JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
HOJA: JE, UMEWAHI KUFANYIWA 'BULLYING' KWENYE MAISHA YAKO?

'Bullying' ni aina ya Unyanyasaji unaofanywa hasa na Watoto na unaweza kujidhihirisha kwa kusukumwa ovyo, kupigwa, kuitwa majina yasiyofaa, matusi au vitisho. Hali hii huweza kumuathiri Mtoto Kisaikolojia na Kihisia

Je, umewahi kufanyiwa 'Bullying' kutokana na maumbile au mwonekano wako? Uliathirikia kwa namna gani na umewezaje kupambana na athari hizo?

Mjadala - https://jamii.app/AthariBullying

#Bullying
DKT. GWAJIMA: VIONGOZI WASIOCHANJA WAACHIE NGAZI

Waziri wa Afya atoa wito huo akisema Viongozi hao hawatetei msimamo wa Serikali kwani hata Rais amechanja

Asema hawawezi kuwa na hamasa ya kusimamia kampeni ya uchanjaji dhidi ya #COVID19

Soma - https://jamii.app/ViongoziChanjo

#UVIKO3
MAREKANI: TRUMP AIOMBA MAHAKAMA KUZUIA BUNGE KUPATA TAARIFA ZAKE

Rais wa zamani wa Marekani ameiomba Mahakama ya Rufaa kuzuia Wabunge wanaochunguza ghasia za Januari 6 katika jengo la Bunge kupata taarifa za mazungumzo yake ya wakati huo

Soma - https://jamii.app/TrumpDataBunge
#JFLeo
Desemba 1 kila Mwaka ni Siku ya UKIMWI Duniani ambao uligundulika kwa mara ya kwanza Mwaka 1988. Takwimu mbalimbali zinaonesha Vijana ndio kundi linaloathirika zaidi

Kaulimbiu ya Mwaka 2021 inasema, "Komesha ukosefu wa usawa. Komesha UKIMWI. Komesha Magonjwa ya milipuko"

Umoja wa Mataifa unalenga kukomesha janga hili ifikapo 2030

#WorldAIDSDay2021 #JamiiForums
ZIMBABWE: WASAFIRI WA KIMATAIFA WATAKIWA KUKAA KARANTINI

Wasafiri wanaoingia Nchini humo watatakiwa kupimwa #COVID19 na kukaa Karantini kwa gharama zao

Serikali imeweka amri ya Raia kutokuwa nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa 12 asubuhi

Soma - https://jamii.app/ZimbabweCurfew

#UVIKO3
USIWE SEHEMU YA UPOTOSHAJI KUHUSU COVID-19 NA CHANJO

Kufuatia usambaaji wa taarifa zisizo sahihi, Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri kila mmoja kuepuka kuwa sehemu ya upotoshaji

Taarifa za kupotosha zinaweza kueneza wasiwasi na hofu

Soma https://jamii.app/ChanjoUpotoshaji

#UVIKO3
UZALISHAJI WA POMBE YA BANANA WASITISHWA KWA KUTOKIDHI VIWANGO VYA UBORA

Uchunguzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) umebaini haifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuongezewa kiwango kikubwa cha kemikali ya Asetic Acid

Soma - https://jamii.app/BananaMarufuku

#JFLeo
MICHEZO: Timu ya #Tanzania ya Watu wenye Ulemavu, Tembo Warriors imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye Ulemavu (CANAF 2021)

Imepata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Dunia yatakayofanyika Uturuki 2022

Soma - https://jamii.app/KombeDunia2022

#JFSports
Rushwa ya Ngono inapotolewa Ofisini au sehemu za kutolea huduma husababisha madhara ikiwemo kukwamisha upatikanaji wa Haki, mtendewa kukosa huduma muhimu, kuongeza idadi ya wenye Magonjwa ya Zinaa

Vilevile Rushwa ya Ngono inadhoofisha nguvu kazi ya Wanawake, kuwakosesha Wanawake na Wasichana kipato binafsi, na kuzorotesha Maendeleo na Uchumi wa Nchi

Soma - https://jamii.app/RushwaMapenzi
#16DaysOfActivism
MSUMBIJI: VIJANA ZAIDI YA 100 WATEKWA NA WAPIGANAJI

Watu wenye silaha wamewateka nyara zaidi ya vijana katika Kijiji cha Naulala kilichopo Mkoa wa Niassa na kuchoma makazi

Taifa hilo limekuwa likikabiliana na waasi tangu Oktoba mwaka 2017

Soma - https://jamii.app/Msumbiji100
#JFLeo
Ili kuzuia Ukatili wa Kingono kwa Watoto, Mzazi/Mlezi hakikisha unadhibiti maudhui anayotazama kwenye Televisheni

