JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SUDAN: WAZIRI MKUU AJIUZULU BAADA YA MAANDAMANO KUPAMBA MOTO

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok amejiuzulu baada ya maandamano ya wanaotaka demokrasia kupamba moto nchini humo

Hamdok ambaye aliwahi kuwa Afisa wa Umoja wa Mataifa(UN) alisaini makubaliano na Jeshi mwezi Novemba ambapo wanademokrasia walipinga hatua hiyo na kuanzisha maandamano

Jeshi lilipindua Serikali ya muda mrefu ya Rais Omar al-Bashir, April 2019 na nchi iliongozwa kijeshi tangu wakati huo

#Accountability #Democracy
ISRAEL YATANGAZA KISA CHA KWANZA CHA 'FLURONA'

Mwanamke Mjamzito ambaye hajapata Chanjo ya Corona amekutwa na mchanganyiko wa Mafua (Flu) na #CoronaVirus

Mchanganyiko huo umetajwa kuwa hatari kwani Maradhi yote yanaathiri Mfumo wa Upumuaji

Soma https://jamii.app/IsraelFlurona

#UVIKO3 #JFAfya
MOROGORO: Upepo mkali uliovuma Kijiji cha Kalengakelo umeezua paa za Nyumba 21, Vyumba 3 vya Madarasa na Ofisi moja

DC Hanji Godigodi ameagiza Wataalamu kufanya tathmini ya gharama ya kurudisha miundombinu ya Madarasa na Ofisi

Soma https://jamii.app/UpepoMorogoro
NDUGAI: TUTENGENEZE MAKUMBUSHO YA BUNGE

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema ni muhimu kwa Bunge kuwa na makumbusho ili wanaotembelea wajue historia ya Bunge

> Amesema suala la makumbusho ni muhimu hata kwa Taasisi nyingine nchini

Soma https://jamii.app/SpikaNdugai

#Governance
NDUGAI: NAMUOMBA RADHI RAIS NA WANANCHI WOTE

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuomba radhi Rais Samia Suluhu na Wananchi wote kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yake

> Amesema wana CCM lengo lao ni moja na hawawezi kutofautiana

Soma https://jamii.app/SpikaNdugai

#Accountability
NDUGAI: NIMEUMIA KUOENEKANA NAPINGA MKOPO WA SERIKALI WA TSH. TRILIONI 1.3

Spika Job Ndugai amesema kauli aliyoitoa Desemba 26, 2021 imenukuliwa vibaya, video iliyosambazwa haikuwa na ujumbe aliokusudia

> Amesema Serikali inafanya vizuri

Soma https://jamii.app/SpikaNdugai

#Accountability #JFUwajibikaji
HONG KONG: UHURU WA HABARI WAENDELEA KUZOROTA. TOVUTI NYINGINE YAFUNGWA

Citizen News itafungwa kuanzia Januari 04 kutokana na mazingira ya Vyombo vya Habari kuzorota

Sheria mpya zilizowekwa na China zataka kuzuia #UhuruWaKujieleza

Soma - https://jamii.app/CitizenNewsHK

#PressFreedom #UhuruWaHabari
ZANZIBAR: Rais Hussein Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji (ZBC), Dkt. Saleh Yussuf Mnemo leo Januari 03, 2022

Dkt. Mnemo aliteuliwa kuhudumu nafasi hiyo Mwezi Mei 2021

Soma - https://jamii.app/UtenguziZBC

#Governance
LAMU, KENYA: Watu sita wameuawa na nyumba kuchomwa moto na Wanamgambo wanaoshukiwa kuwa ni Al Shabaab

Wapiganaji wa Al Shabaab wamefanya mashambulizi kadhaa Nchini humo baada ya Wanajeshi kupelekwa Somalia mwaka 2011

Soma - https://jamii.app/6DeadLamu
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUJENGA NIDHAMU BINAFSI ILI KUFIKIA MALENGO

Muda: Jifunze kusema 'Hapana' kwenye matukio yanayopoteza muda wako na wekeza muda mwingi kwenye masuala yanayokuongezea ujuzi

Fedha: Nidhamu bora ya fedha huchochea kutengeneza uwezekano wa ndoto zako. Wekeza katika maeneo yanayoendana na ndoto zako

