JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VPL: SIMBA YAENDELEA KUJIKITA KILELENI MWA MSIMAMO WA LIGI

- Simba imeendelea kujitengenezea nafasi nzuri kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu baada ya kuitandika Dodoma Jiji goli 3-1

- Magoli ya Simba yamefungwa na C. Mugalu 8' 68', L. Miquissone 56' huku goli la Dodoma Jiji likifungwa na C. Mkangala 29'

- Kwa matokeo hayo Simba inafikisha alama 61 ikiwa ni alama 4 juu ya Yanga inayoshika nafasi ya pili kwa alama 57

#JamiiForums #JFSports
UCL: CHELSEA YATOSHANA NGUVU NA MADRID

Mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Real Madrid dhidi ya Chelsea umemalizika kwa sare ya 1-1
-
Mchezo wa marudiano utapigwa Jumatano ijayo ya tarehe 5 Mei 2021 katika Dimba la Stamford Bridge

#JamiiForums #JFSports #UEFA
MHADHIRI TUDARCo ADAI FIDIA KWA KUWEKEWA MAZINGIRA MAGUMU ILI AACHISHWE KAZI

> Dkt. Kamanija amefungua kesi ya madai Baraza la Usuluhishi wa Migogoro ya Kazi akidai fidia ya Tsh. Milioni 130

> Kamanjina ni kati ya Waanzilishi wa Kitivo cha Sheria

Soma https://jamii.app/MizengweKazini
BURKINA FASO: WAANDISHI WAWILI WA HISPANIA WAUAWA

- Wanahabari hao walitekwa nyara karibu na eneo la Hifadhi ya asili Mashariki mwa Burkina Faso

- Vyombo vya Usalama vimesema raia wa #Ireland pia ameuawa ingawa hilo halijathibitishwa rasmi

Soma - https://jamii.app/WaandishiBurkinaFaso
WHO: WIMBI LA MAAMBUKIZI INDIA NI MATOKEO YA MIKUSANYIKO

- Shirika la Afya limesema wimbi hilo ni matokeo ya mikusanyiko ya watu, viwango vidogo vya Chanjo na uwepo wa aina mpya za Virusi

- Visa 17,997,267 vya Corona vimerekodiwa na vifo ni 201,187

Soma https://jamii.app/WHOCoronaIndia
SERIKALI YATENGA BILIONI 2 KAMA FIDIA KWA WATAKAOVAMIWA NA WANYAMAPORI

- Serikali imesema itawafidiwa Wananchi kulingana na uharibifu utakaojitokeza

> Matukio ya uvamizi wa Wanyamapori yamekuwa yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali Nchini

Soma - https://jamii.app/Bilioni2Fidia
SOMALIA: RAIS ATOA RAI YA KUFANYIKA UCHAGUZI BAADA YA KUONGEZEWA MUDA MADARAKANI

-
Kitendo cha Wabunge kumuongezea Rais miaka 2 kiliibua sintofahamu huku Mataifa yakitishia vikwazo

- Kumekuwa na mvutano tangu Februari baada ya muda wa Rais kumalizika

Soma - https://jamii.app/RaisUchaguziSomalia
SERIKALI YAANDAA MUSWADA WA TARATIBU ZA UVUNAJI NA UPANDIKIZAJI VIUNGO VYA BINADAMU

- Naibu Waziri wa Afya ameeleza hayo akimjibu Mbunge aliyehoji mkakati wa kuanzisha utaratibu wa kuvuna viungo

- Asema kwa sasa Nchi inatumia miongozo ya Kimataifa

Soma https://jamii.app/MuswadaViungo
WANAOISHI KARIBU NA HIFADHI WASHAURIWA KULIMA PILIPILI KUEPUKA UVAMIZI WA TEMBO

> Naibu Waziri wa Maliasili amesema maboga na matikiti huvutia Tembo kuvamia mashamba

> Njia nyingine ni kumwaga Oil chafu iliyochanganywa na Pilipili na majivu

Soma https://jamii.app/MbinuMbadala
SITI BINTI SAAD: MWANAMUZIKI WA KWANZA KUTOKA ZANZIBAR KWENDA KUREKODI NCHINI INDIA.

- Siti binti Saad alizaliwa mwaka 1880 na alifariki 1950.

- Alikuwa Mwanamke wa kwanza Afrika Mashariki kurekodi muziki wake katika mfumo wa albamu.

Soma > https://jamii.app/WasifuSiti
HASUNGA: USHIRIKA UNALAZIMISHA WASIO WANACHAMA KUUZA MAZAO KUPITIA VYAMA

- Amehoji Serikali haioni ulazima wa kuruhusu Wafanyabiashara kununua kwa Wakulima bila Ushirika

- Serikali yasema inaamini Mfumo wa Ushirika ni njia itakayomsaidia Mkulima

Soma > https://jamii.app/MazaoUshirika
ZINGATIA YAFUATAYO UNAPOOMBA USHAURI

- Kuwa makini unapochagua mtu wa kumuomba ushauri. Zingatia uzoefu wa huyo mtu kwenye jambo husika na ukaribu mlionao

- Kuwa wazi juu ya unachotaka kushauriwa, elezea vizuri chanzo cha tatizo lako

- Ikiwezekana jaribu kutatua tatizo mwenyewe kwanza, kisha umweleze mtu unayemuomba ushauri mahali ulipokwama ili akusaidie kutokea hapo

#JamiiForums #JamiiTalks
KILIMANJARO: WAGONJWA WA AKILI WAONGEZEKA

> Mwaka 2019, Wagonjwa walikuwa 8,691 na mwaka 2020 idadi ilipanda hadi 12,152

> Kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha kumetajwa kuwa moja ya sababu za ongezeko

Soma https://jamii.app/WagojwaWaAkil
PROF. KABUDI: SHERIA ZITAKUWA ZIMETAFSIRIWA IFIKAPO DESEMBA

- Akiwa Bungeni, Waziri amesema Wizara nyingine na Taasisi zinaendelea na zoezi la kutafsiri #Sheria zinazosimamia ili ifikapo Desemba Sheria zote ziwe zimetafsiriwa kwa Kiswahili

Soma > https://jamii.app/TafsiriSheria
MBUNGE: KUNA MRUNDIKANO MAGEREZANI KWASABABU YA KESI ZA KUBAMBIKIWA

- Agnesta Kaiza amesema "Kila leo unasikia fulani ana kesi ya Uhujumu Uchumi"

- Asema uwepo wa masharti magumu ya dhamana ni sababu nyingine ya mrundikano ktk Magereza na Mahabusu

Soma - https://jamii.app/MbungeMagereza