JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#AFCON2021: NANI KUWA BINGWA?

Michuano hiyo inaanza kesho Januari 9, kwa wenyeji #TeamCameroon kuivaa #TeamBurkinaFaso majira ya saa 1:00 jioni (EAT)

#TeamAlgeria ambaye ni Bingwa Mtetezi, #TeamCameroon, #TeamSenegal na #TeamEgypt zinapewa nafasi kubwa kuwa Bingwa

#JFSports
JWTZ wamekanusha taarifa zilizochapishwa katika YouTube channel ya News24 ikiwa na kichwa 'MKUU WA MAJESHI AINGILIA KATI SAKATA LA RAIS NA SPIKA'

> Wamesema wanafanya kazi kwa weledi na hawaingilii masuala ya kisiasa

Soma https://jamii.app/KanushoJWTZ

#Accountability
#AFCON2021: CAMEROON YAANZA KWA USHINDI

- Mtayarishaji wa Mashindano hayo #TeamCameroon imeanza kwa ushindi wa goli 2-1 dhidi ya #TeamBurkinaFaso katika mchezo wa ufunguzi

- Mchezo unaofuata saa 4:00 usiku (EAT) ni kati ya #TeamEthiopia na #TeamCapeVerde

#JFSports
KILIMANJARO: BINTI ADAIWA KUMUUA MAMA YAKE KWA TAMAA YA MALI

Wendy anadaiwa kumuua Mama yake mzazi (Mama Ipepu) ambaye ni Nesi mstaafu wa KCMC

Ni takriban mwaka sasa watu wamekuwa wakimuulizia Mama huyo na kuambiwa amekwenda kutibiwa nje ya Nchi

Soma - https://jamii.app/BintiKifoMama

#JFMatukio
USWISI: WANAJESHI WATAKIWA KUACHA KUTUMIA WHATSAPP, SIGNAL NA TELEGRAM

Kwasababu ya ulinzi wa taarifa, Wanajeshi wametakiwa kutumia Mtandao wa Uswisi uitwao Threema Messenger

Jeshi litagharamia kuwa na Threema ambayo ni Dola 4.35 (Tsh. 8,900)

Soma - https://jamii.app/SwissArmy

#Governance
#KAZAKHSTAN: Jumla ya Watu 164 wameuawa tangu yalipoanza machafuko yaliyotokana na maandamano wiki moja iliyopita

Ktk machafuko hayo, zaidi ya Watu 5,000 wamekamatwa na Mamlaka za Nchi hiyo. Raia wanapinga kupanda kwa bei ya Mafuta

Soma - https://jamii.app/DeathTollKaza
#HumanRights
IKULU, CHAMWINO: Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan awaapisha Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu aliowateua Januari 8, 2022

Uapisho huo unafanyika Ikulu, Chamwino, Dodoma

Fuatilia - https://jamii.app/UapishoIkuluDodoma

#Governance
NAIBU SPIKA: KAZI YA BUNGE SIO KUKOSOA SERIKALI TU

Dkt. Tulia Ackson asema itakapohitajika watakosoa Serikali kwa heshima na kuzingatia muktadha

Amesema Rais ni Mkuu wa Serikali na ni Mkuu wa Nchi, hayuko sawa na wakuu wa Mihimili mingine

Soma - https://jamii.app/RaisVsBunge

#Governance
RAIS SAMIA: LUKUVI HATOKUWA SPIKA WA BUNGE

Akanusha uvumi William Lukuvi ameandaliwa kuwa Spika wa Bunge baada ya kutoteuliwa katika Baraza la Mawaziri

Pia, amekanusha kuwa Lukuvi ni kati ya watu waliokuwa wanataka kugombea Urais 2025

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluDodoma

#Governance
RAIS SAMIA: NILIWAACHA LUKUVI NA PROF. KABUDI ILI WAJE KWANGU KUWASIMAMIA MAWAZIRI

Amesema amewaacha Wiliam Lukuvi na Prof. Palamagamba Kabudi kwasababu ya umri, hivyo atafanya nao kazi kwa ukaribu ili kuweza kuwasisimamia mawaziri

