JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: Polisi Kanda Maalum wanamshikilia Mtu mmoja mwenye miaka 16 ambaye jina lake linahifadhiwa kwa tuhuma za kumlawiti Mtoto wa miaka 4 mpaka kumsababishia Kifo

Tukio hilo limetokea Novemba 10, 2021 maeneo ya Chamazi Mbande, Temeke

Soma - https://jamii.app/UlawitiMtt4
#UkatiliWatoto
STEVEN GERRARD ATANGAZWA KUWA KOCHA WA ASTON VILLA

- Klabu ya Aston Villa ya England imemtangaza Nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard kuwa Kocha wake mpya

- Gerrard aliyekuwa akiinoa Klabu ya Rangers ya Scotland, amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu

#Sports
TANZIA: Rais wa Zamani (mzungu wa mwisho kuiongoza Afrika Kusini), FW de Klerk amefariki dunia nyumbani kwake Cape Town alipokuwa akijiuguza Saratani ya Mesothelioma

> Alikuwa Mkuu wa Afrika Kusini kuanzia Septemba 1989 hadi Mei 1994

Soma https://jamii.app/RaisAfrikaKusini
MWANZA: Mwanafunzi wa Darasa la Nne, Ntogoso Gunya (12) amefariki Dunia baada ya kuliwa na Mamba wakati akioga Kando ya Ziwa Victoria

Tukio hilo limetokea Novemba 10, 2021 saa 11 jioni ambapo juhudi za kuutafuta Mwili zimepata Kichwa pekee

Soma - https://jamii.app/KifoMwnfzMamba
#JFLeo
STARS YACHEZEA 3-0 KWA MKAPA

- #TaifaStars imejikuta katika wakati mgumu baada ya kufungwa goli 3-0 na DR Congo kwenye mchezo wa kufuzu #WC2022

- DR Congo inaongoza Kundi J ikiwa na alama 8. Benin ni ya 2 ikiwa na alama 7 na mchezo 1 mkononi. Stars ni ya 3 ikiwa na alama 7

#JFSports
MSUMBIJI: Rais Filipe Nyusi amewafuta kazi Waziri wa Ulinzi, Jaime Neto na Waziri wa Mambo ya Ndani, Amade Muquidade kwa tuhuma za uzembe na kushindwa kutetea Taifa

> Rais aliyasema hayo katika hotuba yake wakati wa Sherehe za Wanajeshi

Soma https://jamii.app/MawaziriMsumbiji
#JFLeo
MATUMAINI YA TANZANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2022 YAZIMIKA

- #TaifaStars imeshindwa kufuzu baada ya Benin kuifunga Madagascar goli 2-0 na yenyewe kufungwa na DR Congo goli 3-0

- Timu moja itasonga mbele. Michezo ya mwisho ni DR Congo vs Benin na Stars vs Madagascar

#JFSports
Utoaji wa Chanjo ya #COVID19 umekuwa ukihamasishwa kona zote za Dunia huku baadhi ya Nchi zikichukua hatua za kuweka Vikwazo kwa Watu ambao hawajapata Chanjo kurudi Maofisini, kusafiri au kushiriki shughuli za kijamii

Wasiochanja wana sababu mbalimbali ambazo zinawapelekea kusitasita katika kufanya Maamuzi.

Ungana na Jamii Forums katika Mjadala na wasiochanja utakaofanyika Ijumaa, Novemba 12, 2021 kupitia Clubhouse

#JamiiForums #UVIKO3
Kwa mujibu wa CCBRT kutengwa kwa Watu wenye Ulemavu mahali pa kazi, ama kwa Ubaguzi au Mazingira ya Kazi yasiyofikika kunaigharimu #Tanzania Dola milioni 480 (Tsh. 1,104,726,985,383) kila Mwaka - 3.76% ya Pato la Taifa

Kaya zinazoongozwa na Watu wenye Ulemavu hukabiliwa na kiwango kikubwa cha Umasikini

Soma - https://jamii.app/WalemavuKazini
#Disabilities
UHABA WA MAFUTA: Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio amesema meli yenye mafuta isipofika ndani ya siku 15 Tanzania itakuwa na uhaba wa mafuta kwa kuwa mafuta yaliyopo yanatosha kutumika wiki mbili tu

