GSM YAJIONDOA KWENYE UDHAMINI WA LIGI KUU BARA

Kampuni ya GSM imejiondoa kwenye Udhamini Mwenza ambapo awali iliweka dau la Tsh. bilioni 2.5

Imeeleza sababu ni kutokana na TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kutimiza Matwaka ya Kimkataba

Soma https://jamii.app/GSMoutLigi

#JFSports
Filamu (Movie) yenye Alama ya PG (Parental Guidance Suggested) huhitaji Mwongozo/Usimamizi wa Wazazi kutokana na baadhi ya Maudhui huenda yasifae kwa Watoto

Huweza kuwa na Lugha chafu, vurugu au maudhui ya Mapenzi kidogo lakini si Ngono

Soma - https://jamii.app/PGMovies

#JFMaarifa
GHALIB WA GSM AJIUZULU MAJUKUMU YA TAIFA STARS

Mmiliki wa Kampuni za GSM, Ghalib Said Mohamed ametangaza kujiuzulu nafasi ya kuwa Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars

Maamuzi hayo yamekuja muda mfupi baada ya Kampuni ya GSM kutangaza kujiondoa katika nafasi ya Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu Bara

#JFSports
Mitandao ya Kijamii imetajwa kama moja ya njia kuu ambazo Intaneti huathiri Afya ya Akili

Hii hutokea unapojilinganisha na watu wengine au kuhisi wasiwasi kuhusu kutopata 'Likes' za kutosha ikielezwa vitendo hivi vinaporudiwa mara kwa mara inakuwa uraibu

Unapotumia Mitandao ya Kijamii usiweke nguvu kubwa kufurahisha watumiaji wengine

Soma - https://jamii.app/InternetMentalHealth

#MentalHealth #JFTech
KOREA KASKAZINI YADAIWA KUIBA FEDHA KUPITIA UDUKUZI

Wataalamu wa UN wanasema Fedha hizo zimekuwa zikitumika kufadhili miradi ya Nyuklia na Makombora

Inaelezwa Wadukuzi waliiba zaidi ya Dola milioni 50 Mwaka 2020 mpaka katikati ya 2021

Soma https://jamii.app/UdukuziKZUN

#CyberCrimes #JFTech
WAFANYABISHARA WA VIFAA VYA UJENZI WAELEKEZWA KUSHUSHA BEI

Waziri wa Viwanda, Dkt. Ashatu Kijaji asema imebainika ongezeko holela la bei ya vifaa vya ujenzi hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa kufanya uzalishaji banifu

Soma - https://jamii.app/BeiBidhaa

#JFBiashara
MAANA YA PG-13 KWENYE FILAMU/MOVIE

PG13 (Parents Strongly Cautioned) inatoa tahadhari kubwa kwa Wazazi/Walezi kutokana na baadhi ya Maudhui ndani ya Filamu kutofaa kwa Watoto walio chini ya miaka 13

Huweza kuwa na Maudhui mazito zaidi ya Vurugu, Utupu, Uasherati, Lugha kali ya Matusi, β€˜shughuli za Watu wazima’ au Dawa za Kulevya.

Soma - https://jamii.app/PGMovies

#JFMaarifa
ATHARI ZA COVID-19: Huduma za Msingi za Afya zikiwemo programu za Chanjo na matibabu ya magonjwa kama UKIMWI ziliripotiwa kuathiriwa kwa 92% katika Nchi 129

WHO imesema huduma ziliathiriwa kwa kiasi kikubwa, huku kukiwa na maboresho kidogo

Soma https://jamii.app/AthariHudumaAfya

#UVIKO3 #JFAfya
DEMOKRASIA: Uwajibikaji wa Kidemokrasia katika utoaji huduma ni pale ambapo Wananchi au Wawakilishi wao wanahoji kuhusu Huduma za Umma na maoni hayo kufanyiwa kazi au Watendaji kuwajibishwa

