JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WATU 2,117,387 WAMEPATA DOZI KAMILI DHIDI YA #COVID19

Kuanzia Januari 29 - Februari 6, 2022 visa vipya 252 vilibainika kati ya watu 8,529 waliopimwa. Dar yaongoza ikiwa na maambukizi 184

Watu 792 wamepoteza maisha tangu mlipuko uanze

Soma https://jamii.app/DataUvikoTz

#UVIKO3 #JFAfya
CCM YAMPITISHA ZUNGU KUGOMBEA U-NAIBU SPIKA

- Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu imempitisha Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu kuwa Mgombea wa Kiti cha Naibu Spika wa Bunge

Soma https://jamii.app/ZunguCCM-NSpika

#Democracy
Aliyewahi kuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Benedict wa 16 amekiri makosa katika kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia alipokuwa Askofu Mkuu wa Munich, na kuomba msamaha

Mawakili wake wanadai hakuwa wa kulaumiwa moja kwa moja

Soma - https://jamii.app/PapaBenRadhi

#Accountability
SERIKALI YAFUTA KIFUNGU CHA SHERIA CHA KUWALINDA POLISI

Muswada huo uliopelekwa Bungeni kwa hati ya dharura uliibua sintofahamu kwa Wananchi huku wakihoji mantiki ya kuwakingia kifua Polisi endapo watafanya jinai na kuhalalisha mauaji ya raia

Soma - https://jamii.app/KifuaPolisi

#JFUwajibikaji #JFSheria
#TUNISIA: Chama cha Majaji kimetoa wito wa kusitishwa kwa shughuli zote za Mahakama kuanzia Februari 9 ili kupinga hatua ya Rais Kais Saed ya kulivunja Baraza la Mahakama ya Juu

Awali Rais huyo aliwafuta kazi Mawaziri na kutwaa Mamlaka yote

Soma - https://jamii.app/MgomoJajiTunis

#Governance
EU YAIONDOLEA BURUNDI VIKWAZO VYA KIUCHUMI

Ni kutokana na mazingira ya Amani ya Kisiasa pamoja na Maendeleo kwenye masuala muhimu ikiwemo #HakiZaBinadamu

Vikwazo viliwekwa baada ya Pierre Nkurunziza kuamua kugombea Urais kwa Muhula wa 3

Soma - https://jamii.app/BurSanctionsEU

#JFUchumi
MDAU: Ili kupunguza uhalifu utokanao na wivu wa mapenzi, Elimu ya mahusiano itolewe na pia Viongozi wa Dini na Serikali washirikishwe

> Anaongeza, uwepo wa Wanasaikolojia unahitajika kwa ukubwa sana kama huduma ya matibabu mengine

Soma https://jamii.app/UhalifuSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
Nukuu ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame

#Governance
MAANA YA R KWENYE FILAMU/MOVIE

Filamu yenye R (Restricted) ni ile iliyozuiliwa kutazamwa na Watoto walio chini ya miaka 17

Huwa na Maudhui ya Watu wazima ikiwemo Lugha ya Matusi, Vurugu kali, Utupu/Ngono na Dawa za Kulevya

Soma - https://jamii.app/PGMovies

#JFMaarifa
Uonevu au Unyanyasaji kupitia Teknolojia unaweza kutokea kwenye Mitandao ya Kijamii. Ni tabia ya kujirudia inayolenga kumtisha, kumdhalilisha au kumkasirisha mlengwa

Umewahi kuwa mhanga wa uonevu wa mitandaoni? Ulichukua hatua gani?

Soma - https://jamii.app/UonevuMitandao

#CyberBullying #DigitalRights
KUKAGUANA/KUCHUNGUZANA KIDEMOKRASIA NDIKO HULETA UWAJIBIKAJI NA MABADILIKO

Wananchi wanatarajia Serikali zao kutoa Huduma za Umma kwa ufanisi mkubwa ambao utakidhi mahitaji yao na kutambua Haki zao kama Binadamu. Pia, kupewa Uwezo wa kusema Kero zao na kuweza kusikilizwa na Mamlaka husika

Utafiti unaonesha Nchi zenye viwango vya chini vya Utoaji wa Huduma hazina #Sheria au zina Sheria dhaifu katika kuwapa adhabu wanaofanya vibaya (International IDEA 2013a).

