JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
GEITA: JELA MIAKA MITATU KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA YA TSH. 30,000

> Samson Kuzenza, Afisa Tabibu wa Kituo cha Afya Katoro alimuomba Said Msuluzya Tsh. 30,000 ili amsafishe mkewe aliyeharibikiwa mimba

> Huduma kwa wajawazito hutolewa bure

Soma https://jamii.app/Jela3Rushwa
MAREKANI YAIWEKEA VIKWAZO UTURUKI KWA KUNUNUA SILAHA ZA URUSI

- Marekani imesema matumizi ya S-400 ni kinyume na Teknolojia ya #NATO na ni tishio kwa washirika wake

- Vikwazo vinailenga sekta ya ununuzi wa silaha ya Uturuki na Maafisa wake

Soma - https://jamii.app/USSactionsTurkey
MDAU: ASHAURI WAFIWA KUCHUNGA MANENO WANAPOOMBOLEZA

> Mdau asema, baadhi ya wafiwa hutamka mambo ya kifamilia hadharani wakiwa wanalia

> Anashauri kuchunga maneno ya kuongea licha ya machungu na msiba ili siri za Familia zisianikwe kwa watu

Soma https://jamii.app/KuombolezaWamama
SERIKALI YAITAKA TRA KUKUSANYA TRILIONI 2 KWA MWEZI

- Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema sio lengo la Serikali kufungia biashara ya mtu

- Amewataka Watendaji kutumia busara ikiwemo kuepuka rushwa, vitisho, ubabe na kuwabambikia kodi Wananchi

Angalia https://youtu.be/fzH9alK2I_k
SERIKALI YAANZA UCHUNGUZI DHIDI YA QNET BAADA YA WENGI KULALAMIKA WAMETAPELIWA

> Kampuni ya QNET imeanza kuchunguzwa, huku Polisi wakiwataka wanaodhani kutapeliwa wakaripoti

> Baadhi ya wahanga waliacha kazi kwa ahadi za kuwa mabilionea

Soma - https://jamii.app/QNetUnderInvestgation
EU YATOA MSAADA KWA TANZANIA ILI KUSAFIRISHA UMEME KWENDA ZAMBIA

- Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), umetoa msaada wa Tsh. Bilioni 84 ili kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme kati ya #Tanzania na #Zambia

Soma https://jamii.app/TZEuromil30EU
UGANDA YAITAKA GOOGLE KUFUNGA BAADHI YA ONLINE TV YOUTUBE

- Tume ya Mawasiliano (UCC) imeitaka Google ifunge Online TV 13 ikiwemo Ghetto TV inayomilikiwa na Bobi Wine

- Inadai TV hizo zilitumika kueneza machafuko yaliyotokea hivi karibuni

Soma - https://jamii.app/UGYoutubeTvs
CHINA KUISAIDIA TANZANIA KWENYE MRADI WA UMEME RUFIJI NA RELI YA SGR

> Rais Magufuli akizungumza kwa simu na Rais wa #China, Magufuli ameiomba China kushirikiana na #Tanzania ktk miradi kwa kutoa mikopo nafuu ikiwemo Miradi ya kuzalisha Umeme

Soma https://jamii.app/ChinaMsaadaTZ
WATU WENGI HAWATAPATA CHANJO YA #COVID19 HADI 2022

> Utafiti unaonesha Mataifa Tajiri yameagiza zaidi ya nusu ya dozi ya chanjo ambayo itazalishwa na Makampuni 13

> 40% ya chanjo inaweza kupatikana kwa mataifa yenye Kipato cha Chini na cha Kati

Soma https://jamii.app/COVID19Y2022
TAKRIBAN ASILIMIA 80 YA WATANZANIA HAWAJAJIUNGA NA BIMA YA AFYA

- Mkurugenzi wa Afya TAMISEMI, Dkt. Ntuli Kapologwe, amesema takriban 5% ya Watanzania ndio wamejiunga na CHF iliyoboreshwa, huku waliojiunga na NHIF ni 8% na Bima Binafsi ni 1%

Soma https://jamii.app/BimaAfyaWatz
CPJ: MWAKA 2020, WAANDISHI 274 WAMEFUNGWA KUTOKANA NA KAZI ZAO

> China inatajwa kuwa kinara wa kuwakamata Waandishi, ikifuatiwa na Uturuki, Misri, Saudi Arabia na Belarus

> Utafiti haujajumuisha Waandishi waliopotea au kutoweka

Soma https://jamii.app/Journalists2020
ETHIOPIA: WATOTO MILIONI 2 WAKOSA MSAADA JIMBO LA TIGRAY

> Mashirika ya kutoa misaada yanalalamikia kuzuiliwa kuingia Tigray mbali na makubaliano yaliyofikiwa

> Desemba mwanzoni Wanajeshi waliwaelekezea risasi Wafanyakazi wa UN huko Tigray

Soma https://jamii.app/WatotoEthiopia
JE, UNAZIJUA HAKI ZA MTOTO IKIWA WAZAZI WAKE WAMETENGANA?

Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 kifungu cha 26 (1)

(a) Kuendelea kupata elimu bora aliyokuwa akiipata kabla ya Wazazi wake kutengana au talaka

(b) Kuishi na Mzazi ambaye, kwa maoni ya Mahakama, ana uwezo wa kulea na kumtunza Mtoto katika maslahi bora ya Mtoto; na

(c) Kumtembelea na kukaa na mzazi mwingine wakati wowote Mtoto atapohitaji, isipokuwa mpangilio huo ukiingiliana na ratiba ya shule au mafunzo

Soma > https://jamii.app/HakiMtotoWazazi

#HakiZaWatoto #JamiiForums #CDF #JFLeo
LUDEWA: MADIWANI WATAKIWA KUHAKIKISHA WANAFUNZI WA KIDATO CHA 1 WANARIPOTI SHULENI

> Katibu Tawala wa Wilaya hiyo amewataka Madiwani wote kuhakikisha mpaka Januari 30, 2021 Watoto wa Darasa la 7 waliopangiwa Shule wanaripoti na kuanza masomo

Soma https://jamii.app/Kidato1Ludewa
BAADA YA UHUSIANO WA KENYA NA SOMALIA KUFA, KENYA ITAFUNGUA UBALOZI SOMALILAND

> Kenya ilimpokea Rais wa Somaliland na kufanya uhusiano na Somalia kuvunjika

> Somaliland ilijitangazia uhuru, mwaka 1991 ila haitambuliki Kimataifa kama Nchi

Soma https://jamii.app/SomalilandKenya
PAKISTAN YAPITISHA SHERIA YA KUWAHASI WABAKAJI

> Pakistan imepitisha Sheria hiyo baada ya maandamano ya Raia waliokerwa na kauli ya Mkuu wa Polisi aliyesema Mwanamke mmoja aliyebakwa na Wanaume kadhaa kuwa alikuwa na makosa

Soma https://jamii.app/CastrationLaw
AIDAN EYAKUZE ATAJWA MIONGONI MWA WENYE USHAWISHI WA MAGEUZI YA KIUTAWALA

> Taasisi ya Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) imemtambua Mkurugenzi Mtendaji wa TWAWEZA miongoni mwa Watu 50 Wenye Ushawishi Duniani na Watetezi wa Wananchi wa kawaida

Soma - https://jamii.app/AidanEyakuzeWEF
WANAOTUHUMIWA KUMUUA ALPHONCE MAWAZO WADAI MASHTAKA DHIDI YAO YAMETENGENEZWA

> Washtakiwa 5 ktk kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa M/Kiti wa CHADEMA, Geita na Kanda ya Ziwa wameanza kutoa ushahidi wao na kuiomba Mahakama kuwaachia huru

Soma https://jamii.app/UteteziMauajiMawazo
DR-CONGO YATANGAZA 'CURFEW' BAADA YA MAAMBUKIZI YA #COVID19 KUONGEZEKA

> Baada ya saa tatu usiku hakuna atakayeruhisiwa kutoka nje na Polisi wataanza doria. Maandamano, matamasha na muziki vikipigwa marufuku

> Desemba 18 Wanafunzi wataanza likizo

Soma https://jamii.app/CurfewDRC
KUMCHUKIA/KUWA NA KINYONGO NA MTU INAKUUMIZA WEWE SIO UNAYEMCHUKIA

- Mdau wa JamiiForums anasema, Jiulize kwa ambao umewachukia, wameathirika na kitu gani juu ya kutowapenda kwako? Je, wewe mwenyewe umefaidika na nini?

- Usilalamike na kutafuta namna ya kuwa na furaha au mitazamo mizuri, hayo ni ngumu kuyapata kama unawekwa vinyongo na chuki kwa wengine

Tembelea - https://jamii.app/ChukiVinyongo
#Hate #Love