JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBUNGE: KWANINI MIKATABA HAIWEKWI WAZI WAKATI SHERIA TULIITUNGA WENYEWE?

- Jesca David Kishoa asema kuweka wazi Mikataba iliyoingiwa na Serikali kwa niaba ya Raia kutajenga uaminifu kati ya Wananchi na Serikali kwasababu Rasilimali ni za Watanzania

Soma https://jamii.app/UwaziMikatabaTZ
MBUNGE: WAZABUNI WANAOIDAI STAMICO WALIPWE, TUACHE KIGUGUMIZI

- Dunstan Kitandula amesema zoezi la Vyombo vya Serikali kutathmini madeni hayo limefanywa kwa muda mrefu

- Ametaka madeni kulipwa kwa Haki akisema ujanja usitumike kuyakwepa

Soma > https://jamii.app/MadeniSTAMICO
ARUSHA: MUUGUZI AJINYONGA KWA MSONGO WA MAWAZO

- Uchunguzi wa awali umebaini David Mtaita (30) aliyekuwa Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Arumeru alijinyonga kwasababu ya Msongo wa Mawazo uliotokana na madeni

Soma > https://jamii.app/KifoMuuguzi
MALAWI YATANGAZA ADHABU YA KIFO KUWA KINYUME CHA KATIBA

> #Malawi ni Nchi ya 22 Kusini mwa Jangwa la Sahara kusitisha adhabu ya kifo ambapo tangu 1975 hakuna aliyenyongwa

> Tume ya #HakiZaBinadamu imesema uamuzi huo ni maendeleo

Soma - https://jamii.app/MalawiBansDeathPenalty
KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2022: UGANDA YAOMBA KUTUMIA UWANJA WA MKAPA

Baada ya FIFA kusema Viwanja vya Uganda havina vigezo, Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) limeomba wautumie Uwanja wa Mkapa (Tanzania) kama Uwanja wao wa nyumbani

Soma>https://jamii.app/UgandaTanzania
UMEWAHI KUTAPELIWA NA RAFIKI AU NDUGU YAKO? ULICHUKUA HATUA GANI?

> Marafiki/ndugu ni rahisi kuwaaamini na kuwapatia fedha nyingi kiuaminifu ambapo mara nyingine wanaweza kuvunja uaminifu

> Je umeshawahi kutapeliwa na ndugu? Ulichukua hatua gani?

Soma https://jamii.app/NduguUtapeli
DAR: MABASI 35 YAZUILIWA KUENDELEA NA SAFARI STENDI YA MAGUFULI

> Mkuu wa Usalama Barabarani ktk Kituo hicho, ASP Ibrahim Samwix, amezuia Mabasi 35 kufanya safari kutokana na ubovu na hayataruhusiwa kuendelea na kazi mpaka yatakapotengenezwa

Soma https://jamii.app/Gari35Mbezi
WATU 231 WAKAMATWA KWA UHALIFU SHINYANGA

- Miongoni mwao ni wenye makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, wakata mapanga na waganga wanaojihusisha na ramli chonganishi

- Pia, Polisi Mkoani humo imekamata Bunduki, Bangi, Heroine na mirungi

Soma > https://jamii.app/Wahalifu231Shy
KILIMANJARO: WAJUMBE WA BODI YA GOFU KLABU YA MOSHI KUKAMATWA KWA KUTOLIPA KODI

> Kiwanja cha Gofu Moshi kinadaiwa kutolipa Kodi ya Ardhi Tsh. Milioni 26 tangu 2013

> Aidha, Wanachama wanalipa Tsh. 100,000 kila mwaka na haijulikani zinavyotumika

Soma - https://jamii.app/GofuKlabu
ONI SIGALA: 70% YA NYIMBO ZA BONGOFLEVA ZIMEJAA MATUSI

> Wasanii wanaotumia lugha za matusi ktk kazi zao watashughulikiwa na BAKITA kwa kushirikiana na BASATA

> Oni Sigala amesema #Kiswahili ni bidhaa ambayo inapaswa kutumiwa kwa usahihi

Soma https://jamii.app/LughaSanaa
#Burudani
FANYA HIVI KUMSAIDIA MWANAO APATE USINGIZI MWANANA

- Shughuli zake wakati wa usiku ziwe tulivu na chache huku zikipungua kadri muda unavyokwenda

- Fanya mazingira ya chumbani kwake kuwa yasiyobadilika. Epusha kelele na sauti za kushtua usiku wa manane

Soma > https://jamii.app/UsingiziWatoto

#Watoto #JamiiForums #JamiiTalks
WAJIBU WA MTUMIAJI WA MTANDAO WA INTANETI

- Wajibika kuripoti matukio yote ya kudhalilisha utu wa mtu, wizi wa picha au utambulisho wa Mtu na ulaghai kwa njia ya ujumbe mfupi

- Unawajibika kulinda na kuheshimu Hakimiliki ya kazi za Sanaa na Uandishi wa Watu wengine. Usiibe kazi ya mtu.

#DataProtection #DigitalRights #JamiiForums #JamiiTalks
WAZIRI MKUU: TUTAWEKEZA KATIKA TEKNOLOJIA ILI UKAGUZI MGODI WA MERERANI USIWE WA KUDHALILISHA

> Mgodi wa Mererani umelalamikiwa kuwavua watu nguo kwa makundi ili kuwakagua kama hawajaiba kitu

> Aina hii ya ukaguzi imesemwa kuwa ni udhalilishaji

Soma https://jamii.app/UkaguziKuvuliwaNguo
TCRA: BEI ZA VIFURUSHI ZIMEREJEA KAMA AWALI

- Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaarifu kurejeshwa kwa bei za awali za vifurushi vya mawasiliano

- Raia mwenye changamoto atoe taarifa kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii

Soma https://jamii.app/VifurushiVimerekebishwa
#DigitalRights
ISRAEL: WATU 44 WAFARIKI DUNIA KWA KUKANYAGANA

- Vifo hivyo vimetokea katika tamasha la kidini ambapo wengine wamejeruhiwa

- Imeripotiwa maelfu walihudhuria tamasha hilo ambalo limetajwa kuwa kubwa zaidi Israel tangu kuanza kwa #COVID19

Soma https://jamii.app/44DieIsrael
SHINYANGA: WATUMISHI KUFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MATUMIZI MABAYA YA MAMLAKA

- TAKUKURU itawafikisha Mahakamani Watumishi wa Halmashauri, Godfrey Mwagairo na Edward Maduhu

- Mwagairo atashtakiwa kwa Uhujumu Uchumi na Maduhu kwa kosa la jinai

Soma > https://jamii.app/WatumishiMahakamani
AINA MPYA YA KIRUSI CHA CORONA KUTOKA INDIA CHARIPOTIWA UGANDA

- Mbali na Kirusi hicho cha B.1.617, aina nyingine 4 zimethibitishwa Nchini humo

- Mamlaka zimesema Virusi vinavyosambaa zaidi #Uganda ni kutoka UK, Afrika Kusini na #India

Soma > https://jamii.app/IndianVariantUG
ZIMBABWE YALAUMIWA KWA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU TANGU KUWEPO KWA #COVID19

> #Zimbabwe imelaumiwa kukiuka haki za kimsingi za Binadamu ikiwemo kuwakamata Wanaharakati kwa kuandamana dhidi ya Serikali kushindwa kuwasaidia walioathiriwa

Soma - https://jamii.app/HakiZaBinadamuZimbabwe