JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: MWANAFUNZI AJERUHIWA KWA KULA CHAPATI 5 BADALA YA 1

Caleb anayesoma Darasa la 7 anadaiwa kupigwa na Walimu ambao pia waliamuru Wanafunzi wenzie wampige

Hawezi kusimama, ana vidonda vya Moto Mgongoni na Figo yake 1 imeharibika

Soma https://jamii.app/CalebChapatiKE

#UkatiliWatoto
UNICEF: WATOTO WALIO MAENEO YENYE MIZOZO WALINDWE

Shirika la Kuhudumia Watoto limelaani mauaji yaliyotokea DR Congo hivi karibuni ambapo Watoto wapatao 15 waliuawa

Wengine takriban 30 walijeruhiwa baada ya Waasi kuvamia Kambi ya Wakimbizi

Soma - https://jamii.app/IturiWatoto

#HakiMtoto
ARUSHA: ANAYETUHUMIWA KUMUUA MLINZI NA KUONDOKA NA KICHWA APATIKANA

Raymond Mollel amekamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumchinja Mlinzi mwenzake na kuondoka na kichwa

Amekiri kuhusika na mauaji na kuonesha alipoficha kichwa cha mwenzake

Soma - https://jamii.app/MauajiYaArusha

#JFMatukio
Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimesema Mawakili 65 wamefariki dunia kwa #COVID19 tangu kutangazwa kisa cha kwanza cha Ugonjwa huo Machi 16, 2020

Serikali imechukua hatua kadhaa kudhibiti maambukizi ikiwemo kutoa chanjo bila malipo

Soma - https://jamii.app/Mawakili65Corona

#UVIKO3
UCHAGUZI WA KUMPATA NAIBU SPIKA KUFANYIKA FEBRUARI 11, 2022

Kila Chama chenye Uwakilishi Bungeni kinachokusudia kushiriki, kinashauriwa kuanza mchakato wa kumpata Mgombea miongoni mwa Wabunge wake

Jina la Mgombea linapaswa kuwasilishwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi kabla ya Saa 10:00 Jioni, Februari 10

Soma - https://jamii.app/NSpikaFeb11

#Bungeni #Democracy
#AFGHANISTAN: WASICHANA KURUHUSIWA KUHUDHURIA MASOMO CHUONI

Wanafunzi wa Kike wataruhusiwa kuhudhuria Masomo endapo watatenganishwa na wa kiume na mtaala utafuata kanuni za Kiislamu

Wanafunzi wa kiume watahudhuria masomo Asubuhi na wa Kike mchana

Soma - https://jamii.app/GirlsUnivTaliban

#ChildRights #JFElimu
DAR: Kesi inayomkabili aliyekuwa RC wa Dar, Paul Makonda imeahirishwa hadi Februari 8 baada ya Makonda kutofika Mahakamani

> Kesi ilifunguliwa na Saed Kubenea, ilitakiwa kusomwa kwa mara ya kwanza leo, Februari 3 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni

Soma https://jamii.app/MakondaKesi

#JFSiasa
UJERUMANI: KADINALI AOMBA KANISA KATOLIKI KURUHUSU NDOA KWA MAPADRI

Askofu Reinhard Marx amekitaja kigezo cha Useja kuwa hatari lakini hawezi kukihusisha moja kwa moja na Kashfa za Unyanyasaji wa Kijinsia zinazotikisa Kanisa hilo Duniani

Soma - https://jamii.app/NdoaMapadri
#JFLeo
TACAIDS: 40% YA VIJANA HAWAJUI HALI ZAO ZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI

Imeelezwa, Wasichana wanapata maambukizi kwa kasi mara tatu zaidi ya Wavulana

Ndoa za kulazimishwa zimetajwa miongoni mwa sababu zinazopelekea Wasichana kupata maambukizi zaidi

Soma - https://jamii.app/MaambukiziWasichana

#JFAfya
Waziri wa Ujenzi, Prof. Mbarawa amesema Fedha zilizojenga Daraja la Tanzanite ni za Mkopo kutoka Korea Kusini na zitalipwa na Serikali, hivyo Watanzania hawatalipa kulitumia

Daraja la Kigamboni linalipiwa kwasababu lilijengwa na Fedha za NSSF

Soma - https://jamii.app/DarajaTanzanite

#JFSiasa
Mshiriki wa #StoriesOfChange amesema Wanawake hupoteza fedha kufanya sherehe zisizo za lazima huku wengine wakitunga sherehe ili kutunzwa na wanakikundi

