JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NACHINGWEA: Wananchi waliouziwa Ardhi kuanzia Juni 2020 mpaka Desemba 2021 wametakiwa kurudisha Ardhi kwani mauziano hayo ni batili

DC Hashim Komba amesema Serikali ilisitisha ugawaji wa Ardhi tangu Juni 2020 mpaka pale itakapotoa mwongozo rasmi

Soma - https://jamii.app/ViwanjaNachingwea
#COVID19: Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema athari inayotokana na Kirusi cha Corona aina ya Omicron bado ipo juu. Maambukizi ulimwenguni yameongezeka kwa 11% wiki iliyopita

Ushahidi waonesha #Omicron ina ukuaji wa haraka zaidi

Soma - https://jamii.app/WHOOmicron

#UVIKO3
SOMALIA: JUMUIYA ZA KIMATAIFA ZAINGILIA MVUTANO WA RAIS NA WAZIRI MKUU

Rais Mohamed Abdullahi alimsimamisha kazi Waziri Mkuu, Mohammed Roble kufuatia tuhuma za ufisadi, kitendo ambacho Waziri Roble amesema ni jaribio la Mapinduzi

Soma - https://jamii.app/SiasaSomalia
Marekani inapanga kuchukua hatua mpya ili kushinikiza Utawala wa Kijeshi Nchini #Myanmar kurudisha Serikali ya Kiraia kutokana na kukandamizwa kwa Wapinzani

UN imetahadharisha juu ya ongezeko la visa vya ukiukwaji wa Haki za Binadamu

Soma - https://jamii.app/USvsMyanmar

#Democracy
DARFUR, SUDAN: GHALA LA WFP LAVAMIWA NA WATU WENYE SILAHA

Ghala la Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilikuwa na Tani 1,900 za Chakula cha Msaada

Darfur imeshuhudia ongezeko la mapigano tangu Oktoba kutokana na migogoro ya ardhi na maji

Soma - https://jamii.app/WFPLooted
ZANZIBAR: Rais Hussein Mwinyi amemteua Charles Martin Hilary kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano - Ikulu

Yusuph Nassor ameteuliwa kuwa
Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Viwango (ZBS) na Dkt. Idrissa Hija kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi

Soma - https://jamii.app/UteuziZnz3
ASHRAF GHANI: SIKUWA NA NAMNA NYINGINE ZAIDI YA KUKIMBIA AFGHANISTAN

Rais wa zamani wa #Afghanistan amekanusha kuwepo mazungumzo ya kuwaachia #Taliban Madaraka kwa amani, kama walivyodai Maafisa wa zamani wa Afghanistan na Marekani

Soma - https://jamii.app/AshrafGhaniFlee
#JFLeo
AFRIKA KUSINI YALEGEZA KANUNI ZA KUDHIBITI COVID-19

Serikali inaamini Nchi imepita kilele cha Wimbi la Nne

Marufuku ya watu kuwa nje kuanzia saa sita usiku imeondolewa. Mikusanyiko ya ndani haitakiwi kuzidi watu 1,000 na nje watu 2,000

Soma - https://jamii.app/OmicronSA

#UVIKO3
👍1
CHINA: WACHEZAJI MPIRA WAPIGWA MARUFUKU KUCHORA TATTOO

Mamlaka ya Michezo Nchini #China imepiga marufuku Wachezaji wa Timu ya Taifa na Wanamichezo wengine kujichora #Tattoo na kuamuru walionazo waziondoe ili kuwa mfano mzuri kwa Jamii

Soma - https://jamii.app/TattooBanChina
#Sports
UTEUZI: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kipindi kingine cha miaka 6

Patience Kilanga Ntwina ateuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

Soma - https://jamii.app/RaisUteuzi4
Baadhi ya aliyozungumza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake kwa Taifa kuelekea mwaka mpya 2022

Zaidi, soma - https://jamii.app/Hotuba2022

#JFLeo
RAIS SAMIA: KIRUSI CHA OMICRON KIMEINGIA NCHINI

Akihutubia Taifa, amesema Kirusi hicho kinaenea kwa kasi kubwa na tayari kimeingia hapa Nchini. Amewasisitiza wananchi kuchukua tahadhari

Ametoa wito kwa watu kupata chanjo akisema, "Natambua chanjo haizuii mtu kupata maambukizi ila inapunguza makali ya ugonjwa huo. Niwahimize wananchi kuchanja, chanjo zipo"

#UVIKO3
- Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watendaji wa JamiiForums tunakutakia Mapokezi mema ya Mwaka mpya wa 2022

- Tunathamini mchango wako na thamani uliyonayo kwetu huku tukiamini utaendelea kuwa nasi ndani ya Mwaka 2022

#JamiiForums #HappyNewYear2022
INDIA: Watu 12 wamefariki dunia na 13 kujeruhiwa kufuatia mkanyagano katika jumba la kidini la Mata Vaishno Devi huko Kashmir

Taarifa za awali zinasema mkanyagano ulitokana na idadi kubwa ya watu kuja kwa kasi kuelekea mwaka mpya

Soma - https://jamii.app/IndiaStampade

#JFLeo
MALI: SERIKALI YAPENDEKEZA UCHAGUZI KUCHELEWESHWA

Serikali ya Mpito imependekeza Mchakato wa kurejea ktk Utawala wa Kidemokrasia kufuatia Mapinduzi ya mwaka 2020 kusogezwa mbele kwa miaka 5

Awali, Serikali ilikubali kufanya Uchaguzi Februari 2022

Soma - https://jamii.app/MaliElectionDelay

#Democracy #Governance
ETHIOPIA, MALI NA GUINEA ZAONDOLEWA AGOA

Serikali ya Marekani imeanza kutekeleza agizo la Rais Joe Biden la kuziondoa #Ethiopia, Mali na Guinea kwenye makubaliano ya kibiashara kati ya Taifa hilo na Afrika kutokana na uvunjwaji wa Haki za Binadamu

Soma - https://jamii.app/MaliOutAgoa

#Diplomacy #JFDiplomasia
DUBAI, UAE: WASIOPATA CHANJO KUTORUHUSIWA KUSAFIRI NJE

Mamlaka za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zapiga marufuku Raia wasiopata Chanjo ya #COVID19 kusafiri nje kuanzia Januari 10

Waliochanjwa wanatakiwa kupata 'Booster' kuweza kusafiri

Soma - https://jamii.app/UAETravelBan

#UVIKO3 #Governance #JFAfya
PROF. ASSAD: SIASA NI TATIZO KUBWA, HATUWEKI MALENGO YANAYOPIMIKA

Aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad amesema, "Kwasababu ya Siasa hatujui malengo ni yapi na yanapimwa vipi. Siasa kwa sehemu kubwa inatuharibia"

Soma - https://jamii.app/AssadSiasa

#JFSiasa #Accountability