JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI ZOEZI LA UPIGAJI KURA BUHIGWE

Jimbo hilo limekuwa wazi baada ya Dkt. Philip Mpango aliyekuwa Mbunge kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais

Pia, Uchaguzi mdogo wa Ubunge unafanyika Muhambwe na Kata 5 zinafanya Uchaguzi wa Madiwani

Soma > https://jamii.app/UchaguziBuhigwe
MASHAMBULIZI GAZA: Idadi ya Vifo vya Raia imeongezeka kufikia 174 tangu kuanza upya kwa mgogoro huo Jumatatu huku kukiwa na Vifo vya Watoto 47 na Wanawake 29. Inaelezwa Watu wanaathiriwa sana na Hewa nzito kutokana na Milipuko

Idadi ya watu walioumia imefikia 1,200. Israel inadaiwa kugoma kusitisha mashambulizi dhidi ya Wapalestina

#GazaUnderAttack
KILIMANJARO: WASTANI WA PIKIPIKI 100 HUIBWA KWA MWAKA

> Madereva huporwa pikipiki kwa kupigwa nondo, kunyongwa au kuumizwa

> Polisi imeshauri madereva, wanapokodiwa na mteja wanayemtilia shaka wampige picha kwa siri na kuiacha kijiweni

Soma https://jamii.app/PikipikiKilimanjaro
MAREKANI: CHAMA CHA WAUGUZI CHAPISHANA NA CDC KUHUSU UMUHIMU WA BARAKOA

- Chama hicho kimesema waliopata chanjo kushauriwa kutovaa barakoa hakutalinda Afya ya Umma na hatua hiyo haipo kisayansi

- Kimesema, huu sio wakati wa kulegeza Masharti

Soma https://jamii.app/WauguziCDC
TUNAKUTAKIA ‘WIKI’ NJEMA NA BARAKA TELE

Tunawatakia mwanzo mwema wa Juma uliojaa furaha na afya njema na kwa wale wenye changamoto katika afya zao, tunawaombea uponyaji wa haraka ili waendelee na majukumu yao

> Tembelea JF Doctors kwa ushauri kuhusu masuala ya #AFYA

#JamiiForums
ILO & WHO: KUFANYA KAZI MUDA MWINGI KUMEPELEKEA VIFO VYA WATU 745,000

> Utafiti wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Shirika la Afya (WHO) unaonesha kufanya kazi kwa muda mwingi kulichangia vifo hivyo kwa mwaka 2016

> 72% ya vifo hivyo ni wanaume

Soma https://jamii.app/KaziVifo
SINGAPORE: AINA MPYA ZA VIRUSI ZINAATHIRI ZAIDI WATOTO

Haijafahamika Watoto wangapi wamepata maambukizi lakini Serikali imesema Kirusi cha #B1617 kinawaathiri kwa kiasi kikubwa

Masomo ya Shule za Msingi na Sekondari kuendelea kutoka nyumbani

Soma https://jamii.app/WatotoVirusi
Rais Samia Suluhu Hassan apokea Ripoti ya Kamati Maalum iliyoundwa kufanya tathmini ya Ugonjwa wa #COVID19 hapa Nchini

> Amepokea Ripoti hiyo Ikulu Dar es Salaam leo Mei 17, 2021 kutoka kwa Prof. Said Aboud ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo

#JamiiForums #JFLeo
SERIKALI YASHAURIWA KURUHUSU CHANJO

> Kamati imeshauri Serikali iendelee na hatua za kuelekea kuruhusu matumizi huru ya Chanjo dhidi ya Corona kwa kutumia Chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa Wananchi kwa kuwa zina ufanisi unaokubalika kisayansi

#JFLeo
SERIKALI YASHAURIWA KUZINGATIA MAZINGIRA YA KITANZANIA KWENYE KUWEKA LOCKDOWN

Kamati ya #COVID19 imeshauri Serikali kuzingatia mazingira ya kitanzania ktk kudhibiti maambukizi

> Pia, kuweka mpango wa kukuza uchumi baada ya kutathmini madhara

Soma https://jamii.app/KamatiCOVID19
SERIKALI YASHAURIWA KUTOA TAKWIMU KUHUSU #COVID19

> Wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na pia Wizara ya Afya imeshauriwa kukamilisha mwongozo mpya wa matibabu

> Tiba asili na tiba mbadala zizingatie misingi ya kisayansi

Soma https://jamii.app/KamatiCOVID19
Serikali imeshauriwa kufanya uhamasishaji na maandalizi ya kupokea, kutunza, kusafirisha na kutoa Chanjo

> Aidha, Wananchi wawe huru kuamua kuchanja au kutochanja

> Kamati pia imeshauri Tanzania ijiunge na #COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa Chanjo

#JFLeo
KAMATI YAPENDEKEZA KUWEPO KIPAUMBELE CHA UTOAJI CHANJO

Kamati iliyoundwa kutathmini #COVID19 imeshauri utoaji Chanjo uanze kwa makundi yafuatayo kwa umuhimu:

Wahudumu ktk Vituo vya Afya na Watumishi walio mstari wa mbele kutoa huduma, Watumishi wa Sekta za Utalii, Hoteli, Mipakani, Viongozi wa Dini na Mahujaji

Wazee na Watu wazima kuanzia miaka 50. Watu wazima wenye maradhi sugu

Watumishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wasafiri wanaokwenda Nje ya Nchi

Soma > https://jamii.app/KamatiCOVID19
KAMATI YA #COVID19: SERIKALI ITENGENEZE KIWANDA CHA CHANJO

> Imesema, COVID-19 imetoa fursa kwa Serikali kuwa na kiwanda cha chanjo

> Pia, imeshauri kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii ili kupanua wigo wa upimaji wa Corona

Soma https://jamii.app/KamatiCOVID19
RAIS SAMIA AWATAKA MAJAJI KUONGOZWA NA UTU

Asema, "Nafsi ikiwaelekeza kwenda kuchukua fedha na kunyima Haki ujue umeshatetereka"

Amesema wakati mwingine kesi huchelewa kwasababu ya upelelezi na kuagiza Vyombo husika kuharakisha mchakato huo

Soma https://jamii.app/UapishoMajaji
MABADILIKO POLISI: MAMBOSASA AHAMISHIWA DODOMA, WAMBURA AREJESHWA DAR

- SACP Lazaro Mambosasa amekuwa Mkuu wa Oparesheni UPEL Dodoma

> SACP Camilius Mongoso Wambura anatoka kuwa Mkuu wa Oparesheni UPEL Dodoma na kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar

Soma https://jamii.app/UhamishoWaPolisi
TANZANIA KUANZA KUTUMIA 5G

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dr. Jabir Kuwe amesema Tanzania inaelekea kuanza kutumia huduma ya 5G

> Majaribio ya #5G yatafanyika kuhakikisha kasi ya Teknolojia inayotakiwa inapatikana ili kuongeza Huduma ya Mawasiliano ya #Data nchini

Soma https://jamii.app/Tz5G

#DigitalRights
SHERIA YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI KUTUNGWA

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema Wizara yake iko mbioni kupeleka Bungeni muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi iili kulinda FARAGHA na TAARIFA za mwananchi

- Wizara inaandaa sheria hiyo ili kulinda FARAGHA na TAARIFA binafsi za wananchi katika hatua ya Ukusanyaji, Usafirishaji, Matumizi na Utunzaji wa taarifa hizo kwa kuwa Taasisi mbalimbali zinatumia taarifa husika

Soma > https://jamii.app/Tz5G