JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UFARANSA: Watu 13 wamekamatwa kwa kutengeneza na kuuza vyeti bandia 62,000 vya #COVID19 jijini Paris na Lyon

Uchunguzi umebaini kundi hilo la wahalifu lilidukua akaunti ya nesi wa kituo cha Afya na kuanza kufoji vyeti hivyo

Soma - https://jamii.app/FakeCOVID19Pass

#UVIKO3
#ETHIOPIA: Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya ya Njaa Kaskazini mwa Nchi hiyo, ikielezwa takriban 40% ya Wakazi wa Tigray wana uhaba wa chakula

Imeelezwa, hakuna msafara wa chakula ambao umefika #Tigray tangu katikati ya Desemba 2021

Soma https://jamii.app/HungerEth

#HumanRights
Ubalozi wa Ufaransa umeitahadharisha Serikali ya #Kenya kuhusu tishio la Kigaidi linalotarajiwa kutokea Magharibi mwa Nchi hiyo mwishoni mwa wiki

Maeneo yanayotakiwa kuepukwa ni Hoteli, Kumbi za Sterehe, na Maduka makubwa jijini #Nairobi

Soma - https://jamii.app/UgaidiKenya

#Governance
INDIA: MAAMBUKIZI YA COVID-19 YAPUNGUA DELHI, MIGAHAWA YAFUNGULIWA

Migahawa, baa na kumbi za sinema zitaruhusiwa kufanya kazi kwa sharti la kuchukua watu 50% ya uwezo

#Delhi ilikuwa miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na Wimbi la Tatu

Soma https://jamii.app/COVIDDelhi

#UVIKO3
👍1
HOJA: IMANI ZA KISHIRIKINA ZINAONGEZA UADUI, TUZIACHE

Anasema ushirikina husababisha kutoendelea kwani Watu huogopa kufanya maendeleo kwa hofu ya kurogwa

Aidha, mauaji ya wenye Ulemavu wa Ngozi na Wazee maeneo mbalimbali yanasababisha na imani hizi

Soma https://jamii.app/ImaniUshirikina

#JFMdau
ECOWAS YASIMAMISHA UANACHAMA WA BURKINA FASO

Kufuatia Mapinduzi ya Kijeshi, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza kusitisha Uanachama wa #BurkinaFaso

Kwa sasa haijaweka vikwazo vyovyote dhidi ya Taifa hilo

Soma - https://jamii.app/UanachamaBF

#JFDiplomasia
Waziri wa Elimu, Prof. Adolf Mkenda ameitaka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kutengeneza vipuri vya vyombo vya moto

> Amesisitiza DIT kuendelea kujenga ushirikiano na taasisi nyingine ili kubadilishana wataalamu na kukuza teknolojia

Soma https://jamii.app/DITVipuri

#JFElimu
DAR: SERIKALI KUKABILIANA NA UHALIFU MTANDAONI

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni asema Teknolojia inavyozidi kutanuka ndiyo matatizo ya uhalifu wa kimtandao yanavyoongezeka

Amesema lazima Jeshi liwe tayari kudhibiti uhalifu huo

Soma - https://jamii.app/UhalifuMtandao

#DigitalRights
UTURUKI: Rais Recep Tayyip Erdogan ametishia Vyombo vya Habari kuchukuliwa hatua vikisambaza maudhui aliyodai yanaharibu Maadili ya Nchi

Mara kadhaa, amekuwa akikosoa maudhui yasiyoendana na maadili yanayopendekezwa na Chama chake

Soma - https://jamii.app/MaudhuiTurkey

#PressFreedom
MJUE JENERALI MSTAAFU MUSUGURI, MWENYE MIAKA 102

Jenerali mstaafu David Bugozi Waryoba Musuguri amezaliwa Januari 4, 1920

> Amelitumikia Jeshi la Mkoloni, Tanganyika Rifles na JWTZ. Alistaafu mwaka 1988, anaishi Butiama akijishughulisha na kilimo

