JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ZANZIBAR: AHUKUMIWA KUTUMIKIA CHUO CHA MAFUNZO KWA KUBAKA

- Mahakama imemuhukumu Khalifa Khalfan Mwaveso (25) kwenda kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa miaka kumi (10) na kulipa fidia ya Tsh. Laki 2 kwa kosa la kumbaka msichana wa miaka 17

Soma - https://jamii.app/HukumuChuoUbakaji
WATUMISHI 22 WA TRA WASIMAMISHWA KAZI KWA KUTOTIMIZA MAJUKUMU IPASAVYO

> Dkt. Mpango ameagiza Watumishi 22 wasimamishwe kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za uzembe na ufisadi

> Pia, ameagiza maafisa waliokaa kituo kimoja muda mrefu wahamishwe

Soma https://jamii.app/22Wasimamishwa
WIZARA YA AFYA: KUNA HAJA YA KUENDELEZA VITUO VYA TIBA ASILI

> Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara hiyo amesema, Ukoloni umefanya watu wadharau dawa za asili ambazo zilikuwa zinatumika Afrika

> Kwa Takwimu, 80% ya dawa zinaagizwa kutoka nje

Soma https://jamii.app/TibaAsili
DAR: MBARONI KWA KURUSHA MAUDHUI MTANDAONI BILA KIBALI

> Benedict Kimbusu anatuhumiwa kusambaza maudhui kwenye Chaneli ya YouTube inayoitwa Poih the 90s Lyrics bila kibali

> Amedaiwa kufanya kosa hilo kati ya Februari 27, 2014 na Desemba 7, 2020

Soma https://jamii.app/MaudhuiBilaKibali
ARUSHA: DC AWACHAPA BAKORA WANAFUNZI KWA TUHUMA ZA KUUZA MADAWATI KAMA CHUMA CHAKAVU

> Wanafunzi 3 wa Kidato cha Kwanza Shule ya Sekondari Sinoni wameiba madawati 108 yenye thamani ya Tsh. Milioni 10

> Watu 5 waliouziwa wamekamatwa na Polisi

Soma https://jamii.app/ArushaWanafunzi
MR. KUKU AHUKUMIWA MIAKA 10 AU FAINI MILIONI 5

- Tariq Machibya amehukumiwa kwa kujihusisha na biashara ya upatu na kupokea miamala ya fedha bila leseni

- Pia, Tsh. Bilioni 5.4 ambazo zipo kwenye akaunti yake zitaenda kwenye akaunti ya DPP

Soma - https://jamii.app/HukumuMrKuku
JAMES HAMBLIN: DAKTARI AMBAYE HAONI UMUHIMU WA KUOGA

> James Hamblin hajaoga miaka 5 na hajapata madhara. Anafafanua kuwa, harufu hutokana na mafuta, mwili huacha kuyatoa usipooga muda mrefu

> Anasema, mtu hutumia wastani wa miaka 2 kuoga, muda ambao angefanya kazi

Soma https://jamii.app/5yrsKuoga
UGANDA: GOOGLE YAKATAA KUFUNGA 'CHANNEL' KWA MAOMBI YA SERIKALI

> Google imesema inafuata Sheria za Nchi lakini ni lazima iwe Amri ya Mahakama

> UCC iliitaka Google ifute Chaneli 17 za YouTube ikiwemo ya Bobi Wine ikidai hazizingatii Mizania

Soma https://jamii.app/GoogleUG
UGANDA: RAIS MUSEVENI AMTEUA MWANAYE KUWA KAMANDA WA KIKOSI MAALUM JESHINI

- Lt. Gen. Muhoozi Kainerugaba (46) amekuwa Kamanda wa Kikosi cha SFC ambacho humlinda Rais wa #Uganda na kusimamia majukumu mengine ya kipekee kulingana na Amri za Rais

Soma https://jamii.app/MuseveniElectSon
NIGERIA: WALIMU WAITISHA MGOMO KWA UKOSEFU WA USALAMA

> Walimu wameitisha mgomo kutokana na kuwa ktk hatari ya kuvamiwa na Makundi ya Wenye Silaha

> Hivi karibuni Boko Haram waliwateka Wanafunzi 300, hali iliyopelekea shule nyingine kufungwa

Soma https://jamii.app/NigeriaMgomo
BAWACHA YAWATAKA MDEE NA WENZAKE KUACHA KUTUMIA NEMBO YA CHADEMA

- Imesema, Wabunge hao wanashirikiana na Mamlaka kuwahadaa baadhi ya Viongozi wa BAWACHA kwa fedha ili wafike Dar kwenye mkusanyiko wanaouandaa kwa Jina la CHADEMA