> Ameshauri "Msisubiri Rais aje awawezeshe wakati mtaji mdogo mlionao mnautumia vibaya"

Soma https://jamii.app/ShereheUmasikini

#JFMdau
#AFCON2021: MISRI YATINGA FAINALI

#TeamEgypt imeingia fainali kwa kumfunga mwenyeji wa michuano, #TeamCameroon kwa penati 3-1 baada ya kutofungana ndani ya dk 120

Misri sasa itacheza fainali na #TeamSenegal huku #TeamCameroon ikiivaa #TeamBurkinaFaso kusaka mshindi wa 3

#JFSports
SYRIA: KIONGOZI WA ISLAMIC STATE (IS) AJILIPUA

Abu Ibrahim Al-Hashimi al-Quraysh amejilipua na Familia yake baada ya Vikosi vya Marekani vilivyoenda Syria kupambana na ugaidi kudhibiti eneo alilokuwa akiishi

Miili ya watu 13 imeokotwa eneo hilo

Soma - https://jamii.app/KiongoziISAjiua

#JFMatukio
SIKU YA SARATANI DUNIANI

Siku ya Saratani huadhimishwa kila Februari 4. Kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO) Mwaka 2021, takriban watu Milioni 20 walibainika kuwa na Saratani

Kaulimbiu 2022 ni "Huduma za Saratani sawa kwa wote"

Soma - https://jamii.app/SikuYaSaratani

#WorldCancerDay #JFAfya
BUNGENI: Waziri wa Elimu, Profesa Adolf Mkenda amesema Wanafunzi watakaopata Ujauzito hawataruhusiwa kuingia Darasani na Watoto

Ametoa ufafanuzi huo kutokana na picha inayosambaa Mitandaoni ikimwonesha Mwanafunzi akiwa na Mtoto wake Darasani

Soma https://jamii.app/WanfzWatotoDrs

#JFElimu
RAIS SAMIA: JESHI HALIWEZI KUFANYA MAUAJI KISHA LIJICHUNGUZE LENYEWE

Ameagiza kuwepo kwa Kamati Huru ya kuchunguza mauaji yanayodaiwa kufanywa na Maafisa wa Polisi mkoani Mtwara

Ripoti ya Kamati Huru ya Uchunguzi kulinganishwa na Ripoti ya Polisi

Soma - https://jamii.app/KamatiHuru

#JFUwajibikaji
WAKURUGENZI WANNE WATENGULIWA KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU

Rais Samia Suluhu Hassan amewatengua Wakurugenzi wa Halmashauri za Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini

Utenguzi umefanyika Rais akiwa njiani Magu (Mwanza) kuelekea Musoma

Soma - https://jamii.app/RaisAtumbua

#JFUwajibikaji
ZAIDI YA 90% YA VISA VYA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTOKEA NCHI ZINAZOENDELEA

Mnamo Mwaka 2020, inakadiriwa Wanawake 604,000 waligunduliwa kuwa na Saratani ya Shingo ya Kizazi Duniani kote na takriban Wanawake 342,000 walipoteza maisha kutokana na Ugonjwa huo

Kwa kiasi kikubwa Saratani hii husababishwa na maambukizi ya muda mrefu (Persistence Infection) ya Virusi viitwavyo Human Papilloma, ambavyo huenezwa kwa njia ya kujamiiana

Soma - https://jamii.app/CervicalCancer

#CervicalCancer #JFAfya
SARATANI YA OVARI: Ni Saratani nadra kutokea Duniani na ambayo huchelewa kugundulika. Hali hii husababisha Wanawake wengi kuondolewa kabisa Mji wa Mimba

Wanawake ambao hawajazaa kabisa au waliochelewa mno kuzaa (juu ya miaka 35) wanatajwa kuwa kundi lililopo kwenye uwezekano mkubwa wa kupata Saratani hii

#JFAfya #CancerDay2022 #WorldCancerDay2022
NCHI ZINAZOENDELEA HUTOA TIBA KWA 30% YA WATOTO WENYE SARATANI

WHO yasema Watoto 400,000 chini ya miaka 19 duniani hupata Saratani kila mwaka

Nchi za kipato cha juu hutibu 80% ya Watoto, za kipato cha kati/chini zina 29%

Soma - https://jamii.app/SarataniWatoto

#WorldCancerDay #JFAfya