JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: AFISA TRA TEMEKE AKAMATWA KWA RUSHWA

Humphrey Mhagama amekamatwa kwa kuomba Tsh. 500,000 ambapo alipokea Tsh. 250,000

TAKUKURU imesema Mtuhumiwa atafunguliwa Mashtaka kwa kosa la kushawishi, kuomba na kupokea Rushwa

Soma > https://jamii.app/RushwaAfisaTRA
Hutumika kuongoza mahusiano kati ya Viongozi na Watumishi wa Umma, Bodi mbalimbali za Kitaaluma, Vyombo vya Habari, Wadau na Makundi mengine ya wananchi katika jamii

> Kwa ujumla huwataka Viongozi wa Umma kufanya kilicho sahihi ikiwa ni pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, weledi, uwajibikaji na uwazi

#GoodGovernance
DAR: WATU 161 WAKAMATWA KWA WIZI WA MAGARI NA PIKIPIKI

Watano kati yao wamekamatiwa Zanzibar wakiwa na pikipiki 40

Vilevile, Polisi imekamata vitu mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa vya wizi vikiwemo pikipiki 91, bajaji na vipuri vya magari

Soma > https://jamii.app/161WiziDar
HOJA: EPUKA KUFUATA MKUMBO IKIWA UNATAKA KUFANIKIWA

> Mdau anasema usishiriki kwenye mabishano yoyote ambayo hayana manufaa kwako. Usifanye jambo sababu wa Watu bali tumia akili zako kufanya kilicho sahihi.

> Kitu pekee kinachotutofautisha Binadamu na viumbe wengine ni uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi kulingana na hali tuliyonayo

Mjadala zaidi - https://jamii.app/MkumboMafanikio
#Maisha
UHAMISHO KWA WATUMISHI KUFANYIKA MARA 4 KWA MWAKA

- Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI amewataka Makatibu Tawala kutokupitisha maombi ya wanaotaka kuhamia kwenye Majiji, Manispaa na Miji kwa kuwa maeneo hayo yana idadi kubwa ya Watumishi

Soma > https://jamii.app/UhamishoWatumishi
MTWARA: 11 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI

Wanadaiwa kughushi nyaraka za Serikali na kulipwa fedha za fidia isivyo halali, na kuisababishia Halmashauri ya Wilaya ya Masasi hasara ya zaidi ya Milioni 13.2

Soma > https://jamii.app/11UhujumuMtwara
UTAFITI: KULALA KWA SAA 6-7 USIKU KUTAKUEPUSHA NA MAGONJWA YA MOYO

Utafiti wa Chuo Kikuu cha #Cardiology cha Marekani umebaini Watu wanaolala kwa saa 6-7 wakati wa usiku wana uwezekano mdogo zaidi wa kupata mshtuko wa Moyo au Kiharusi

Soma - https://jamii.app/UsingiziMoyo
#JFAfya
UTAFITI: WAGONJWA WALIOKAA ICU WAPO KWENYE HATARI YA KUJIUA NA KUJIDHURU

Watafiti kutoka Ottawa wamesema matokeo ya Utafiti huo yana umuhimu mkubwa wakati huu ambapo watu wengi wamewekwa katika Uangalizi maalum kwasababu ya mlipuko wa #COVID19

Soma > https://jamii.app/UtafitiWagonjwaICU
#COVID19-UINGEREZA: KARANTINI YASABABISHA VIFO VYA UNYWAJI POMBE KUONGEZEKA

Ofisi ya Takwimu imesema kulikuwa na vifo 7,423 Mwaka 2020 ikiwa ni ongezeko la 19.6% kutoka 2019

Unywaji Pombe uliongezeka baada ya Watu kutakiwa kukaa majumbani

Soma - https://jamii.app/AlcoholDeathsUK
#COVID19: MAAMBUKIZI MAPYA ZAIDI YA 400,000 YAREKODIWA INDIA

Maambukizi katika Nchi hiyo yamefikia Milioni 21.49 huku waliofariki dunia hadi sasa wakiwa 234,083

#India yenye takriban watu Bilioni 1.4 imeshatoa Dozi Milioni 162 za Chanjo

Soma > https://jamii.app/COVIDCasesIndia
NEW ZEALAND KUZUIA UVUTAJI SIGARA KWA WALIOZALIWA BAADA YA 2004

Serikali inataka hadi kufikia 2025 kusiwepo na Mtu anayevuta Sigara Nchini humo

Takriban Watu 4,500 Nchini humo hupoteza Maisha kila mwaka kutokana na matumizi ya Tumbaku

Soma - https://jamii.app/ZealandTobaccoBan
#SmokingBan
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
UINGEREZA: JESHI LA MAJI LATUMIA TEKNOLOJIA YA MTU KUPAA ILI KUPAMBANA NA UHALIFU BAHARINI

- Kampuni ya Utafiti wa #Teknolojia ya Anga ya Gravity Industries imechapisha video inayoonesha Wanajeshi wakifanya mazoezi kwa kutumia Teknolojia hiyo mpya katika Meli ya kivita ya HMS Tamar ya Uingereza.

#JamiiForums #Technology #Crimes
DR CONGO: MDOGO WA RAIS JOSEPH KABILA AONDOLEWA MADARAKANI

Zoe Kabila aliyekuwa Gavana wa Tanganyika amepigiwa kura ya kuondolewa akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya Madaraka

Desemba 2020, wafuasi wa Kabila waliokuwemo Bungeni waliondolewa

Soma > https://jamii.app/ZoeKabilaDRC
NDUGAI: WANAOFUKUZA WANACHAMA WAAMBATANISHE KATIBA YAO NA MIHUTASARI YA VIKAO KWENYE BARUA

Spika wa Bunge amesema, "Kufanya hivyo inarahisisha kazi yangu ya kutenda Haki nisije nikaonea watu. Wenye nia hizo mnaogopa nini kuambatanisha hizo Nakala?"

Soma > https://jamii.app/NdugaiBunge