JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Ukatili unajitokeza katika sura mbalimbali kama vile vipigo, Ukeketaji, Ubakaji, Mauaji ya Wanawake na Watoto wa Kike, kurithi Wajane, Udhalilishaji wa Wanawake Mitandaoni au kwenye Siasa, na rushwa ya ngono

Ukatili una athari mbaya kwa Wanawake na Watoto wa Kike, kwani huathiri Afya zao Kimwili na Kisaikolojia na hupelekea kudidimiza Maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

#JamiiForums #GenderBasedViolence #16DaysofActivism2021
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
RWANDA: WAZEE WAANZA KUPATIWA DOZI YA TATU YA CHANJO YA CORONA

Walio na umri wa zaidi ya miaka 50 na wenye maradhi wataanza kupokea dozi kuanzia leo, Novemba 30

Watumishi wa Afya wametajwa katika kundi la kupokea dozi hiyo dhidi ya #COVID19

Soma https://jamii.app/WazeeChanjo
#UVIKO3
TABORA: Wauguzi 2 wa Hospitali ya Kaliua wamesimamishwa kazi kwa vitendo vya utovu wa nidhamu

Mmoja anatuhumiwa kufanya mapenzi wodini na Daktari aliye katika mafunzo kwa vitendo huku mwingine akituhumiwa kuwa kinara katika utoaji wa Mimba

Soma - https://jamii.app/NursesFiredSex
#JFLeo
CHANJO ZA COVID-19 ZIMEPITIA HATUA ZA KIUSALAMA

Wataalamu wa Afya wa Chuo Kikuu cha Johns Hopkins wanasema utengenezwaji wa haraka haumaanishi hatua zilirukwa

Teknolojia zimekuwa zikiandaliwa kupambana na milipuko ya Virusi vya kuambukiza

Soma https://jamii.app/ChanjoUsalama

#UVIKO3
CHINA YAIAHIDI AFRIKA DOZI BILIONI 1 ZA CHANJO

Rais Xi Jinping ameahidi kuipa Afrika Dozi Bilioni 1 za Chanjo dhidi ya #COVID19

Katika dozi hizo, Milioni 600 zitatoka #China moja kwa moja na Milioni 400 zitatoka kwa vyanzo vingine

Soma - https://jamii.app/ChinaChanjo

#UVIKO3
Mradi wa Uzalishaji wa Sukari Mbigiri ambao unamilikiwa na Kampuni tanzu ya Mkulazi Wilayani Kilosa ulilenga kuzalisha Sukari tani 50,000 kwa Mwaka

CAG alibaini Kampuni ya Mkulazi kushindwa kusimika mtambo wa kuchakata Sukari kwa wakati kinyume na mkataba wa Mwaka 2018

Pia, Kampuni haikuweza kusimamia Utendaji wa Wakulima wanaouzunguka Mradi kwa kuwapatia ushauri wa Kitaalamu

Soma - https://jamii.app/CAGSukariMbigiri
#JFUwajibikaji
MALEZI: UDHALILISHAJI WA MTOTO KWA NJIA YA MANENO

Udhalilishaji kwa njia ya maneno unatokea pale ambapo Mzazi/Mlezi au Mtu aliye karibu na Mtoto anapotumia maneno yenye kumuumiza Mtoto Kihisia

Baadhi ya maneno ni; Kumkemea au kumkaripia mbele ya hadhara ya Watu au Familia/Ndugu. Kumuita Mtoto majina mabaya (Matusi) na majina mengine ikiwemo majina ya Wanyama

Soma - https://jamii.app/AbuseWordsChild
#Malezi #ChildViolence
Novemba 29, 2021, Taasisi ya WAJIBU ilizindua kitabu kiitwacho "Principles of Public Sector Auditing - The Case of SAI Tanzania" Jijini Dar es Salaam
-
Kitabu hicho kilizinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emanuel Tutuba kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba
-
Kitabu hicho kimeandikwa na CAG mstaafu na Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU, CPA. Ludovick Utouh.

