JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTAFITI: KULALA KWA SAA 6-7 USIKU KUTAKUEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO

Utafiti wa Chuo Kikuu cha #Cardiology cha Marekani umebaini Watu wanaolala kwa saa 6-7 wakati wa usiku wana uwezekano mdogo zaidi wa kupata mshtuko wa Moyo au Kiharusi

Soma - https://jamii.app/UsingiziMoyo
#JFAfya
UTAFITI: WAGONJWA WALIOKAA ICU WAPO KWENYE HATARI YA KUJIUA NA KUJIDHURU

Watafiti kutoka Ottawa wamesema matokeo ya Utafiti huo yana umuhimu mkubwa wakati huu ambapo watu wengi wamewekwa katika Uangalizi maalum kwasababu ya mlipuko wa #COVID19

Soma > https://jamii.app/UtafitiWagonjwaICU
#COVID19-UINGEREZA: KARANTINI YASABABISHA VIFO VYA UNYWAJI POMBE KUONGEZEKA

Ofisi ya Takwimu imesema kulikuwa na vifo 7,423 Mwaka 2020 ikiwa ni ongezeko la 19.6% kutoka 2019

Unywaji Pombe uliongezeka baada ya Watu kutakiwa kukaa majumbani

Soma - https://jamii.app/AlcoholDeathsUK
#COVID19: MAAMBUKIZI MAPYA ZAIDI YA 400,000 YAREKODIWA INDIA

Maambukizi katika Nchi hiyo yamefikia Milioni 21.49 huku waliofariki dunia hadi sasa wakiwa 234,083

#India yenye takriban watu Bilioni 1.4 imeshatoa Dozi Milioni 162 za Chanjo

Soma > https://jamii.app/COVIDCasesIndia
NEW ZEALAND KUZUIA UVUTAJI SIGARA KWA WALIOZALIWA BAADA YA 2004

Serikali inataka hadi kufikia 2025 kusiwepo na Mtu anayevuta Sigara Nchini humo

Takriban Watu 4,500 Nchini humo hupoteza Maisha kila mwaka kutokana na matumizi ya Tumbaku

Soma - https://jamii.app/ZealandTobaccoBan
#SmokingBan
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
UINGEREZA: JESHI LA MAJI LATUMIA TEKNOLOJIA YA MTU KUPAA ILI KUPAMBANA NA UHALIFU BAHARINI

- Kampuni ya Utafiti wa #Teknolojia ya Anga ya Gravity Industries imechapisha video inayoonesha Wanajeshi wakifanya mazoezi kwa kutumia Teknolojia hiyo mpya katika Meli ya kivita ya HMS Tamar ya Uingereza.

#JamiiForums #Technology #Crimes
DR CONGO: MDOGO WA RAIS JOSEPH KABILA AONDOLEWA MADARAKANI

Zoe Kabila aliyekuwa Gavana wa Tanganyika amepigiwa kura ya kuondolewa akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya Madaraka

Desemba 2020, wafuasi wa Kabila waliokuwemo Bungeni waliondolewa

Soma > https://jamii.app/ZoeKabilaDRC
NDUGAI: WANAOFUKUZA WANACHAMA WAAMBATANISHE KATIBA YAO NA MIHUTASARI YA VIKAO KWENYE BARUA

Spika wa Bunge amesema, "Kufanya hivyo inarahisisha kazi yangu ya kutenda Haki nisije nikaonea watu. Wenye nia hizo mnaogopa nini kuambatanisha hizo Nakala?"

Soma > https://jamii.app/NdugaiBunge
DOGO JANJA AHOJIWA KWA MADAI YA KUHAMASISHA ABIRIA KUTOPIMA #COVID19

Msanii Abdulaziz Chende (26) aliyerudi kutoka Afrika Kusini amelalamika kwamba alifanya Kipimo alikotoka lakini Cheti kilikataliwa na kutakiwa kulipa fedha ili kupima upya

Kamanda wa Kikosi cha Viwanja vya Ndege Nchini, Jeremia Shila, amesema wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kama tuhuma zinazomkabili Dogo Janja na Wenzake wawili ni za jinai ili wafikishwe Mahakamani.

Soma - https://jamii.app/DogoJanjaCorona
AAR YATANGAZA KUFILISIWA. YAFUNGA KLINIKI ZAKE NA KUUZA VIFAA VYA MATIBABU

Kampuni ya AAR Healthcare (T) Ltd imetangaza kuuza vifaa vyote vilivyopo kwenye Kliniki zake 7

Aprili 28, 2021 Wafanyakazi waliandamana wakidai kulipwa stahiki zao

Soma - https://jamii.app/AARYafilisiwa
MBUNGE ASHAURI KUWEPO SERA YA WATANZANIA KUVUNA MAJI YA MVUA

Dkt. Alfred Kimea ameshauri kutengenezwa Sera itakayowafanya Watanzania wawe na tabia ya kuvuna Maji ya Mvua

Amesema, "Kila Mtanzania mwenye Nyumba ya Bati tayari ana chanzo cha Maji"

Soma > https://jamii.app/SeraMajiMvua
Parachichi pia lina faida zifuatazo;

- Parachichi husaidia afya ya Mama Mjamzito na ukuaji wa mtoto aliye tumboni

- Parachichi husaidia afya ya Mama Mjamzito na ukuaji wa mtoto aliye tumboni

#JamiiTalks #JamiiForums
SERIKALI: TANZANIA HAINA WAFUNGWA WA KISIASA

Serikali imesema hayo leo Mei 07, 2021 baada ya Chombo cha Habari kutoka Nchi jirani kuripoti Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo la kuachiwa Wafungwa 23 wa Kisiasa Nchini

Soma > https://jamii.app/TZWafungwaSiasa
Baadhi ya aliyosema Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Dar mbele ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 07, 2021 Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam