JamiiForums
βœ”
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SHEIKH JONGO: VIONGOZI WA DINI MSIPIGIE CHAPUO VYAMA VYA SIASA MNAPOHUBIRI

> Afisa wa Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Thabiti Jongo
amewashauri kutoonesha mahaba ya vyama misikitini ili kutowagawa waumini

> Amewataka wahubiri amani

Soma https://jamii.app/DiniSiasaPemba
#Uchaguzi2020
NJOMBE: MBARONI KWA KUUA NA KUMWAGA UBONGO WA BABU YAKE

> Imani Mbilinyi (25) anatuhumiwa kumuua Elia Mbilinyi (90)

> Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alimuuliza Mwenyekiti kama angeweza kumlinda. Mwenyekiti akawaita Mgambo na kutaarifu Polisi

Soma https://jamii.app/MauajiBabuNjombe
UHOLANZI YARUHUSU KIFO CHA MAPEMA KWA WATOTO WENYE MAGONJWA YASIYOPONA

> Serikali ya #Uholanzi imeidhinisha mpango wa kuruhusu kifo cha mapema kwa watoto wenye mwaka 1 mpaka miaka 12

> Lengo ni kuzuia watoto kuteseka kwa maumivu wanayopitia

Soma https://jamii.app/EuthanasiaHoland
MAALIM SEIF AFUNGIWA KUFANYA KAMPENI KWA SIKU 5

> Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imemfungia Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo kuanzia kesho hadi Oktoba 20 kwa kuwashawishi watu wapige kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28

Soma - https://jamii.app/MaalimSeifAfungiwa5
#TZ2020
JAJI MSTAAFU: WASAIDIZI WA SHERIA MJIEPUSHE NA USHABIKI WA KISIASA

> Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman amewataka Wasaidizi wa Sheria wa Majaji kutumia taaluma na kuzingatia weledi katika uendeshaji wa mashauri ya Uchaguzi

Soma https://jamii.app/SheriaWelediUchaguzi
#TZ2020
MDAU: CHUKI NI CHANZO CHA MACHAFUKO, NI MUHIMU KUIEPUKA

> Mdau wa Jamiiforums.com anasema chuki hutokana na hasira inayochochewa na fitina au taarifa mbaya

> Chuki huaribu familia hadi mataifa, ameshauri kujifunza ili kuiepuka

Soma - https://jamii.app/KuepukaChuki
#JFMaarifa
MOROGORO: WATATU MBARONI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

> Rajabu Ramadhani, Athumani Ramadhani na Daniel William wanashikiliwa kwa mauaji ya Bernadetha Kibwana na Zabibu Maulidi

> Bernadetha ameuawa kwa shoka na Zabibu alipigwa na mchi kichwani

Soma - https://jamii.app/TuhumaMauaji
#JFLeo
BAKWATA: VIONGOZI WA DINI WASIFANYE KAMPENI KWENYE NYUMBA ZA IBADA

> Baraza za Ulamaa BAKWATA Taifa limewasihi viongozi wa dini kubaki kuwa wasuluhishi na wapatanishi

> Limewataka waislamu kuiombea nchi ili Uchaguzi Mkuu upite salama

Soma https://jamii.app/BAKWATAUchaguzi
#Uchaguzi2020
WIZARA YA AFYA: WAUGUZI WAZOEFU MUWASIMAMIE WATARAJALI

> Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Ziada Sellah amesema watarajali (interns) wasifanye kazi wenyewe

> Amesema, si sahihi wakiachwa peke yao kuwahudumia wagonjwa hospitalini

Soma - https://jamii.app/WauguziWatarajali
#JFLeo
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
NEC YATAKA VYAMA VYA SIASA KUZINGATIA MAADILI YA UCHAGUZI
-
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka Vyama vya Siasa na Wagombea kuendelea kufuata Maadili ya Uchaguzi na kunadi Sera kwa kufuata utaratibu wa ratiba ambayo imepangwa
-
Pia, Vyama vya Siasa vimetakiwa kukwepa maneno ya uchochezi, kukwepa kuhamasisha watu kufanya vurugu, badala yake vihamasishe watu kwa amani kwenda kupiga kura
-
NEC imesisitiza kwamba Sheria za nchi zipo na zinapaswa kuendelea kufuatwa