Soma - https://jamii.app/UapishoIkuluDodoma

#Governance
UTAFITI: GONGO HUSABABISHA SARATANI YA TUMBO

Shirika la Kimataifa la Utafiti wa Saratani, IARC limebaini gongo, Chang'aa na Kachasu zinasababisha Saratani ya Tumbo hasa kwa wanaume

Saratani hii imeshamiri zaidi Kusini na Mashariki mwa Afrika

Soma https://jamii.app/GongoSaratani

#JFAfya
SOMALIA: Viongozi wa kisiasa wamefikia makubaliano ya kukamilisha Uchaguzi wa Bunge la chini kati ya Januari 15 na Februari 25, 2022

Waziri Mkuu na Rais wamekuwa wakijibizana kuhusu zoezi hilo, hali iliyozua wasiwasi wa ghasia Nchini humo

Soma https://jamii.app/UchaguziSomalia
#Democracy
Aliyewahi kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, Bunge la Afrika(PAP), Stephen Masele na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson wamechukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea Uspika wa Bunge

Wengine waliojitokeza ni Patrick Nkamah na Godwin Kunambi

Soma https://jamii.app/SpikaWaBunge

#Governance #Democracy
MDAU: MAONESHO YA VYAKULA VYA ASILI NI FURSA NZURI YA KUKUZA UTALII

Anasema Tanzania bado hatujanufaika na Utalii wa matukio na maonesho (Event Tourism) kwa namna ya kuridhisha. Hatujaweza kuandaa maonesho makubwa ya kitamaduni ambayo yangeweza kuvutia Watu

Mfano #Brazil huvutia maelfu ya Watu katika ngoma yao ya Samba. #Tanzania tunaweza kuanzisha maonesho ya vyakula vya asili na kuandaa msimu wa maonesho hayo ambayo ungepambwa na matukio mbalimbali

Soma - https://jamii.app/VyakulaUtalii

#StoriesOfChange #JFMdau
UTAFITI: COVID-19 YABAINIKA KUSHUSHA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME

Utafiti uliofanywa kwa Wanaume 120 waliougua na kupona #COVID19 nchini Ubelgiji umebaini ujazo wa mbegu za kiume hupungua kwa wanaume baada ya kupata Ugonjwa huo

Soma - https://jamii.app/MbeguZaKiume

#JFAfya
#AFCON2021: GUINEA, MOROCCO ZAPATA USHINDI

Mchezo wa 2 wa Kundi B kwa siku ya leo, umemalizika kwa #TeamGuinea kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya #TeamMalawi

Pia, mchezo wa kwanza wa Kundi C kwa leo, umemalizika kwa #TeamMorocco kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya #TeamGhana

#JFSports
KAZAKHSTAN: Rais Kassym-Jomart Tokayev amesema Nchi imerejea katika utulivu, na maandamano yaliyotokea yalikuwa ni jaribio la mapinduzi

Wananchi waliandamana kupinga ongezeko la bei za mafuta. Watu zaidi ya 150 waliuawa kwenye machafuko hayo

Soma https://jamii.app/KazakhstanMapinduzii

#Governance
MYANMAR: KIONGOZI WA KIRAIA AONGEZEWA MIAKA 4 JELA

Mahakama Nchini #Myanmar imemhukumu tena Aung San Suu Kyi miaka mingine 4 kwa kumiliki na kuingiza vifaa vya mawasiliano kinyume cha #Sheria na kuvunja masharti ya kupambana na #COVID19

Soma - https://jamii.app/Suu4yrsJail
#Democracy
UGANDA: SHULE ZAFUNGULIWA BAADA YA MIAKA TAKRIBAN MIWILI

Ili kudhibiti usambaaji wa maambukizi ya #COVID19, Uganda ilifunga Shule tangu Machi 2020

> Mtaala utawekwa sawa ili kuwasaidia Wanafunzi ambao hawakutumia Teknolojia kuendelea kujifunza

Soma https://jamii.app/ShuleUganda

#Governance #JFElimu
AJALI SIMIYU: Takriban Watu 14 wamefariki Dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana

Kati ya waliopoteza maisha ni Waandishi wa Habari 5 waliokuwa katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza

Soma - https://jamii.app/Ajali14Simiyu

#JFMatukio