JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SARATANI YA TEZI DUME: Saratani hii hutokea pale ambapo chembechembe hai za Tezi huasi na kuanza kujigawanya bila kufuata utaratibu wa mfumo wa Mwili na hutengeneza vivimbe

Visababishi hatarishi ni Umri Mkubwa kuanzia miaka 50, Vinasaba kwenye Ukoo, Lishe hatarishi, Unene uliokithiri na Maambukizi ya mara kwa mara kwenye Tezi Dume

Soma - https://jamii.app/ProstateCancer

#WorldCancerDay2022 #JFAfya
MAMBO YA KUZINGATIA KUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUPATA SARATANI

Fanya mazoezi, kula mlo kamili na epuka kutumia tumbaku

Wataalamu wanashauri kushiriki programu za upimaji Saratani na kupata Chanjo dhidi ya Saratani ya Mlango wa Kizazi

Soma - https://jamii.app/SikuYaSaratani

#WorldCancerDay #JFAfya
SIMBA YAMSIMAMISHA KWA MUDA BERNARD MORRISON

Simba SC imemsimamisha kwa muda mchezaji wake Bernard Morrison hadi suala lake la kinidhamu litakapopatiwa ufumbuzi

Klabu hiyo imesema Morrison amekuwa na tabia ya kutoka kambini bila ruhusa

Soma https://jamii.app/SimbaMorrison

#JFSports
👍1
BALOZI WA MAREKANI AITEMBELEA JAMIIFORUMS

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Donald Wright leo Februari 4, 2022 ametembelea Ofisi za #JamiiForums na kukutana na watendaji na mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi

Balozi Wright na timu yake wamepata kuelezwa namna Jamii Forums ambayo ni Asasi ya Kiraia inavyoendesha shughuli zake katika kufanya uchechemuzi wa Haki za Kidijitali, Uwajibikaji, Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania
NJOMBE: Israel Msigwa maarufu kama 'Mtoa Roho' anatuhumiwa kumuadhibu Mwanaye Haskad Msigwa (7) kwa nyaya za umeme kwa kosa la kukojoa kitandani, na kumsababishia kifo

Mtuhumiwa alikamatwa Februari 3 Mkoani Iringa alipokimbilia kujificha

Soma - https://jamii.app/KifoNjombe

#JFMatukio
SONGWE: MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMCHOMA MOTO MTOTO WA MIEZI 6

Mariko Kahinga aliyedai Mkewe alipewa mimba na Mwanaume mwingine atafikishwa mahakamani kwa mujibu wa Sheria

Mama wa Mtoto huyo, Patricia Mwilenga asema Mumewe alikuwa akitamka kauli mbaya

Soma https://jamii.app/SongweBaba

#JFMatukio #HakiMtoto
KIRUSI KIPYA CHA HIV CHAGUNDULIKA UHOLANZI

Kirusi kipya cha HIV/AIDS kimegundulika Nchini Uholanzi na kupewa jina la #VBVariant. Kinadaiwa kushambulia Kinga ya Mtu mara mbili zaidi

Siku mbili zilizopita Kampuni ya #Moderna ilitangaza kuanza majaribio ya Chanjo ya HIV (mRNA-based HIV vaccive) ambapo Watu 56 waliojitolewa watapewa Dozi moja na wengine mbili huku wakifuatiliwa kwa Miezi 6.

Soma - https://jamii.app/VBvariantHIV

#JFAfya
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa agizo kwa IGP Simon Sirro kuwasimamisha kazi RPC na RCO Mkoa wa Mtwara, pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi eneo alilofia Mfanyabiashara Mussa Hamisi

Viongozi hao wametakiwa kukaa pembeni ili kupisha uchunguzi

Soma - https://jamii.app/PolisiMtwara

#JFUwajibikaji
WAZIRI UMMY: WANAUME JITOKEZENI KUPIMA TEZI DUME

Waziri wa Afya amesema watu 28,610 hufariki dunia kwa Saratani kwa mwaka. Saratani inayoongoza kwa Wanaume ni tezi dume na Wanawake ni mlango wa kizazi

Tezi dume inapimwa kisasa sio kama awali

Soma - https://jamii.app/TeziDume

#JFAfya
URUSI YAFUNGA SHUGHULI ZA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA DW

Urusi imefunga shughuli za Shirika la Habari la DW mjini #Moscow na kuwapokonya Wafanyakazi vibali vya Kazi ili kulipiza kisasi baada ya #Berlin kukifunga kituo cha Russia Today

Soma - https://jamii.app/DWBanRussia
#PressFreedom
NJOMBE: Mganga wa kienyeji aitwaye Joseph Mgunda (41) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwaua Suzana Mtitu (38) na Kassim Kitamkanga (35) baada ya dawa ya utajiri aliyowapa kuonekana haifanyi kazi

Anadaiwa kuwaahidi wateja wake utajiri

Soma - https://jamii.app/MgangaAua

#JFMatukio
UTABIRI TMA: KIMBUNGA BATSIRAI KUPIGA KUSINI MAGHARIBI MWA BAHARI

Kimbunga hicho kilijitokeza Januari 27, 2022 na kimesogea Kisiwa cha #Madagascar

Mamlaka imesema uchambuzi unaonesha kutokuwepo kwa uwezekano wa Kimbunga kufika Pwani ya #Tanzania

Soma - https://jamii.app/BatsiraiCyclone
GEITA: Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Naomi amejinyonga kwa kamba ya manila katika choo cha nyumba ya wageni inayomilikiwa na Mumewe

Alifika kwenye nyumba hiyo na kuomba mhudumu amsaidie kumshika Mtoto wa miezi minne akidai anajisikia vibaya

Soma - https://jamii.app/NyumbaYaWageni

#JFMatukio
RIPOTI UN: MALI YAONGOZA KWA VIFO VYA WALINDA AMANI MIAKA 8 MFULULIZO

Wanajeshi 24 na Mfanyakazi 1 wa UN waliuawa Mwaka 2021 huku 19 kati yao wakiuawa nchini Mali

> Inaelezwa kuwa hakuna aliyekamatwa wala kuwajibishwa kwa mauaji hayo


Soma - https://jamii.app/DeathPeaceKeepers

#HumanRights
ARUSHA: James Sindio (16) anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua kaka yake, Zakayo Sindio walipogombana kuhusu kulisha mifugo

> Baba mzazi wa watoto hao, Paulo Sindio alikwenda kuwaamua alikuta tayari Zakayo amechomwa kisu na James

Soma https://jamii.app/NduguWauana

#JFMatukio
MBEYA: Gloria Kibira (38) ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto cha Kabwe, Kata ya Iyela amekutwa amenyongwa kwenye nyumba yake ndani ya eneo la Kituo cha Mahabusu

Watu wawili wanahojiwa kubaini chanzo cha mauaji

Soma - https://jamii.app/MbeyaAnyongwa

#JFMatukio
#AFCON2021: #TeamSenegal imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga #TeamEgypt 4-2 kwa mikwaju ya penati

Hii ni mara ya kwanza kwa Senegal kutwaa Ubingwa huo baada ya kucheza jumla ya Fainali tatu za #AFCON

Soma https://jamii.app/SenegalAFCON

#JFSports
TUNISIA: RAIS SAIED AVUNJA BARAZA KUU LA MAHAKAMA

Kitendo hicho kimetajwa kuwa kinyume na Sheria, huku Majaji wakisema hawatokaa kimya. Rais amewashutumu Majaji kwa upendeleo na ufisadi

Julai 2021, Rais huyo alisitisha shughuli za Bunge

Soma - https://jamii.app/TunRaisMajaji

#Democracy