JamiiForums
βœ”
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS SAMIA AWATAKA VIONGOZI WAENDELEE KUSIMAMIA UTOAJI CHANJO

Asema waliopata Chanjo hawapati madhara kama wasiopata Chanjo

Ameongeza Tanzania imekumbwa na mawimbi kadhaa na kwasasa kuna wimbi la 4 ambalo halijaua sana kama yaliyotangulia

Soma - https://jamii.app/ChanjoViongozi

#UVIKO3 #JFAfya
Rais Samia amesema baada ya kujenga Masoko na kuboresha maeneo wataweka Kodi itakayotakiwa kulipwa na Machinga ambapo amewaasa walipe kadiri itakavyowekwa

Pia, amewaasa kutotumika na wenye Maduka kusambaza Bidhaa hali inayoinyima Serikali Kodi

Soma - https://jamii.app/KodiMachinga

#JFSiasa
KENYA YARUHUSU NDEGE ZA ABIRIA KUTOKA UMOJA WA FALME ZA KIARABU KUTUA

Januari 10, 2022, Kenya ilizuia Ndege za Abiria toka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kutua Nchini humo baada ya marufuku iliyowekwa na UAE dhidi ya Ndege za Abiria toka Kenya

Soma https://jamii.app/UAEVsKenya

#JFSiasa
NINI HUSABABISHA SARATANI?

Hakuna sababu moja, Saratani tofauti zina vyanzo vyake. Miongoni mwa Visababishi visivyozuilika ni Umri

Umri unapokuwa mkubwa, uwezekano wa kutokea dosari katika mabadiliko ya DNA yanayosababisha Kansa huongezeka

Baadhi ya Visababishi vinavyozuilika ni pamoja na uvutaji wa sigara, ulaji mbovu, kutumia pombe kupita kiasi na kutofanya mazoezi

Soma - https://jamii.app/SarataniOR

#JFAfya #Cancer #Saratani
MDAU: FIKRA BORA NA UHURU WA MAONI VITACHOCHEA MAPINDUZI YA KIUCHUMI

Anashauri;

1) Mfumo wa Elimu ulenge kujenga zaidi uwezo: Anasema bado Tanzania ina changamoto kwani Jamii imeshaamini kusoma ni kuruka Vidato na sio kupima mtu anafahamu nini

2) Kuondoa Sheria zinazominya Uhuru wa Maoni: Kuwa na jamii iliyofungwa mdomo humaanisha Serikali itabaki kuamini Sera zake ni nzuri hata kama si uhalisia

Soma - https://jamii.app/FikraUhuruSOC

#StoriesOfChange #JFMaarifa
RIPOTI: ONGEZEKO LA UFISADI LINAKANDAMIZA HAKI ZA BINADAMU

Ripoti ya Transparency International inasema #COVID19 imetumiwa na Nchi nyingi kama kisingizio cha kuacha kufanya ukaguzi

Serikali zatakiwa kuwa wazi kuhusu namna Fedha zinavyotumika

Soma - https://jamii.app/RipotiUfisadi

#HumanRights
JE, UNAYAFAHAMU MAGARI YENYE UWEZO WA KUTEMBEA NCHI KAVU NA MAJINI?

Yanaitwa β€˜Amphibious Vehicles’ ambapo huwa na Injini kwa ajili ya kutembea Nchi kavu na propela ili kutembea Majini

Magari haya hayahitaji uwepo wa gati kuingia kwenye Maji

Soma https://jamii.app/AmphibiousVehicles

#JFMaarifa #JFGarage
#AFCON2021: SENEGAL YAFUZU KUCHEZA ROBO FAINALI

- #TeamSenegal imefuzu baada ya kuifunga #TeamCapeVerde goli 2-0 ndani ya dk 90. Wachezaji wawili wa Cape Verde walipewa kadi nyekundu

- Senegal itakutana na mshindi wa mechi kati ya #TeamMali na #TeamEquatorialGuinea

#JFSports
MOROCCO YAFUZU KUCHEZA ROBO FAINALI #AFCON2021

- #TeamMorocco imefuzu kwa kuifunga #TeamMalawi goli 2-1 ndani ya dk 90

- Morocco itakutana na mshindi kati ya #TeamCotedIvoire na #TeamEgypt

- Hii ilikuwa ni mechi ya 10 ya Malawi kwenye michuano na imeshinda mechi 2

#JFSports
MTWARA: MAAFISA POLISI 7 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAUAJI

Wanatuhumiwa kwa mauaji ya Mfanyabishara Mussa Hamisi Hamisi aliyekuwa akiwadai Maafisa hao zaidi ya Tsh. Milioni 33.7

