JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#NAMIBIA: WANAFUNZI ZAIDI YA 300 WAKUTWA NA #CORONAVIRUS

> Wizara ya Afya nchini humo imesema wanafunzi walioambukizwa wengi wao wanasoma Shule za Bweni

> Mpaka sasa #Namibia imethibitisha kuwa na jumla ya maambukizi 11,373 vya #CoronaVirus

Soma https://jamii.app/COVID19Namibia
ORCI: WAGONJWA WENGI WA SARATANI WANAKIMBILIA KWA WAGANGA NA IBADANI

> Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), amesema sababu kubwa ni kurubuniwa na matangazo yasiyo rasmi kuhusu dawa katika Mitandao ya Kijamii

Soma https://jamii.app/SarataniTibaWaganga
SAMIA: HAMNA HAJA YA KUPOTEZA NGUVU ZENU KUPIGIA KURA UPANDE MWINGINE

> Amesema "Ni sawa na kwamba unachukua fedha yako unatia shimoni. Haina faida, haina tija"

> Amewataka wananchi waipigie kura CCM ili kuendelea na safari ya maendeleo

Soma https://jamii.app/SamiaSingida
#TZ2020
LISSU: UAMUZI WA NEC HAUKUBALIKI, KAMPENI ZITAENDELEA JUMAPILI

> Amesema hajapokea malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi na hajawasilisha utetezi wake

> Pia, amesema hajapokea nakala ya kusimamishwa japokuwa ipo mitandaoni

Soma - https://jamii.app/LissuVsTume
#Uchaguzi2020
KENYATTA: NABADILI KATIBA KUWEKA UMOJA WA KITAIFA SIO KUBAKI MADARAKANI

> Rais wa #Kenya amekanusha kutaka kugombea kwa muhula wa 3

> Mabadiliko yanayopendekezwa ni kuundwa Ofisi ya Waziri Mkuu mwenye Mamlaka na Rais atakayechaguliwa na Bunge

Soma https://jamii.app/KenyattaKatiba
#TAKUKURU: UDSM INAONGOZA KWA RUSHWA YA NGONO

> Utafiti uliofanyika kuhusu rushwa ya ngono ktk Chuo cha Dar na Dodoma umegundua UDSM inaongoza kwa 40.5% na UDOM 38.6%

> Mbinu zinazotumika kurubuni ni ahadi ya kuolewa, Cheo na kuongezewa ufaulu

Soma https://jamii.app/RushwaNgonoVyuoni
#COVID19-UGANDA: WAGONJWA WASIOONESHA DALILI KUTOKA HOSPITALI BILA KUPIMWA

> Ni baada ya Serikali kurekebisha mwongozo wake wa kukabiliana na Virusi hivyo

> Awali, wagonjwa walipimwa mara 2 kabla ya kutoka, hatua ambayo baadhi waliilalamikia

Soma https://jamii.app/Corona-UG
MSAJILI: NI MUHIMU KUEPUKA MIGONGANO NA SERIKALI SIKU ZILIZOSALIA

> Jaji Mstaafu Francis Mutungi amewataka wenye malalamiko kufika Tume ya Uchaguzi

> Amesema hafurahishwi na baadhi ya kauli za Wagombea zinazoenda kinyume na Kanuni

Soma - https://jamii.app/MsajiliUchaguzi
#Uchaguzi2020
MAJAJI WA USKOCHI, URUGUAY NA UGANDA KUSIMAMIA KESI YA KABUGA

> Majaji 3 watasimamia kesi ya Felicien Kabuga anayetuhumiwa kufadhili mauaji ya Kimbari ya #Rwanda 1994

> Kesi hiyo itasikilizwa Jijini Arusha na tarehe ya kusikilizwa haijatajwa

Soma https://jamii.app/UNArushaMajaji
QUEEN SENDIGA: MKULIMA KUTUMIA JEMBE LA MKONO NI JAMBO LA HURUMA

> Akiwa Pwani, amesema Mkulima anahitaji nyenzo bora, pembejeo za kisasa na uhakika wa kuuza mazao

