JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
JE, WAJUA KUWA SPIKA SIO LAZIMA AWE MBUNGE?

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Ibara ya 84(9) iwapo mtu asiye Mbunge akichaguliwa kuwa Spika wa Bunge atatakiwa kuapa kiapo cha Uaminifu

Soma - https://jamii.app/SpikaBunge

#JamiiForums #JFMaarifa
MBINU UNAZOWEZA KUTUMIA KULINDA AFYA YA MACHO YAKO

1. Unashauriwa kuvaa Miwani ya kuzuia Mionzi ya Jua ili kuzuia Mionzi ya UV na hakikisha unatumia Miwani yenye uwezo wa kuzuia Mionzi kwa 99%-100%

2. Kula Mlo wenye Virutubisho Kamili: Virutubisho muhimu kwa utunzaji wa Macho ni Vitamini A, Vitamini E, Vitamini C, Asidi ya Mafuta ya Omega-3, Zinki, Lutein na Zeaxanthin zinazopatikana kwenye Karoti, Mchicha, Samaki na Mayai.

Soma - https://jamii.app/RoutineEyeCare

#JFAfya #EyeCare
#ZIMBABWE: Rais Emmerson Mnangagwa amemfuta kazi Waziri wa Usalama wa Nchi hiyo, Owen Ncube kwa kufanya vitendo visivyofaa kama Kiongozi wa Serikali

Owen anadaiwa kuwatisha baadhi ya Wanachama wa ZANU-PF ktk Uchaguzi wa ndani hivi karibuni

Soma - https://jamii.app/OwenOutZimb

#Accountability
UTAFITI: MAFUA YANAWEZA KUZUIA KUPATA #COVID19

Watafiti wa Imperial College of London wamebaini 'T-Cells' husaidia kuzuia maambukizi. Mafua yamebainika kuzalisha 'T-Cells' nyingi

Chanjo imetajwa kuwa njia thabiti kukabiliana na Corona

Soma - https://jamii.app/CommonCold

#UVIKO3 #JFAfya
RAIS SAMIA: AJIRA NDIYO NGUZO YAKO YA MAISHA, SIO 'BY THE WAY'

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kubadilika wakiajiriwa sekta binafsi hata Serikalini huku akiongeza "sekta binafsi ukizubaa nafasi yako inachukuliwa"

Amefafanua "Nilishawahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, wakati ule kesi nyingi nilizokuwa nikipokea ni uzembe, kutokuwa na nidhamu sehemu za kazi, umefiwa na shangazi wa shangazi yako unakwenda kuzika bila kutoa taarifa"

Soma - https://jamii.app/SamiaAjira

#Governance
MDAU: MAMBO YANAYOWEZA KUKUSABABISHIA LAANA KWENYE MAISHA

1. Kumdhulumu Mtu: Jasho la Mtu huzaa mikosi. Machozi na manung'uniko anayoyatoa Mtu aliyeumizwa kwa kudhulumiwa, hugeuka laana

2. Kuua au kutoa kafara: Damu ya Mtu ni laana, Damu ya Mtu ni mkosi, Damu ya Mtu ni nuksi. Ukisikia kuwa kuna vitu havina midomo lakini vinaongea, basi ni Damu ya Mtu

3. Kumkana au kumtukana Mzazi: Vitabu vya Mungu vinaeleza, "Waheshimu Baba na Mama upate kheri na miaka mingi Duniani"

Soma - https://jamii.app/TabiaLaana

#StoriesOfChange #JFMdau
KENYA YAZUIA NDEGE ZA UAE

Mamlaka ya Usafiri wa Anga (KCAA) yapiga marufuku ndege za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kujibu marufuku iliyowekwa kwa ndege za Kenya

UAE iliweka marufuku baada ya kubaini udanganyifu katika vipimo vya #COVID19

Soma - https://jamii.app/KenyaVsUAE

#Governance
#UGANDA: MWANDISHI ASHTAKIWA KWA KUTUMA TAARIFA ZA KASHFA DHIDI YA RAIS NA MWANAE

Kakwenza Rukirabashaija anayetuhumiwa kutuma taarifa za kashfa kuhusu Rais na Mtoto wake kwenye #Twitter amefunguliwa mashtaka 2 ya Mawasiliano ya kukera

Soma - https://jamii.app/RukirabashaijaCourt

#FreeSpeech
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mhifadhi William Simon Mwakilema kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)

Anachukua nafasi ya Dkt. Allan Herbert Kijazi ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi

Soma - https://jamii.app/UteuziTANAPA

#Governance
MDAU: KUMPIGA/KUMGOMBEZA MTOTO KWA KUFANYA VIBAYA DARASANI SIO KUMSAIDIA

Anasema Binadamu tunatofautiana uwezo wa kuelewa mambo. Kuna Watoto uwezo wao wa Darasani ni mdogo lakini ana kipaji au uwezo fulani ni vizuri kumuendeleza upande huo ili kumsaidia

Ameongeza, kama Mtoto kila siku anaenda Shuleni, anahudhuria kila kipindi na kufanya kazi za nyumbani (home work), ya nini kumchapa anaposhika namba za chini? Usitumie kigezo kimoja kumpima Mwanao.