Wananchi ni mfano mzuri wa wadai haki kwasababu wao ndio wanaoipa Mamlaka Wawajibikaji na mara nyingi wanalipia huduma wanazopata

Soma - https://jamii.app/UwajibikajiHuduma
#Democracy #Accountability
MDAU: BAADHI YA VITU NITAKAVYOWAFUNDISHA WANANGU KABLA YA KIFO CHANGU

1. Chochote unachofanya hakikisha unakuwa imara kuliko Mtu mwingine yeyote. Usipende kukaa na walioshindwa

2. Kama unataka kutajirika usitatue matatizo ya Asili bali tatua matatizo ya Watu ya kujitakia. Kama huwezi kuona Hela katikati ya wajinga basi wewe ni mmoja wao

Soma zaidi - https://jamii.app/MafundishoWatoto

#StoriesOfChange #JFMdau
BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI BINADAMU: Mwaka 2018 takriban waathirika 50,000 waliripotiwa ktk Nchi 148 huku Wanawake na Wasichana wakiendelea kuwa waathirika wakuu

Wanawake wanachukua hadi 46% ya waathirika wote na Wasichana ni 19%

Soma zaidi - https://jamii.app/HumTrafficking

#EndHumanTrafficking
MFAHAMU SADIO MANE WA SENEGAL, LIVERPOOL

Alipokuwa mdogo alitamani kuwa kama El Hadji Diouf na Ronaldinho hivyo akiwa na miaka 16 alitoroka nyumbani Bambali kwenda Dakar ili akacheze mpira

Kabla ya #AFCON2021 kuanza alitamani Senegal icheze Fainali na Misri au Guinea na jambo hilo lilitimia kwani walicheza dhidi ya Misri

Soma - https://jamii.app/SadioMane

#JFSports
DAR: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni imetoa kibali cha kuchapisha Gazetini wito wa kumuita Mahakamani Paul Makonda na kuubandika wito huo ktk Makazi yake ya Dar na Koromije

Kesi hiyo iliyofunguliwa na Saed Kubenea imeahirishwa hadi Machi 2, 2022

Soma https://jamii.app/KesiMakonda

#JFUwajibikaji
DODOMA: Akishiriki Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema "Sasa hivi kuna biashara za mtandao nyingi zinafanyika hazilipi Kodi na hatuzijui. Utakapoingia Mfumo huu tutawajua"

Soma - https://jamii.app/RaisMfumoAnwani

#JFSiasa
Katika kuadhimisha #SaferInternetDay, changamoto kama unyanyasaji Mtandaoni hupewa umuhimu kwani siku hii hulenga kuongeza ufahamu kuhusu masuala ya Mtandao

Kaulimbiu ya Mwaka 2022 ni "Pamoja kwa Mitandao bora"

Soma - https://jamii.app/MitandaoSalama

#SaferInternetDay2022 #DigitalRights
NINI HUFANYA MTU KUWA KWENYE HATARI YA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU?

Umasikini: Wasafirishaji hulenga jamii masikini na zilizotengwa na kuwapa watu fursa za uongo. Kundi hili lina uwezekano mkubwa wa kuhatarisha maisha yao ili kuhudumia familia zao

Afya ya Akili: Watu walio na matatizo ya afya ya akili hukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo uwezo mdogo wa kutathmini hatari. Wasafirishaji haramu wana ujuzi wa kugundua udhaifu huu na kuutumia kwa manufaa yao

Soma - https://jamii.app/HumTrafficking

#EndHumanTrafficking
WATU MILIONI 13 KWENYE PEMBE YA AFRIKA WANAKABILIWA NA NJAA

Ukame umepelekea mazao kuharibika, mifugo kufa na watu wapatao Milioni 13 ktk Nchi za Kenya, Ethiopia na Somalia kukumbwa na njaa

> Uhaba wa chakula unalazimu Familia kuacha makazi yao

Soma - https://jamii.app/UhabaNjaaWFP

#HumanRights