Soma https://jamii.app/Mafuta15
WHO imesema kutokana na kiwango kidogo cha upatikanaji wa Chanjo Afrika, Wagonjwa wa Kisukari wanakabiliwa na tishio kubwa la kufariki kwa #COVID19

Uchunguzi uliofanywa kwa Nchi 13 umeonesha kiwango cha Vifo kwa wenye Kisukari kinazidi 10%

Soma - https://jamii.app/KisukariCoronaAF
#UVIKO3
UINGEREZA: Mwanzilishi wa Mtandao wa #Wikileaks, Julian Assange ambaye amefungwa jela ya Belmearsh tangu 2019 ameruhusiwa kumuoa mpenzi wake Stella Moris akiwa jela

> Uingereza inatambua haki ya wafungwa ya kuomba kufunga ndoa wakiwa jela

Soma https://jamii.app/NdoaAssange
#JFLeo
UPDATE: Waziri wa Nishati, January Makamba asema Mkurugenzi wa TPDC, Dkt. James Mataragio atatakiwa kutoa maelezo baada ya kusema mafuta yaliyopo yanatosha kwa siku 15 tu

Amekanusha uhaba wa mafuta na kusema kauli ya uhakika ni ya Serikali

Soma - https://jamii.app/UhabaMafuta

#JFLeo
MDAU: DUNIA YA SASA NA WAZAZI KUKOSA MUDA WA KULEA WATOTO WAO

Mshiriki wa Shindano la 'Stories of Change' anasema kutokana na kuendelea kwa Dunia Ulezi wa Watoto umekuwa mgumu sana kusimamiwa na Wazazi

Jambo hili limepelekea Watoto wengi kukosa Maadili mema kwasababu Wadada wengi wa kazi za Nyumbani sio walezi wazuri. Watoto huiga tabia na mienendo ya Wadada hawa kwasababu ndio hukaa nao muda mrefu.

Msome - https://jamii.app/UtandawaziMalezi
#Malezi
HOJA: Mshiriki wa #StoriesOfChange amesema ndoa ni muungano wa mume na mke hivyo jukumu la kutunza ndoa ni la wote

Mdau amekosoa sherehe za 'Kitchen Party' ambazo humuandaa mwanamke kwa ndoa huku mwanaume akiwa hana sherehe inayomuandaa na maisha hayo

Je, kuna mafunzo gani anayopatiwa Mwanaume kabla ya kuingia kwenye ndoa?

Soma https://jamii.app/MfumoDumeNdoa
Ripoti ya Uwajibikaji kutoka WAJIBU inasema Masoko ya Chakula Nchini yamekuwa ktk hali ya uchakavu na uchafu hivyo kuhatarisha #Afya za Watumiaji wa huduma za Masoko hayo

Halmashauri 8 zilishindwa kutenga 15% ya kiasi cha Fedha kinachokusanywa kama Mapato ktk Masoko ili kugharamia Usafi wa Masoko hayo

Soma - https://jamii.app/UchafuMasoko
#JFUwajibikaji
MFAHAMISHE DAKTARI KUHUSU 'ALLERGY' KABLA YA KUPATA CHANJO

WHO inashauri wenye historia ya mzio wa chanjo (Allergic reaction) kuwaeleza Wataalamu kabla ya kupata Chanjo ya #COVID19

Hii itasaidia kukupa mwongozo sahihi kabla ya kuchanjwa

Soma - https://jamii.app/ChanjoMzio

#UVIKO3
DAR: GUGAI NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Aliyekuwa Mhasibu wa TAKUKURU, Godfrey Gugai na wenzake wawili wameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kushindwa kuthibitisha Mashtaka yanayowakabili

Walikuwa wanakabiliwa na makosa 40

Soma https://jamii.app/GugaiWenzake
#JFLeo
KIGOMA: MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMPIGA HADI KIFO MTOTO ALIYEKATAA KUOLEWA

Mbaru Juakali (17) amepigwa na fimbo sehemu mbalimbali mwilini akilazimishwa kuolewa kwa mahari ya Ng'ombe 13

Baba mzazi na ndugu zake wawili wanashikiliwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/KIgomaNdoa
#JFLeo