Mjadala zaidi - https://jamii.app/KuchapaWttMasomo
#Malezi
HOJA: WOSIA NI JAMBO MUHIMU LINALOSAHAULIKA NA WENGI

Mshiriki wa #StoriesOfChange asema kutoacha wosia husababisha Wajane na Watoto wa Marehemu kupoteza Haki kwa kukosa mwongozo wa mgawanyo wa mali

Ashauri watu kuandika wosia ili kupunguza migogoro

Soma https://jamii.app/WosiaMirathi

#JFMdau
Jamii Forums tunawatakia Watanzania wote Maadhimisho mema ya Miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya #Zanzibar

Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea Mwaka 1964 ili kumuondoa Madarakani Sultani wa Zanzibar na Serikali yake, iliyoundwa hasa na Waarabu

#MapinduziZanzibar #JamiiForums
WHO: 50% YA WATU BARANI ULAYA WATAAMBUKIZWA OMICRON

Shirika la Afya (WHO) lasema nusu ya watu wataambukizwa #Omicron kipindi cha wiki 6 - 8 zijazo

Makadirio yanatokana na Visa vipya Milioni 7 vilivyoripotiwa Ulaya wiki ya kwanza ya 2022

Soma - https://jamii.app/OmicronUlaya

#UVIKO3 #JFAfya
PWANI: Athumani Ramadhani (20), Maneno Hamis (23) na Abdallah Rajabu (21) wamefariki baada ya kulipukiwa na Chuma walichookota kinachodhaniwa kuwa ni bomu

Wanaojihusisha kuuza na kununua Vyuma chakavu watakiwa kuwa waangalifu wanapokusanya

Soma - https://jamii.app/VifoBomuPwani

#JFMatukio
👍1
BURKINA FASO: WANAJESHI 8 WASHIKILIWA KWA NJAMA ZA KUPANGA MAPINDUZI

Burkina Faso imetangaza kuwashikilia Wanajeshi akiwemo Kanali Mohamed Emmanuel Zoungrana ambaye ni mkosoaji wa Serikali

> Wizara ya Haki inaendelea kuchunguza tuhuma hizo

Soma https://jamii.app/BurkinaFasoWanajeshi

#Governance
DAR: Manawa Samson Horera (22) mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amefariki baada ya kujirusha kutoka ghorofa ya pili ktk hostel za Magufuli alipotuhumiwa kwa wizi wa laptop ya mwanafunzi mwenziye

Soma https://jamii.app/AjirushaGhorofani

#JFMatukio
RAIS SAMIA AKUTANA NA NDUGAI MARA YA KWANZA TANGU AJIUZULU

- Rais Samia amekutana na kuzungumza na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai aliyefika Ikulu Chamwino

- Ndugai alijiuzulu Uspika akisema ni kwa hiari na maslahi ya Taifa

Soma https://jamii.app/SamiaNdugai

#JFSiasa
#AFCON2021: REFA AMALIZA MPIRA MARA 2 KABLA YA DK 90

Janny Sikazwe ameibua utata kwenye mechi ya Tunisia na Mali baada ya kumaliza mchezo ktk dk ya 85, kisha kuruhusu uendelee na kumaliza tena ktk dk ya 89.43

- Mali imeshinda kwa goli 1-0

Soma https://jamii.app/RefaJanny

#JFSports
UINGEREZA: WAZIRI MKUU AKUMBWA NA SHINIKIZO LA KUMTAKA AJIUZULU

Upinzani wamemtaka Boris Johnson ajiuzulu kwa kushiriki sherehe iliyokiuka vizuizi vya #COVID19

Boris ameomba radhi na kusema aliuchukulia mkusanyiko huo kuwa wa kikazi

Soma - https://jamii.app/BorisPMQs

#Accountability #UVIKO3
MBEYA: MTOTO AUA BABA YAKE KWA TUHUMA ZA KISHIRIKINA

Jeshi la Polisi linamshikilia Mussa (Mtumishi wa Ruvu JKT) kwa kumuua Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Edward Ndonde kwa kumchoma visu

Mussa alikuwa akimtuhumu Baba yake kuwa mchawi

Soma - https://jamii.app/MauajiNaibuMBY

#JFMatukio