Soma - https://jamii.app/BawachaHadaaMdee
MKENYA ANAYETUHUMIWA KWA UGAIDI APELEKWA NEW YORK

> Cholo Abdi Abdullah alikamatwa Ufilipino Julai 2019 amekabidhiwa kwa Maafisa wa #Marekani

> Anatuhumiwa kula njama za kuteka Ndege ya Abiria na kuiangusha kwenye jengo moja Nchini Marekani

Soma https://jamii.app/MkenyaGaidi
KISUTU, DAR: Mahakama yamwachia huru Tariq Machibya (29) almaarufu “Mr. Kuku” baada ya kulipa faini ya Tsh. Milioni tano

> Alikuwa akishtakiwa kwa kufanya biashara ya upatu na kukusanya Fedha za Umma Tsh. Bilioni 17

> Tsh. Bilioni 5.4 zilizokuwa kwny akaunti yake zimetaifishwa
WANAFUNZI 759,706 WALIOFAULU DARASA LA 7, WACHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA 1

- Kati yao, Wavulana ni 368,174 na Wasichana ni 391,532

- Wanafunzi 74,166 hawajapangiwa shule katika Awamu ya Kwanza kutokana na uhaba wa Vyumba vya Madarasa

Soma - https://jamii.app/FormOne2021
ARUSHA: POLISI WAONYA BODABODA WANAOCHAKACHUA VYOMBO

> Mkuu wa Usalama Barabarani amewaonya Waendesha Pikipiki wanaochakachua vyombo hivyo ili vitoe mlio mithili ya Bomu

> Asema, milio hiyo imekuwa kero na inaleta mshtuko kwa wasiopenda kelele

Soma - https://jamii.app/MilioBodaboda
WANAOCHUNA NGOZI ZA MIFUGO WATAKIWA KUWA NA LESENI

> Wizara ya Mifugo imesema, watakaoruhusiwa kuchuna Ngozi za Wanyama Machinjioni ni waliopata mafunzo na kupewa Leseni

> Hatua hiyo inakuja kuongeza Ubora wa Ngozi ili ziweze kuuzwa nje ya Nchi

Soma https://jamii.app/RevenueBase
GEITA: TAKUKURU WAFANIKIWA KUREJESHA TSH. MILIONI 5.48 ZA MWALIMU ALIYETAPELIWA NA QNET

> Imemrejeshea fedha hizo alizodhulumiwa kwa njia za ushawishi, urubuni na kuahidiwa

> Pia, imewataka Watanzania wajiepushe na biashara wasizo na uhakika nazo

Soma https://jamii.app/TAKUKURUQnet
RAIS WA UFARANSA AKUTWA NA #COVID19

> Emmanuel Macron (42) amekutwa na maambukizi ya #CoronaVirus na ana dalili za wazi hivyo atajitenga kwa siku saba

> Waziri Mkuu, Jean Castex pia atajitenga kwa kuwa ni mtu aliyechangamana na Rais huyo

Soma https://jamii.app/MacronFrance
MAKOSA NA ADHABU KWA MUJIBU WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO YA MWAKA 2015

- Vifungu vya 13 na 14: Vinazuia uchapishaji wa Ponografia zinazohusisha #Watoto na watu wazima

- Kifungu cha 16 kinazuia uchapishaji wa taarifa au data ya uongo

- Kifungu cha 20: Kinaainisha makosa kwa kusambaza, kurusha, kusambaza tena taarifa zinazotumwa bila ridhaa au kughushi

- Kifungu cha 23 kinazuia kutumia mawasiliano ya kielektroniki kwa lengo la kusababisha madhara ya kiakili kwa mpokeaji.

Soma > https://jamii.app/CyberCrimeAct15

#Sheria #Haki #JamiiForums
TATIZO LA KUKOSA USINGIZI (INSOMNIA): ATHARI ZAKE NA NAMNA YA KUJIKINGA (2)

- Hali hii huweza kusababisha Uchovu wa mwili, kuwa na hasira au mkali bila sababu za msingi, kupoteza kumbukumbu na kupata magonjwa ya Shinikizo la Damu au Kisukari

- Kujilinda: Usitumie vinjwaji vyenye Caffeine kama Kahawa usiku/jioni, jiwekee ratiba ya kufanya mazoezi, kula mlo mdogo na mwepesi nyakati za usiku na epuka Msongo wa Mawazo

Soma - https://jamii.app/InsomniaDisease
#HealthCare