JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI AMTEUA MAMA SAMIA SULUHU KUWA MGOMBEA MWENZA

> Rais Magufuli amemsifu Samia Suluhu Hassan kuwa ni mchapakazi na ni mwanamke mzuri

> Ameongeza wao (Wasukuma) wanapenda wanawake weupe, wanaondoa ‘stress’, na mama Samia ni mweupe

Soma https://jamii.app/MkutanoCCM2020
#JFSiasa
LIGI KUU SOKA ENGLAND: KLABU YA NORWICH YASHUKA DARAJA RASMI

- Norwich City imeshuka daraja leo Julai 11, 2020 baada ya kupokea kipigo cha goli 4-0 kutoka kwa West Ham

- Klabu hiyo ipo nafasi ya mwisho ikiwa na alama 21 baada ya kucheza michezo 35

#JFSports #JFMichezo #Sports
SHEIKH PONDA MBARONI. KUHOJIWA KUHUSU WARAKA WA SHURA YA MAIMAMU

> Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda amekamatwa na Polisi kuhojiwa kuhusu waraka ambao viongozi wote wa Taasisi hiyo wameukana

Soma https://jamii.app/SheikhArrested
DKT. KAZI ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TIC

> Rais Magufuli amteua Dkt. Maduhu Isaac Kazi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania

> Dkt. Kazi alikuwa Meneja Idara ya Sera za Kibajeti na Madeni wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT

Soma https://jamii.app/TeuziDktKazi
#JFLeo
UGOMVI WA MALI: KANISA LASHAMBULIWA, WATANO WAUAWA

> Kanisa la International Pentecostal Holiness la Afrika Kusini lavamiwa, waumini watekwa na watano kuuawa

> Polisi wamewaokoa waliotekwa, watu 40 wamekamatwa. Pia, bunduki 16 na bastola 13 zimekamatwa

Soma https://jamii.app/AttacksSAChurch
WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAFARIJIWA NA MKUTANO MKUU WA CCM

> Jukwaa la Wahariri Tanzania, wameipongeza CCM kurusha 'live' Mikutano yao

> Wameshauri utaratibu huo uwepo kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi Zanzibar, Mahakamani na Bungeni, kwani mambo wanayojadili ni kwa maslahi ya taifa na watu wake

Soma https://jamii.app/TEFYaombaUwazi
#JFSiasa
UCHAGUZI 2020: UDP WAOMBA KUPEWA NAFASI MOJA YA DIWANI NA WABUNGE WATATU

> