JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TCRA YAZUIA KIPINDI CHA EFATHA KWA MIEZI MITATU

Kamati ya Maudhui ya TCRA imesema Kituo cha Star TV kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries kwa kuruhusu maudhui yenye ukakasi, kinyume na Kanuni za Mawasiliano

Star TV yapewa onyo na kuamriwa kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo

Soma - https://jamii.app/EFATHA-TCRA

#DigitalRights
WAZIRI UMMY: MADUKA YA DAWA YALIYO NDANI YA MITA 500 ZA HOSPITALI KUONDOLEWA

Asema yapo kinyume cha Sheria, akihoji "Hospitali Dawa hakuna lakini kwenye Maduka ya Nje zipo"

Ni siku chache baada ya Wadau ndani ya JamiiForums.com kusema yanachangia kukosekana kwa Dawa Hospitalini

Soma https://jamii.app/MadukaDawa

#JFAfya
UHOLANZI: Polisi Nchini humo wamemkuta Mtu mmoja akiwa hai ktk Uwanja wa Ndege wa #Amsterdam ambapo alijibanza kwenye Tairi la mbele

Safari kutoka Afrika Kusini hadi Amsterdam huchukua Saa 11 ambapo Ndege hupumzika kwa Saa 1 #Nairobi, Kenya

Soma - https://jamii.app/MzamiajiAmsterdam

#JFMatukio
ELIMU YA SARATANI ITOLEWE KWA WATANZANIA

Mshiriki wa #StoriesOfChange anasema hapa Nchini, watu wachache tu ndiyo wana Elimu sahihi kuhusu visababishi na Matibabu ya Saratani

Anasema watu waishio maeneo ya Vijijini na yasiyo na Huduma nzuri za Afya wanapata Elimu hiyo wakishapata Ugonjwa, jambo ambalo haliwasaidii

Anashauri Serikali na wadau wengine kuweka kipaumbele kwenye suala hili

Soma - https://jamii.app/CancerSOC

#JFAfya
ATHARI ZA COVID-19 KWENYE SEKTA YA ELIMU

#CoronaVirus imeathiri Sekta ya Elimu Duniani kote, na masomo ya takriban Wanafunzi Bilioni 1.6 wa Shule na Vyuo yaliathiriwa mwanzoni mwa mlipuko huo

Watoto kutoka Familia za chini hawakupata nafasi ya kuendelea na Masomo yao kama wengine kutokana na changamoto za Umeme na Vifaa vya kielektroniki

Soma - https://jamii.app/WorldEduDay

#EducationDay #JFElimu
ISRAEL YADHIBITI #OMICRON BAADA YA KUTOA DOZI YA NNE

Wizara ya #Afya ya Israel imesema Watu wenye umri wa miaka 60 na kuendelea waliopata Chanjo ya nne wameonesha kuwa na kinga ya Ugonjwa mara tatu zaidi kuliko wale waliopata Dozi tatu

Soma - https://jamii.app/DoziYaNne

#UVIKO3 #JFAfya
DAR: Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla amesema Kamati imebaini Moto uliounguza Soko la Karume ulisababishwa na mshumaa uliowasha na mateja wanaojihifadhi katika vibanda

Wafanyabiashara wameruhusiwa kurejea na Serikali imeweka mpango mzuri kuzuia Moto

Soma - https://jamii.app/MatejaMoto

#JFMatukio
MWANZA: WALIOHUSIKA NA MAUAJI YA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAKAMATWA

Jeshi la Polisi limesema waliokamatwa wamekiri kufanya mauaji chanzo kikiwa migogoro ya kibiashara

> Panga lililotumika kwa mauaji lipo kwa mkemia ili kupimwa vinasaba

Soma https://jamii.app/MauajiMwanza

#JFMatukio
TOZO ZA SIMU NI KIKWAZO KWA UCHUMI WA KIDIGITALI NCHINI

Mshiriki wa Stories of Change anasema Serikali imeweka Tozo ili kupata Fedha lakini gharama zitashindwa kuwavutia Watu zaidi hivyo Uchumi wa Kidigitali unaweza kuporomoka

Soma - https://jamii.app/TozoDigitali

#StoriesOfChange #DigitalRights
BURKINA FASO: JESHI LAMPINDUA RAIS KABORE. LASIMAMISHA KATIBA NA KUVUNJA SERIKALI

