JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTEUZI: Rais Samia amteua Dkt. Baghayo Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)

Charles Itembe ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzo ya Nje (EPZA), na Ernest Mchanga Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha

Soma - https://jamii.app/Uteuzi3Rais

#Governance
MSUMBIJI: Rais Filipe Nyusi na mkewe Isaura Nyusi wamekutwa na #COVID19 na wamelazimika kujitenga

> Nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu 193,000 wanaougua COVID-19, na vifo 2,031

Soma https://jamii.app/FilipeNyusi

#UVIKO3 #JFAfya
SUDAN: WANAHARAKATI WAITISHA MAANDAMANO ZAIDI

Wanaoongoza Kampeni dhidi ya Utawala wa Kijeshi wamesema Waandamanaji watakuwa wakielekea Ikulu hadi ushindi utakapopatikana

Idadi ya waliopoteza maisha tangu Mapinduzi kufanyika imefikia 56

Soma - https://jamii.app/ProtestsSdn

#Democracy
UTAJIRI WA KAMPUNI YA APPLE WAZIDI GDP YA AFRIKA

Kampuni ya Apple imefikisha thamani ya Dola trilioni 3 (takriban Tsh. Trilioni 6,920.88) katika Soko la Hisa

Pato la Ndani la Afrika (GDP) ni Dola Trilioni 2.6 sawa na Tsh. Trilioni 5,998.1

Soma - https://jamii.app/AppleUtajiri

#JFTech
MWIGULU: DENI NI HIMILIVU, TUTAENDELEA KUKOPA

Asema Mkopo sio Msaada na hutolewa kwa mwenye chanzo cha kulipa

Pia, amesema sio uungwana kusema Rais anakopa akisisitiza Marais hawakopi bali ni Serikali akisema "Hilo si jambo la Familia, ni la Nchi"

Soma https://jamii.app/MwiguluDeni

#Governance
👍1
RAIS SAMIA: TANZANIA IMEKUWA IKIKOPA TANGU UHURU

Amesema inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"

Asema "Toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"

Soma - https://jamii.app/RaisTozoMikopo

#Governance
RAIS SAMIA: TAIFA HALIWEZI KUENDESHWA NA TOZO PEKEE

Rais Samia asema kumekuwepo watu wanaohoji kwanini Nchi imekopa japokuwa kuna fedha za tozo, akifafanua kuwa Taifa haliwezi kwenda na fedha za tozo pekee

Amesema kuleta ustawi wa Nchi sio miujiza na ni lazima kutumia mbinu zote zilizopo

Soma - https://jamii.app/SSHTozo

#Governance
RAIS SAMIA KUFANYA MABADILIKO YA BARAZA LA MAWAZIRI HIVI KARIBUNI

Amesema ataenda na wale wote anaohisi wanaweza kwenda naye kuleta maendeleo kwa Watanzania na kwamba wale ambao anahisi ndoto zao ni "kule" atawapa nafasi waende kujiandaa

Asema, "Wakajitayarishe vizuri huko nje kwasababu nikiwatuma ndani nitawasumbua"

Soma - https://jamii.app/RaisBarazaMawaziri

#Governance
RAIS SAMIA: UMEME HAUWEZI KUUNGANISHWA KWA ELFU 27

Rais Samia Suluhu amesema ni ngumu kwa TANESCO kuwaunganishia umeme Watanzania kwa Tsh. 27,000

> Amesema Wananchi wamelipa lakini wanashindwa kuunganishiwa umeme kwa kuwa TANESCO hawana nguzo

Soma - https://jamii.app/Tsh27kTANESCO

#ServiceDelivery
PEMBA: WATU TISA WAFARIKI KWA AJALI YA BOTI

Boti iliyokuwa inatokea Chakechake kuelekea Panza kwa shughuli za mazishi imezama usiku wa kuamkia Januari 5, 2022

> Uokoaji ulisitishwa kwasababu ya giza ambapo maiti 9 ziliopolewa, na Watu 6 waliokolewa

Soma https://jamii.app/PembaAjalii

#JFMatukio
KAZAKHSTAN: SERIKALI YAJIUZULU KUFUATIA MAANDAMANO YA KUPINGA BEI ZA MAFUTA

Rais Kassym-Jomart Tokayev ametangaza Hali ya Dharura kwa wiki mbili katika baadhi ya maeneo