#JFLeo #JamiiForums #Uchaguzi2020 #TZ2020
ASKOFU SHOO: VIONGOZI WA DINI KUEGEMEA CHAMA KIMOJA CHA SIASA KUNAWAGAWA WANANCHI

> Kiongozi wa Kanisa la KKKT amesema, "Maandiko yanaelekeza namna ya kusimama na kama kuna mahali pa kukemea kutokana na ukiukwaji wowote, fanya bila ubaguzi”

Soma - https://jamii.app/ViongoziDiniSiasa
#TZ2020
SAMIA SULUHU: HATA UKIPIGIA KURA KWINGINE, CCM ITAUNDA SERIKALI

> Amesema kupigia kura Chama kingine ni sawa na kuweka sukari Ziwa Victoria

> Amewaambia wananchi wakifanya hivyo, hawatakuwa sehemu ya maendeleo yatakayoletwa na CCM

Soma - https://jamii.app/SamiaChunya
#Uchaguzi2020
TUNDU LISSU: NITAONGOZA NCHI KWA KUFUATA KATIBA MPYA ITAKAYOPATIKANA

> Mgombea Urais kupitia CHADEMA amesema, Nchi inahitaji #KatibaMpya ili kurudisha Mamlaka kwa Wananchi kujichagulia Viongozi kwenye maeneo yao na kuwawajibisha wanapokosea

Soma https://jamii.app/LissuSimiyu
#TZ2020
SHINYANGA: VIJANA 2 MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 6

> Jeshi la Polisi linawashikilia vijana 2 wenye umri chini ya miaka 18 kwa tuhuma za kumbaka mtoto kwa zamu baada ya kumlaghai kuwa watamnunulia pipi pamoja na kumpatia hela

Soma - https://jamii.app/VijanaKubakaMtoto
SERIKALI YAHIMIZA WAANDISHI KUSHIRIKI MASHINDANO YA SADC KWA WAANDISHI WA HABARI 2021

> Mashindano hayo yanahusisha washiriki kutoka nchi zote wanachama wa SADC

> Yatakuwa katika makundi manne ambayo ni Picha, Uchapishaji, Runinga na Radio

Soma - https://jamii.app/MashindanoSADC
NEC: VYAMA VIWASILISHE ORODHA YA MAWAKALA SIKU SABA KABLA YA UCHAGUZI

> Pia, imevikumbusha Vyama kuwa, Mawakala ambao vyama vyao havitawapangia vituo hawataapishwa

> NEC imesema kuwa, hakutakuwa na uchelewaji wa vifaa ktk vituo

Soma https://jamii.app/UchaguziMawakala
#TZ2020
WAUGUZI WATAKIWA KUACHA KUTUMIA LUGHA CHAFU KWA WAGONJWA

> Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga amesema, kumekuwa na tabia ya baadhi ya Wauguzi na Wakunga kutoa maneno yasiyofaa kwa wagonjwa jambo linaloharibu taswira ya Sekta ya Afya

Soma - https://jamii.app/LughaChafuWauguzi
WHO: AFRIKA HAIWEZI KUHIMILI WIMBI LA PILI LA #CORONAVIRUS

> Shirika la Afya Duniani limesema mlipuko huo hautaweza kudhibitiwa kama mataifa barani Afrika hayatachukua tahadhari

> Wimbi la pili la #COVID19 litakuwa na athari kubwa kiuchumi

Soma - https://jamii.app/CoronaAfrica
PROF. LIPUMBA: SITISHIKI NA WATU KUJAA KWENYE MIKUTANO YA WAGOMBEA WENGINE

> Mgombea Urais (CUF) amesema anachokifanya yeye ni kwenda Vijijini ambako kuna changamoto kubwa za wananchi na sio kukusanya watu na kuwapeleka kwenye mikutano

Soma https://jamii.app/LipumbaMikutano
#Uchaguzi2020