> Amesema ataweka mkazo ktk hayo endapo atapigiwa kura Oktoba 28

Angalia https://youtu.be/lm-d8er9kZ4

#Uchaguzi2020
PROF. LIPUMBA: NITATUMIA ELIMU YANGU KUKUZA UCHUMI NA KUFUTA UMASIKINI

> Mgombea Urais wa JMT kupitia CUF, Msomi wa Uchumi, Prof. Ibrahim Lipumba amesema ukuaji wa Uchumi haujapunguza idadi ya masikini

> Amedai umasikini umeongezeka

Soma https://jamii.app/ProfLipumbaUchumi
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI NA DKT. MWINYI KUENDELEA NA KAMPENI ZANZIBAR

> Mgombea Urais JMT na Mgombea Urais Zanzibar (CCM) watafanya kampeni leo ktk Viwanja vya Mnazi Mmoja

> Magufuli aliwasili jana na kumtembelea Kada wa CCM aliyeshambuliwa kwa mapanga

Soma https://jamii.app/MagufuliMwinyi
#TZ2020
RAIS TRUMP AFIKISHWA HOSPITALI KWA HELIKOPTA

> Ni baada ya kupata #COVID19. Rais huyo amepewa kingamwili ya majaribio na alikuwa na uchovu

> Imesisitizwa kuwa, amefikishwa Hospitali kama tahadhari na ataendelea kufanya kazi kutoka hapo

Soma - https://jamii.app/TrumpHospCorona
KENYA: CHAMA TAWALA CHAPENDEKEZA NAIBU RAIS KUFUTWA UONGOZI

> Jubilee kimependekeza William Ruto kuondolewa ktk nafasi yake kama Naibu Kiongozi wa Chama

> Katibu Mkuu wa Jubilee, amedai Ruto ni mjeuri, ana dharau na hamuheshimu Rais Kenyatta

Soma https://jamii.app/JubileeRutoKE
KAMATI YA MAADILI: TAFSIRI YA KWAMBA LISSU AMEADHIBIWA NA NEC SIO SAHIHI

> Katibu wa Kamati ya Maadili ya Kitaifa amesema Lissu ameadhibiwa na Kamati ambayo inajumuisha wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi wa Rais

Soma - https://jamii.app/KamatiMaadiliLissu
#Uchaguzi2020
POLEPOLE: WAPINZANI HAWAONGEZEKI HADI CCM WAWE NA MGOGORO NDANI YA CHAMA

> Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema awamu hii CCM haikuwa na migogoro ya ndani hivyo imekuwa ngumu kwa Upinzani kuongezeka

Soma https://jamii.app/UpinzaniCCM
#Uchaguzi2020
DKT. MWINYI: MUUNGANO UNALETA UMOJA WA KITAIFA

> Mgombea Urais Zanzibar kupitia CCM, Dkt. Hussein Mwinyi amesema, Muungano unaleta amani, utulivu na unatoa fursa kwa Wazanzibari kufanya biashara na kumiliki ardhi Tanzania Bara

Soma https://jamii.app/DktMwinyiMuungano
#Uchaguzi2020
DKT. MAGUFULI: MIPAKA YA TANZANIA SIO YA KURITHI KWA WAKOLONI

> Amesema nchi nyingi za Afrika zina mipaka iliyowekwa na kipindi cha Ukoloni lakini Muungano wa #Tanganyika na #Zanzibar unaifanya #Tanzania kuwa nchi isiyo na mipaka ya kurithi

Soma https://jamii.app/TzMipakaUkoloni
#TZ2020
DKT. MAGUFULI: NIKICHAGULIWA, NITAPATA SHIDA KUMPATA WAZIRI WA ULINZI

> Amesema Waziri wa Ulinzi ana uwezo hata wa kupindua nchi kutokana na vifaa vyote kuwa chini yake

> Amesema ni vigumu kumpata mtu mwadilifu kama alivyokuwa Dkt. Mwinyi

Soma https://jamii.app/WaziriUlinziRais
#TZ2020
ZITTO KABWE: LENGO LETU NI KUMSHINDA MAGUFULI

> Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo akiwa kwenye Kampeni Tandahimba amewaambia wananchi wamchague Mgombea wanayeona ana Nguvu za Kumshinda Dkt. Magufuli (CCM) na wala wasizigawe kura zao

Angalia https://youtu.be/nJYE7F1RC_8
#Uchaguzi2020