JamiiForums
βœ”
52.8K subscribers
34.4K photos
2.44K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI YAPIGA MARUFUKU DAWA ZA KUULIA WADUDU KUPULIZWA BUCHANI

Bodi wa Nyama Nchini imesema Dawa hizo ni sumu zinazofanya kazi taratibu ndani ya mwili wa Binadamu na husababisha maradhi ikiwemo Saratani

Wenye Bucha wametakiwa kuzingatia Usafi kuzuia Nzi

Soma - https://jamii.app/BanDawaBuchani
Siku ya Watoto Duniani huadhimishwa tarehe 20 Novemba kila mwaka. Pamoja na kuboresha hali zao za Maisha, Siku hii pia inalenga kuimarisha Haki zao

Watoto na Vijana wamekuwa wakipaza sauti kwenye masuala yanayowagusa, na ni muhimu kwa Viongozi kusikiliza mawazo na matakwa yao

#JamiiForums #WorldChildrensDay
TETESI: MANCHESTER IMEAMUA KUMFUTA KAZI SOLSKJAER

- Inadaiwa kuwa Bodi ya timu ya Man. Utd, imeamua kumfukuza kazi Kocha Ole Gunnar Solskjaer

- Fletcher/Carrick ataiongoza timu hiyo kama Kocha wa muda iwapo Kocha wa kumrithi Solskjaer hatapatikana hivi karibuni

#JFSports
SUDAN: Wanaharakati wanaopinga Mapinduzi Nchini #Sudan wameitisha Maandamano leo Jumapili, wakati idadi ya Watu waliouawa ikifikia 40

Marekani na AU zimelaani ukandamizaji na kuwataka Viongozi wa Sudan kuacha matumizi ya nguvu

Soma - https://jamii.app/ActivistRiotsSudan

#Democracy
RASMI: MAN. UTD YAMFUKUZA SOLSKJAER

Baada ya Mkutano wa dharura wa Bodi ya timu hiyo kukaa jana kutokana na mlolongo wa matokeo mabovu, klabu imeachana na Ole Gunnar Solskjaer

Solskjaer alichaguliwa kuinoa timu hiyo Desemba 2018 baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi

#JFSports
UGANDA: Rais Yoweri Museveni amewataka Waasi wa Kundi la ADF wanaoshutumiwa kuhusika na milipuko ya hivi karibuni kujisalimisha

Amesema Jeshi limewahi kupambana na kuwashinda Waasi hao kabla, hivyo wajitokeze au wote watauawa

Soma - https://jamii.app/MuseveniADF

#JFLeo
SUDAN: Baada ya wiki kadhaa za maandamano, Jeshi limemrejeshea Madaraka Waziri Mkuu wa Nchi hiyo, Abdalla Hamdok na kutangaza kuwaachia huru Wafungwa wote wa kisiasa

Hamdok amesema amekubali ili kuzuia umwagaji damu zaidi Nchini humo

Soma - https://jamii.app/JeshiWaziriMkuu

#JFLeo
KENYA: Serikali imesema kuanzia Desemba 21, anayehitaji huduma za Serikali za ana kwa ana lazima awe amepata chanjo kikamilifu

Baa, migahawa na biashara zinazohudumia watu zaidi ya 50 kwa siku zimeelekezwa kuomba uthibitisho wa Chanjo

Soma - https://jamii.app/ProofVaccineKE

#UVIKO3
AFGHANISTAN: TALIBAN YAPIGA MARUFUKU WANAWAKE KWENYE TAMTHILIA

Serikali imevitaka Vituo vya Televisheni kuacha kurusha Tamthilia au Maigizo yenye Waigizaji wa Kike

Pia, Waandishi wa Habari na Watangazaji wa Kike wametakiwa kuvaa hijabu

Soma - https://jamii.app/WanawakeTaliban

#JFLeo
KUTOKUWA NA CHA KUFICHA, HAIMAANISHI FARAGHA YAKO ISIHESHIMIWE

Watu wengi hudhani β€˜Kukosa cha kuficha’ humaanisha Faragha haina umuhimu. Lakini hata kama chumbani hauna kitu cha kuibwa haina maana uache mlango wazi

Suala la faragha ni zaidi ya kuogopa vitu kuibwa, bali kuwa na staha ya vitu vyako. Hata kama unahisi hauna cha kupoteza Mtandaoni, jali kuhusu faragha yako

Soma - https://jamii.app/DataPrivacy
#DataPrivacy
UN: KILA SEKUNDE 24 MTU 1 HUFARIKI KWA AJALI ZA BARABARANI