Soma https://jamii.app/Musuguri

#JFMaarifa
#AFCON2021: EGYPT YAINGIA NUSU FAINALI

- #TeamEgypt imefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuifunga #TeamMorocco goli 2-1 baada ya dk 120

- Egypt itakutana na #TeamCameroon kwenye nusu fainali

- Mechi inayofuata ni kati ya #TeamSenegal na #TeamEquatorialGuinea

#JFSports
#AFCON2021: SENEGAL YAINGIA NUSU FAINALI

- #TeamSenegal imefanikiwa kuingia nusu fainali baada ya kuifunga #TeamEquatorialGuinea goli 3-1

- Senegal itakutana na #TeamBurkinaFaso kwenye nusu fainali

#JFSports
BURKINA FASO: Wanajeshi wakisaidiana na Vikosi vya #Ufaransa wamewaua takriban Magaidi 60 kati ya Januari 16, 2022 hadi Januari 23, 2022

Burkina Faso inakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wenye uhusiano na Al-Qaida na Islamic State tangu 2015

Soma https://jamii.app/Magaidi60
YEMEN: Ripoti ya UN inasema Watoto 2,000 waliosajiliwa na Waasi wa Kihouthi kuwa wapiganaji walifariki vitani, kati ya Januari 2020 - Mei 2021

Wahouthi hutumia Misikiti na Shule kueneza nadharia zao. Vita vya #Yemen vimedumu kwa miaka 7

Soma https://jamii.app/ChildDeathYemen
#ChildSafety
MISS USA 2019 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJIRUSHA GHOROFANI

Kwa mujibu wa Polisi, Cheslie Kryst (30) amefariki baada ya kujirusha ghorofani Manhattan, New York

Kabla ya kifo chake aliweka picha yenye ujumbe "Siku hii ikuletee Pumziko la Amani" Instagram

Soma - https://jamii.app/MissUSA

#JFMatukio
Waziri wa Habari, Nape Nnauye ametangaza kufanyika kwa mabadiliko kwenye Kanuni, ikiwemo namba 18 ya mwaka 2018 inayohusiana na miundombinu ya utangazaji wa kidigitali

Marekebisho hayo yamepelekea Chaneli za bure zionekane tena kwenye DStv

Soma - https://jamii.app/LocalChannelsLaw

#JFSheria
VIASHIRIA/TABIA HATARISHI KWA MTU ANAYETAKA KUJARIBU KUJIUA

1. Miongoni mwa dalili za Watu wanaotaka kujiua ni upweke au kujitenga. Mara nyingi Watu wanaofikiria kujiua huwa wanakwepa mwingiliano na wengine, hupenda kuwa wenyewe

2. Kufanya Mazungumzo ya kujiua: Kuna baadhi ya Watu ambao hupenda kuzungumzia kuhusu kujiua au kuua wengine. Wanasaikolojia wanaonya Watu hawa wasichukuliwe kimasihara

Soma - https://jamii.app/SuicideWarningSigns
#SuicideAttempts
KENYA: TAKRIBAN WATU 13 WAHOFIWA KUFARIKI KWENYE MLIPUKO

Mlipuko umetokea leo, Januari 31 asubuhi ktk eneo la Mandera baada ya Daladala kukanyaga Bomu lililokuwa limetegwa ardhini

Mlipuko umetokea Siku 2 baada Ufaransa kutoa tahadhari ya Shambulio

Soma - https://jamii.app/ManderaBombKE

#JFMatukio
TANGA: Watu watano wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na mapanga, huku wengine 3 wakijeruhiwa katika mapigano ya wakulima na wafugaji yaliyotokea Kijiji cha Kibirashi na Elerai Wilayani Kilindi

Mgogoro wa ardhi umetajwa kuwa chanzo cha mapigano

Soma - https://jamii.app/5WauawaTanga

#JFMatukio