Soma Makala - https://jamii.app/NidhamuSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
TANZIA: MZEE KAMBAULAYA AFARIKI DUNIA

Msanii maarufu na Mwanahabari mkongwe, Barnabas Maro maarufu kama Mzee Kambaulaya au Baba Bishanga amefariki dunia Januari 4, 2022 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akipatiwa matibabu

Soma https://jamii.app/Kambaulaya
IRAN YATAKA TRUMP AWAJIBISHWE KWA MAUAJI YA SOLEIMANI

Rais Ebrahim Raisi ataka kuundwe Mahakama ambayo Donald Trump, Mike Pompeo na wengine watashtakiwa kwa mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani yaliyotokea miaka 2 iliyopita, au Iran italipiza kisasi

Soma https://jamii.app/TrumpSoleimani

#JFUwajibikaji #Accountability
ISRAEL YAWA NCHI YA KWANZA KUTOA CHANJO YA NNE YA #COVID19

Ongezeko la maambukizi ya #Omicron limefanya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wapewe 'booster' ya pili

Wengine wanaopewa kipaumbele ni wenye Magonjwa Sugu na Wahudumu wa Afya

Soma https://jamii.app/SecondBoosterDose

#UVIKO3 #JFAfya
KENYA: Kiongozi wa ODM, Raila Odinga amehoji chanzo cha Mamilioni ya Fedha ambayo amesema Naibu Rais, William Ruto anamwaga kwenye Kampeni zake

Awataka Wakenya kutomchagua Ruto kuongoza Taifa hilo akisema Uongozi wake utatawaliwa na Ufisadi

Soma https://jamii.app/RailaRutoKE

#Accountability
MDAU: NAMNA SERIKALI INAVYOWEZA KUWASAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI

1. Serikali na Sekta Binafsi zinapaswa kuwaamini Vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu

2. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine, kwani hii itasaidia kupanua soko la nje

3. Kuwepo uwazi katika masuala ya Ajira kuanzia Serikali mpaka Mashirika Binafsi. Ukabila, Rushwa na Udini viepukwe

Soma - https://jamii.app/WahitimuSerikaliSOC

#StoriesOfChange #JFMdau
UTEUZI: Rais Samia amteua Dkt. Baghayo Saqware kuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (TIRA)

Charles Itembe ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Eneo Maalum la Mauzo ya Nje (EPZA), na Ernest Mchanga Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha

Soma - https://jamii.app/Uteuzi3Rais

#Governance
MSUMBIJI: Rais Filipe Nyusi na mkewe Isaura Nyusi wamekutwa na #COVID19 na wamelazimika kujitenga

> Nchi hiyo imethibitisha kuwa na watu 193,000 wanaougua COVID-19, na vifo 2,031

Soma https://jamii.app/FilipeNyusi

#UVIKO3 #JFAfya
SUDAN: WANAHARAKATI WAITISHA MAANDAMANO ZAIDI

Wanaoongoza Kampeni dhidi ya Utawala wa Kijeshi wamesema Waandamanaji watakuwa wakielekea Ikulu hadi ushindi utakapopatikana

Idadi ya waliopoteza maisha tangu Mapinduzi kufanyika imefikia 56

Soma - https://jamii.app/ProtestsSdn

#Democracy
UTAJIRI WA KAMPUNI YA APPLE WAZIDI GDP YA AFRIKA

Kampuni ya Apple imefikisha thamani ya Dola trilioni 3 (takriban Tsh. Trilioni 6,920.88) katika Soko la Hisa

Pato la Ndani la Afrika (GDP) ni Dola Trilioni 2.6 sawa na Tsh. Trilioni 5,998.1

Soma - https://jamii.app/AppleUtajiri

#JFTech
MWIGULU: DENI NI HIMILIVU, TUTAENDELEA KUKOPA

Asema Mkopo sio Msaada na hutolewa kwa mwenye chanzo cha kulipa

Pia, amesema sio uungwana kusema Rais anakopa akisisitiza Marais hawakopi bali ni Serikali akisema "Hilo si jambo la Familia, ni la Nchi"

Soma https://jamii.app/MwiguluDeni

#Governance
👍1