JamiiForums
52.4K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RC HAPI NA RC CHALAMILA WAHAMISHWA MIKOA

- Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza

- Aidha, amemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora

#JFLeo #Uteuzi
DPP MPYA NI SYLVESTER ANTHONY MWAKITALU

Rais Samia Suluhu amemteua Bw. Mwakitalu kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka

> Anachukua nafasi ya Biswalo Mganga aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu

#JFLeo #Uteuzi
QUEEN SENDIGA ATEULIWA KUWA RC IRINGA

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ADC, Queen Cuthbert Sendiga, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa

> Anachukua nafasi ya Ally Hapi aliyeteuliwa kuwa RC Tabora

#JFLeo
RAIS SAMIA AMTEUA DAVID KAFULILA KUWA RC ARUSHA

- Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. David Zacharia Kafulila kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha. Kafulila anachukua nafasi ya Bw. Idd Hassan Kimanta ambaye amestaafu

#JFLeo #Uteuzi
AMOS MAKALLA AWA RC DAR ES SALAAM

- Rais Samia Suluhu amemteua Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akichukua nafasi ya Aboubakar Kunenge ambaye amekuwa RC Pwani

- Pia, amemteua Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

#JFLeo
MAKONGORO NYERERE AWA MKUU WA MKOA MANYARA

- Mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere ameteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara akichukua nafasi ya Mkirikiti

- Mkirikiti amepelekwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa

#JFLeo #Uteuzi
RAIS SAMIA AMTEUA ADAM MALIMA KUWA RC WA TANGA

> Kabla ya Uteuzi huu, Adam Kigoma Malima alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara

> Pia, amemteua Bi. Rosemary Staki Senyamule kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita

#JFLeo #Uteuzi
SALUM HAMDUNI AWA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU

> Hamduni aliyepandishwa cheo na Rais Samia Suluhu kutoka ACP hadi Kamishna wa Polisi (CP) amechukua nafasi ya Brig. Jen. Mbungo atakayepangiwa majukumu mengine

#JFLeo #Uteuzi
RAIS SAMIA AMTEUA STEPHEN KAGAIGAI KUWA RC KILIMANJARO

- Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanzania, Stephen Kagaigai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akichukua nafasi ya Anna Mghwira aliyestaafu

#JFLeo #Uteuzi
GAGUTI RC MPYA MTWARA, BYAKANWA KUPANGIWA MAJUKUMU MENGINE

- Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mej. Jen. Marco Elisha Gaguti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara

- Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Gelasius Gasper Byakanwa atapangiwa majukumu mengine

#JFLeo #Uteuzi
RUVUMA: WATUMISHI WA MANISPAA YA SONGEA WATUHUMIWA KUJIMILIKISHA MADUKA YA KITUO KIKUU CHA MABASI

> Wananchi wamelalamika kwa DC Pololet Mgema kuwa, Watumishi wamejimilikisha maduka na hawayatumii kwa nia ya kuwapatia wafanyabiashara kwa bei kubwa

Soma https://jamii.app/MadukaSongea
YANGA NA NAMUNGO ZATOKA SULUHU

Namungo ya Lindi imetoka suluhu na Yanga SC kwa kutofungana katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

> Mchezo ulichezwa Uwanja wa Majaliwa ulio mkoani Lindi

#JamiiForums #JFMichezo
USAFI WA TAULO ILI KUEPUKA MAGONJWA

Taulo linabeba fangasi na bakteria ambao husababisha magonjwa, yakiwemo ya ngozi, UTI na muwasho

Wataalamu wanashauri kulifua kila baada ya siku 3 na kulipiga pasi. Pia kulianika juani baada ya kulitumia

Soma https://jamii.app/UsafiTaulo
PALESTINA: ISRAEL YAPOROMOSHA GHOROFA YA VYOMBO VYA HABARI

Jengo hilo la ghorofa 12 lilikuwa ni ofisi ya Shirika la Habari la AP, Al Jazeera, Ofisi nyingine pamoja na Makazi

Lilipigwa saa 1 baada ya Jeshi kuwataka Watu kuondoka ndani ya ghorofa

Soma - https://jamii.app/AlJazeeraOficeDown
👍1
MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI ZOEZI LA UPIGAJI KURA BUHIGWE

Jimbo hilo limekuwa wazi baada ya Dkt. Philip Mpango aliyekuwa Mbunge kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais

Pia, Uchaguzi mdogo wa Ubunge unafanyika Muhambwe na Kata 5 zinafanya Uchaguzi wa Madiwani

Soma > https://jamii.app/UchaguziBuhigwe
MASHAMBULIZI GAZA: Idadi ya Vifo vya Raia imeongezeka kufikia 174 tangu kuanza upya kwa mgogoro huo Jumatatu huku kukiwa na Vifo vya Watoto 47 na Wanawake 29. Inaelezwa Watu wanaathiriwa sana na Hewa nzito kutokana na Milipuko

Idadi ya watu walioumia imefikia 1,200. Israel inadaiwa kugoma kusitisha mashambulizi dhidi ya Wapalestina

#GazaUnderAttack
KILIMANJARO: WASTANI WA PIKIPIKI 100 HUIBWA KWA MWAKA

> Madereva huporwa pikipiki kwa kupigwa nondo, kunyongwa au kuumizwa

> Polisi imeshauri madereva, wanapokodiwa na mteja wanayemtilia shaka wampige picha kwa siri na kuiacha kijiweni

Soma https://jamii.app/PikipikiKilimanjaro
MAREKANI: CHAMA CHA WAUGUZI CHAPISHANA NA CDC KUHUSU UMUHIMU WA BARAKOA

- Chama hicho kimesema waliopata chanjo kushauriwa kutovaa barakoa hakutalinda Afya ya Umma na hatua hiyo haipo kisayansi

- Kimesema, huu sio wakati wa kulegeza Masharti

Soma https://jamii.app/WauguziCDC
TUNAKUTAKIA ‘WIKI’ NJEMA NA BARAKA TELE

Tunawatakia mwanzo mwema wa Juma uliojaa furaha na afya njema na kwa wale wenye changamoto katika afya zao, tunawaombea uponyaji wa haraka ili waendelee na majukumu yao

> Tembelea JF Doctors kwa ushauri kuhusu masuala ya #AFYA

#JamiiForums