Mbali na Rais Roch Kabore kupinduliwa, Jeshi pia limesema Bunge limevunjwa na Mipaka ya Nchi imefungwa

Jeshi limesisitiza Mchakato huo umefanyika bila ghasia

Soma - https://jamii.app/KaboreOusted

#Democracy #Governance
MALAWI: BARAZA LA MAWAZIRI LAVUNJWA KWA KASHFA ZA UFISADI

Kashfa za ubadhirifu wa mali za umma za baadhi ya Mawaziri zikijumuisha kuchepusha fedha za #COVID19 na kuingia mikataba ya kifisadi imepelekea Rais Chakwera kulivunja Baraza la Mawaziri

Soma https://jamii.app/MalawiCabinet

#Accountability
CAMEROON: WATU SITA WAFARIKI NA 40 WAJERUHIWA KTK MKANYAGANO

Watu takriban 50,000 walikuwa wakitaka kushuhudia mechi kati ya #TeamCameroon na #TeamComoros ktk michuano ya #AFCON2022

Hospitali iliyo jirani na uwanja wa Olembe imepokea majeruhi 40

Soma - https://jamii.app/6AFCON

#JFSports
LINDA TAARIFA ZAKO BINAFSI MTANDAONI

Taarifa binafsi kama Jina lako, Namba ya Simu na Anwani huweza kuleta madhara zikiwa mtandaoni bila kulindwa, kwani ni rahisi kudukuliwa

Weka Password imara kwenye kifaa chako cha kielektroniki

Soma - https://jamii.app/UlinziTaarifa

#DataProtection
JE, WAJUA: Kahawa aina ya Arabika inauzwa kwa bei kubwa kuliko Robusta ktk soko la dunia

Kwa kipindi cha Mwaka 2002 hadi 2021 Arabika iliuzwa hadi kwa Tsh. 15,250 kwa Kg, na bei kubwa ya Robusta iliyorekodiwa kwa kipindi hiko ni Tsh. 8,550

Soma - https://jamii.app/ArabikaRobusta

#JFBiashara
WHO: CORONA INAWEZA KUISHA MWISHO WA MWAKA 2022

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ikiwa nchi zote zitachukua hatua zinazostahili, #COVID19 inaweza kuisha kufikia mwishoni mwa 2022

Soma https://jamii.app/Corona2022

#JFAfya #UVIKO3
👍1
SARATANI NI NINI?

Miili yetu ina chembechembe hai nyingi ambazo huzaliana, hukua, na kufa kwa mpangalio maalum

Chembechembe za Saratani zinazaliana haraka zaidi bila mpangilio na kukua haraka

Zisipotibiwa mapema zinaweza kusambaa na kuota sehemu nyingine mwilini

Soma - https://jamii.app/SarataniOR

#JFAfya #Cancer #Saratani
TMA YATABIRI UPEPO MKALI NA MAWIMBI

Tahadhari ya Upepo mkali unaozidi Kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi yakiwemo Dar, Tanga, Mtwara, Visiwa vya Unguja na Pemba

Soma - https://jamii.app/UpepoTMA

#JFMatukio
DAR: MACHINGA WAOMBA UWAKILISHI KWENYE VYOMBO MBALIMBALI

Pia, wamesema maeneo mengi waliyopelekwa baadhi yao hayana miundombinu rafiki, na yana ukosefu wa wateja

Wapendekeza maeneo hayo kuboreshwa ili wasirudi walipohamishwa

Soma - https://jamii.app/MachingaRaisIkulu

#JFBiashara
👍1
MACHINGA KUWA MIONGONI MWA MAKUNDI MAALUM

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inawatambua rasmi Machinga kama kundi maalum, na litakuwa moja ya Makundi yatakayohudumiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalum

Soma - https://jamii.app/MachingaRaisIkulu

#JFBiashara
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ina mipango kadhaa ya kuhakikisha Wafanyabiashara wadogo wanapata mitaji kwa urahisi

Aidha, ameagiza Benki kuja na Mifumo kwaajili ya kuwasaidia Wanawake na Vijana, ambayo itakuwa ikitoa huduma ya Mikopo

Soma - https://jamii.app/ProgramBenki

#JFSiasa