Soma - https://jamii.app/KukaguanaDemokrasia
#Accountability
RAIS SAMIA KUFANYA ZIARA UFARANSA NA UBELGIJI

Akiwa Ufaransa Rais atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani

Vilevile, atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa

Soma - https://jamii.app/RaisKaziZiara

#Governance
SIHA: MGANGA MFAWIDHI ASHUSHWA CHEO KWA HUDUMA MBOVU

Naibu Waziri wa #Afya, Dkt. Godwin Mollel amemshusha Cheo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Siha baada ya Wananchi kulalamikia huduma mbovu na Mgonjwa kuachwa zaidi ya Saa 1 bila huduma

Soma - https://jamii.app/MgangaOutSiha

#JFUwajibikaji
BURUDANI: Wadau wa Jukwaa la Entertainment ndani ya JamiiForums.com wanasema Nyimbo za kale (Bendi) hazichuji na zinavutia hadi sasa

Wewe ni shabiki wa Bendi? Ni 'Classic' gani zinakuburudisha mpaka leo?

Zaidi, Tembelea - https://jamii.app/MuzikiBendi

#JFBurudani
UREMBO/MITINDO: Unakumbuka Nguo au Mitindo gani ya 'Fashion' ya zamani ambayo kwasasa inaonekana kuwa Kituko ukivaa?

Wadau wa JamiiForums.com wametaja baadhi ikiwemo Chupi za VIP ambazo ilikuwa ikikatika inapanda juu. Viatu vya Raizon, Suruali za Kitambaa cha Mchele Mchele pamoja na Viatu vya utanikoma Saa 6

Mjadala zaidi - https://jamii.app/OldFashion

#JFBurudani
Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imeiamuru #Uganda kuilipa DRC dola milioni 325 kama fidia kwa kuingilia mgogoro wa Jimbo la Ituri Miaka ya 1990

ICJ imesema mapigano yaliyofanywa na Majeshi ya Uganda Nchini #DRC yalikiuka Sheria ya Kimataifa

Soma - https://jamii.app/ICJUGvsDRC

#JFDiplomasia
UGANDA: Mwandishi Kakwenza Rukirabashaija ambaye aliwekwa chini ya ulinzi kwa takriban mwezi mmoja akituhumiwa kumkosoa Rais Yoweri Museveni amekimbia Nchini humo

Wakili wake amesema mazingira yalikuwa magumu kwa Kakwenza kuendelea kukaa

Soma - https://jamii.app/KakwenzaUG

#PressFreedom
LIBYA: MSAFARA WA WAZIRI MKUU WASHAMBULIWA KWA RISASI

Shambulio dhidi ya Abdulhamid Dbeibah Jijini Tripoli linakuja wakati kuna mvutano mkali kuhusu udhibiti wa Serikali

Uchaguzi Mkuu ulipangwa kufanyika Desemba 2021 lakini uliahirishwa

Soma - https://jamii.app/ShambulioPM

#JFSiasa
MALEZI: ONESHA UMAKINI PALE UNAPOZUNGUMZA NA MTOTO WAKO

Mtoto huumizwa Kisaikolojia pale ambapo utaonesha kutokuwa makini wakati unazungumza naye. Unatakiwa kuhakikisha Macho yako hayatazami kwengine zaidi ya Uso wa Mtoto wako

Msikilize kwa makini na utumie Lugha rahisi kumwelewesha. Wataalamu wa makuzi wanaeleza, Watoto wanaosikilizwa hujengeka na kuwa Watu wazima wanaoheshimu mawazo ya wengine

Soma - https://jamii.app/ListenChild

#JFMalezi #Parenthood