Mshiriki wa 'Stories Of Change' anasema anasema mzuie Mtoto kuhudhuria Ngoma za mikesha (vigodoro) kwakuwa zinachochea vitendo vya Ngono. Tambua mazingira anayocheza Mtoto pamoja na anaocheza nao kama ni salama kwake

Ikiwezekana Mtoto asilale na wageni waliomzidi umri mkubwa Chumba kimoja

Soma - https://jamii.app/UkatiliKingonoSOC

#StoriesOfChange
Baadhi ya Wachangiaji ndani ya JamiiForums wamezua Mjadala kuhusu 'Homeworks' nyingi wanazopewa Watoto toka Shuleni hasa kipindi cha likizo

Baadhi wanaona ni jambo la manufaa kwani humpa nafasi Mzazi kushiriki katika maendeleo ya Mtoto huku wengine wakiona ni kumtesa Mtoto kipindi anachotakiwa kupumzika

Ikiwa wewe ni Mzazi, Mlezi au Mwalimu ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika Desemba 2, 2021 kupitia Clubhouse

#JamiiForums #Malezi
Takwimu zilizokusanywa na UNITAID na WHO kwa pamoja zinaonesha kati ya Mwaka 2015 na 2020, idadi ya Nchi zilizo na Sera za kujipima VVU imeongezeka kutoka Mataifa 6 hadi 88 - na Mataifa mengine 31 yanaandaa Sera hizo

Kujipima VVU kumesaidia kufikia idadi ya Watu wengi wakiwemo Wanaume na Vijana ambao wana uwezekano mdogo wa kufika Vituo vya Afya na walikuwa na viwango vya chini vya upimaji.

#WorldAIDSDay #JamiiForums
MDAU: MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUEPUKA TALAKA

Kutopuuza shida na haja za Mwenza wako hata kama ni mambo madogo madogo

Anashauri kuepuka mazingira yote yanayoweza kufanya utumbukie katika vishawishi vya kuvunja uaminifu

Anasisitiza kuepuka kuanzisha mijadala itakayoleta mabishano yasiyo ya lazima

Soma Makala yake - https://jamii.app/NdoaTalaka

#StoriesOfChange
WHATSAPP NA iMESSAGE ZABAINIKA KUTOA TAARIFA NYINGI ZA WATUMIAJI

Kwa maombi ya kawaida, #WhatsApp huwatumia FBI taarifa kila baada ya dakika 15 hata kwa watumiaji wa iPhone

Signal na Telegram zimetajwa kutotoa taarifa nyingi

Soma - https://jamii.app/TaarifaWatumiaji

#DataProtection
MANYARA: ELIMU YA COVID-19 KUTOLEWA NYUMBA KWA NYUMBA

Mratibu wa Chanjo ya #CoronaVirus Mkoani humo, Suleiman Manoza amesema mwamko wa Chanjo ni mdogo

Wameiomba Wizara ya Afya kuwapatia Chanjo ya #Janssen ambayo inatolewa mara moja

Soma - https://jamii.app/DoorToDoor

#UVIKO3
Baadhi ya Wachangiaji ndani ya JamiiForums wamezua Mjadala kuhusu 'Homeworks' nyingi wanazopewa Watoto toka Shuleni hasa kipindi cha likizo

Baadhi wanaona ni jambo la manufaa kwani humpa nafasi Mzazi kushiriki katika maendeleo ya Mtoto huku wengine wakiona ni kumtesa Mtoto kipindi anachotakiwa kupumzika

Ikiwa wewe ni Mzazi, Mlezi au Mwalimu ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika Desemba 2, 2021 kupitia Clubhouse

#JamiiForums #Malezi
Serikali imesema tafiti zinaonesha Maambukizi mapya ya VVU yanawakabili zaidi Vijana wenye miaka 15-24, huku 80% wakiwa wa Kike

Mikoa yenye maambukizi makubwa na juu ya kiwango cha kitaifa ni Njombe, Iringa, Mbeya, Kagera na Geita

Soma https://jamii.app/VijanaVVUTZ

#WorldAidsDay2021
COVID-19: KOREA KUSINI YAWATAKA WASAFIRI WOTE KUKAA KARANTINI

Taifa hilo lasema Wasafiri wote wakiwemo waliopata Chanjo kamili watatakiwa kukaa Karantini kwa siku 10

Safari za ndege kutoka Nchi 8 za Afrika ikiwemo Afrika Kusini kudhibitiwa

Soma https://jamii.app/ChanjoKoreaKusini

#UVIKO3