Idadi hiyo ni sawa na Watu 3 ndani ya dakika Moja. 90% ya vifo vya Barabarani hutokea Nchi za kipato cha chini na kati

UN imetoa wito wa umuhimu wa kupunguza mwendokasi ili kuzuia ajali

Soma - https://jamii.app/AjaliVifo
KESI YA MBOWE: Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetupilia mbali Hoja 3 zilizotolewa na Utetezi

Mawakili Upande wa Utetezi walipinga kitabu cha kumbukumbu za mahabusu cha Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kupokelewa kama kielelezo cha ushahidi Upande wa Mashtaka

Soma - https://jamii.app/JajiPingamizi3

#JFLeo
GEITA: AHUKUMIWA MIAKA 3 AU FAINI YA TSH MILIONI 2 KWA KUPOKEA RUSHWA

Aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Maji Wilaya ya Geita, Eng. Rael Buliba alipokea rushwa ya Tsh. Milioni 75 kutoka kwa Mkandarasi ili kuongeza muda wa kusambaza mabomba ya Maji

Soma - https://jamii.app/Milioni2Faini
ZANZIBAR: UNGUJA YATAJWA KUONGOZA KWA UKAHABA NA USHOGA

Waziri Dkt. Saada Salum Mkuya amesema #Unguja ina Wanawake 4,854 na Pemba 700 wanaofanya Biashara ya kuuza miili yao

Wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja #Zanzibar ni 3,300

Soma - https://jamii.app/UshogaUkahaba
MAPUNGUFU KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Ripoti ya CAG ilibaini Mamlaka ya Serikali za Mitaa 152 hazikupokea Tsh. Bilioni 410.4 sawa na 46% ya Fedha za Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2019/20

Hazina na Washirika wa Maendeleo hawakutoa Fedha za Miradi ya Maendeleo kiasi cha Tsh. Bilioni 53.4 sawa na 22% ya Bajeti iliyoidhinishwa

Soma - https://jamii.app/MapungufuMiradi

#JFUwajibikaji
Jamii Forums inatoa nafasi 2 za ajira kwa Wasanifu Grafiki (Graphic Designers)

MAJUKUMU: Kuandaa na kusanifu picha kulingana na mahitaji, Kuandaa na kuhariri picha mjongeo zitakazotumika kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Kwa Maelezo zaidi tembelea - https://jamii.app/GraphicDesignersJF
MDAU: UWAJIBIKAJI NI KICHOCHEO CHA UTAWALA BORA

Anasema Nchi hukumbwa na madhara makubwa kwa kukosa Utawala Bora, ikiwemo kuongezeka vitendo vya unyanyasaji, upendeleo, rushwa, wizi na ubadhirifu wa mali za Umma

Kupitia Shindano la #StoriesOfChange amesisitiza suala la Uwajibikaji wa Viongozi kuhakikisha wanatawala kwa kufuata Misingi ya Haki na Usawa

Soma - https://jamii.app/UwajibikajiViongozi

#Accountability
DAR: RC Amos Makalla ametangaza Jumamosi ya kila mwisho wa Mwezi kutumika kufanya usafi kwa mkakati aliouita β€˜Safisha Pendezesha Dar es Salaam’

Katika mkakati huo baadhi ya nyumba za Watu binafsi, Mashirika na Kampuni zimetakiwa kupakwa rangi

Soma - https://jamii.app/UsafiDar
#JFLeo
HOJA: LIPIA TANGAZO MTANDAONI ILI KUPATA WATEJA WANAOHITAJI BIDHAA YAKO

Mdau wa Jamiiforums.com ameandika kuhusu umuhimu wa kulipia matangazo mtandaoni ambapo hufanya bidhaa yako imfikie Mtu mwenye uhitaji nayo badala ya kumfikia Mtu yeyote

Teknolojia ya Mtandao kama #Facebook kwa matangazo yanayolipiwa huyafanya yawafikie Watu ambao walishawahi kutafuta bidhaa unayoitangaza hivyo utapata Watu wenye uhitaji na kuuza

Soma - https://jamii.app/SponsoredAds
#SponsoredAds
SERIKALI: UKIJENGA KWENYE MAENEO HATARISHI TUTABOMOA

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi ametangaza kuvunja Nyumba zilizo maeneo hatarishi na mabondeni hata kama wamiliki wana Hati

Asema walio maeneo hatarishi mara nyingi hupewa Hati kijanja janja

Soma - https://jamii.app/NyumbaKubomolewa