#JamiiForums #JFUwajibikaji
Taarifa binafsi ni taarifa zozote zinazohusiana na Mtu na ambazo zinaweza kumtambulisha Mmiliki wa taarifa hizo

Hizi ni taarifa ambazo Mtu anapaswa kuwa makini katika Matumizi yake ili kuepuka uwezekano wa kutumika vibaya

#JamiiForums #PersonalDataProtection
HOJA: JE, UMEWAHI KUFANYIWA 'BULLYING' KWENYE MAISHA YAKO?

'Bullying' ni aina ya Unyanyasaji unaofanywa hasa na Watoto na unaweza kujidhihirisha kwa kusukumwa ovyo, kupigwa, kuitwa majina yasiyofaa, matusi au vitisho. Hali hii huweza kumuathiri Mtoto Kisaikolojia na Kihisia

Je, umewahi kufanyiwa 'Bullying' kutokana na maumbile au mwonekano wako? Uliathirikia kwa namna gani na umewezaje kupambana na athari hizo?

Mjadala - https://jamii.app/AthariBullying

#Bullying
DKT. GWAJIMA: VIONGOZI WASIOCHANJA WAACHIE NGAZI

Waziri wa Afya atoa wito huo akisema Viongozi hao hawatetei msimamo wa Serikali kwani hata Rais amechanja

Asema hawawezi kuwa na hamasa ya kusimamia kampeni ya uchanjaji dhidi ya #COVID19

Soma - https://jamii.app/ViongoziChanjo

#UVIKO3
MAREKANI: TRUMP AIOMBA MAHAKAMA KUZUIA BUNGE KUPATA TAARIFA ZAKE

Rais wa zamani wa Marekani ameiomba Mahakama ya Rufaa kuzuia Wabunge wanaochunguza ghasia za Januari 6 katika jengo la Bunge kupata taarifa za mazungumzo yake ya wakati huo

Soma - https://jamii.app/TrumpDataBunge
#JFLeo
Desemba 1 kila Mwaka ni Siku ya UKIMWI Duniani ambao uligundulika kwa mara ya kwanza Mwaka 1988. Takwimu mbalimbali zinaonesha Vijana ndio kundi linaloathirika zaidi

Kaulimbiu ya Mwaka 2021 inasema, "Komesha ukosefu wa usawa. Komesha UKIMWI. Komesha Magonjwa ya milipuko"

Umoja wa Mataifa unalenga kukomesha janga hili ifikapo 2030

#WorldAIDSDay2021 #JamiiForums
ZIMBABWE: WASAFIRI WA KIMATAIFA WATAKIWA KUKAA KARANTINI

Wasafiri wanaoingia Nchini humo watatakiwa kupimwa #COVID19 na kukaa Karantini kwa gharama zao

Serikali imeweka amri ya Raia kutokuwa nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa 12 asubuhi

Soma - https://jamii.app/ZimbabweCurfew

#UVIKO3
USIWE SEHEMU YA UPOTOSHAJI KUHUSU COVID-19 NA CHANJO

Kufuatia usambaaji wa taarifa zisizo sahihi, Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri kila mmoja kuepuka kuwa sehemu ya upotoshaji

Taarifa za kupotosha zinaweza kueneza wasiwasi na hofu

Soma https://jamii.app/ChanjoUpotoshaji

#UVIKO3
UZALISHAJI WA POMBE YA BANANA WASITISHWA KWA KUTOKIDHI VIWANGO VYA UBORA

Uchunguzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) umebaini haifai kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuongezewa kiwango kikubwa cha kemikali ya Asetic Acid

Soma - https://jamii.app/BananaMarufuku

#JFLeo
MICHEZO: Timu ya #Tanzania ya Watu wenye Ulemavu, Tembo Warriors imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye Ulemavu (CANAF 2021)

Imepata tiketi ya kushiriki Mashindano ya Dunia yatakayofanyika Uturuki 2022

Soma - https://jamii.app/KombeDunia2022

#JFSports