Inadaiwa walijipatia fedha hizo wakati wakimfanyia upekuzi

Soma - https://jamii.app/MaafisaPolisiMauaji

#JFUwajibikaji
IDARA YA HABARI TANESCO YAVUNJWA KWA KUSHINDWA KUTIMIZA MAJUKUMU YAKE

Waziri January Makamba amesema Serikali haifurahishwi na malalamiko ya Wananchi kuhusu kukatika kwa Umeme na upungufu wa taarifa zinazotolewa kwa Wateja

Soma - https://jamii.app/MawasilianoTANESCO

#Accountability
πŸ‘1
MEXICO: WANAHABARI WAANZA MAANDAMANO YA NCHI NZIMA KUKEMEA MAUAJI YA WENZAO

Maandamano hayo yanakuja baada ya Waandishi wa Habari watatu kuuawa tangu kuanza mwaka 2022

#Mexico inatajwa kuwa miongoni mwa Mataifa hatari zaidi duniani kwa Wanahabari

Soma - https://jamii.app/JournalistsMexico

#PressFreedom
πŸ‘1
Ili kupambana na athari ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, Naibu Waziri, David Silinde amewaagiza Ma-RC na DC's kusimamia zoezi la kila Mwanafunzi kupanda Mti mmoja kila Mwaka

#Tanzania hupoteza Hekta laki nne za Misitu kutokana na shughuli mbalimbali

Soma - https://jamii.app/MitiShuleni

#JFSiasa
UTALII: NUSU YA SIMBA DUNIANI WANAPATIKANA TANZANIA

Rais wa Jumuiya ya Uwindaji ya Kimataifa (SCI), Sven Lindqueast ameipongeza #Tanzania kwa juhudi za utunzaji Wanyamapori

Tanzania inakusudia kukomesha Ujangili kwa 90% ifikapo 2025

Soma - https://jamii.app/SimbaTz

#Utalii
PFIZER NA BioNTech WAANZA MAJARIBIO YA CHANJO YA #OMICRON

Majaribio yatajumuisha Watu zaidi ya 1,400 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 55

Wamegawanywa ktk makundi; waliopata Chanjo 2, waliopata Chanjo 2 na Booster, na wale wasiopata Chanjo

Soma - https://jamii.app/OmicronChanjo

#UVIKO3 #JFAfya
DODOMA: Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya #Tanzania, Mustapha Siyani amewataka Watumishi wa Mahakama kutenda Haki kwa kuondoa urasimu ktk uendeshaji kesi

Asema Mahakama inaposhindwa kutoa Haki husababisha Wananchi kujichukulia Sheria mkononi

Soma - https://jamii.app/MahakamaHaki

#JFUwajibikaji
πŸ‘Ž1
SERIKALI: 3,147 WALILAZWA KUTOKANA NA CORONA KATI YA SEPTEMBA 2021 - JANUARI 23, 2022

Waziri Ummy Mwalimu asema kati yao 2,990 hawakuwa wamechanjwa

Wagonjwa 31 walikuwa mahututi ICU Januari 23, 2022 na kati yao 30 walikuwa hawajapata chanjo

Soma https://jamii.app/WizaraUVIKO

#UVIKO3 #JFAfya
#COVID19: Korea Kusini imerekodi maambukizi 13,102 huku Mamlaka zikionya Kirusi cha Corona aina ya #Omicron kinaweza kuchangia hadi 90% ya maambukizi mapya wiki zijazo

Ni mara ya kwanza Visa zaidi ya 13,000 kurekodiwa katika Taifa hilo

Soma - https://jamii.app/OmicronSK

#UVIKO3 #JFAfya
MARA: Naibu Waziri, Sagini Jumanne ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka wanaodaiwa kuwatapeli Wanakijiji wa Mwanza-Buriga

Waliwashawishi Wananchi kujiunga na Kanisa lao kwa kuchangia Tsh. 20,000 kwa ahadi ya kuwapa Mchele 90Kg, Mafuta na Sabuni

Soma - https://jamii.app/Mara20000

#JFMatukio
#ETHIOPIA: SERIKALI YARIDHIA KUONDOA HALI YA DHARURA

Hali ya Dharura ya miezi 6 iliwekwa Novemba 2021 baada ya Vikosi vya #Tigray kusema vinaelekea Addis Ababa

Serikali imesema sasa vitisho vinaweza kudhibitiwa kupitia taratibu za kawaida

Soma - https://jamii.app/HaliDharuraEth

#Governance