Hatua kadhaa za dharura zimetangazwa ikiwemo marufuku ya mikusanyiko

Soma - https://jamii.app/GovtResigns

#Accountability #JFUwajibikaji
HONG KONG YAPIGA MARUFUKU NDEGE KUTOKA NCHI 8

Miongoni mwa Nchi hizo ni Canada, Marekani na India. Mamlaka zimeweka marufuku hiyo kutokana na hofu ya Wimbi la Tano la #COVID19

Baa, klabu na makumbusho kufungwa ili kudhibiti maambukizi

Soma - https://jamii.app/FlightBanHK

#UVIKO3 #JFAfya #Governance
Wateja wa njia moja watalipia Tsh. 320,960, Tsh. 515,618 na Tsh. 696,670 kwa Mita 30, 70 na 120 ili kuunganishiwa umeme

Kwa njia 3 ni Tsh. 912,014, Tsh. 1,249,385 na Tsh. 1,639,156 kwa Mita 30, 70 na 120 mtawalia. Kwa Watu wa Kijijini ni Tsh. 27,000

Soma https://jamii.app/BeiKuunganisha

#ServiceDelivery
MDAU: NJIA ZA KUTATUA TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA NCHINI

Kuanzisha Programu za Ujuzi, Elimu na Mafunzo: Serikali inatakiwa kuanzisha Mitaala Maalum itakayoweza kutumika kuanzia ngazi ya Msingi mpaka Vyuo

Kuboresha Sayansi na Teknolojia: Vijana wafunzwe ujuzi wa kubuni, kutengeneza na kutumia vifaa au programu zenye kulenga kutatua kero za kijamii

Soma - https://jamii.app/TatizoAjiraSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
JE, WAIFAHAMU NJIA YA KUZIKA YA AQUAMATION?

#Aquamation ni namna ya uzikaji ambayo imekuwepo tangu miaka ya 1880. Njia hii huyeyusha Maiti na kufanya iwe Majivu kabisa tofauti na njia ya kuchoma

Ndivyo namna Desmond Tutu alivyochagua kuzikwa

Soma - https://jamii.app/Aquamation

#JFMaarifa
SUDAN: Utawala wa Kijeshi umeonywa kutofanya uamuzi wa upande mmoja wa uteuzi wa Waziri Mkuu mpya

Marekani, Uingereza, Norway na Umoja wa Ulaya zimesema hazitamuunga mkono Waziri Mkuu atakayeteuliwa iwapo wadau wa kiraia hawatahusishwa

Soma - https://jamii.app/UteuziWaziriSudan

#Democracy
UFARANSA YARIPOTI AINA MPYA YA #COVID19, WAKIITA 'IHU'

Watu 12 wamekutwa na kirusi hicho kiitwacho B.1.640.2 au IHU

> Shirika la Afya Duniani (WHO) likithibitisha uwepo wa kirusi hicho kitaweza kuitwa 'Pi' ndio herufi inayoifuata #Omicron

Soma https://jamii.app/UfaransaIHU

#UVIKO3 #JFAfya
MAREKANI: Mshauri wa Masuala ya Kitabibu wa Ikulu, Dkt. Anthony Fauci amesema tafiti kuhusu Watoto wa miezi 6 hadi miaka 5 kupatiwa Chanjo ya #COVID19 zinaendelea na ndani ya kipindi cha nusu Mwaka majibu yatakuwa yameshatoka

Soma - https://jamii.app/FauciVaccines

#UVIKO3 #JFAfya
RIPOTI: Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabiliana na Dharura linasema zaidi ya watu Milioni 6.4 katika maeneo kame ya Mashariki na Kusini mwa Ethiopia watahitaji msaada wa chakula

Vita ya Serikali na TPLF vimeacha mamilioni wakihitaji misaada

Soma - https://jamii.app/WatuMsaadaETH
NIGERIA: MAGENGE YA UHALIFU KUTAMBULIKA KAMA MAKUNDI YA KIGAIDI

Serikali imefanya hivyo kuimarisha Usalama kufuatia ongezeko la ghasia

Magenge hayo yamekuwa yakifanya mashambulizi, kuvamia vijiji, kuiba mifugo na kuteka nyara watu ili kulipwa fedha

Soma - https://jamii.app/UhalifuNigeria

#Governance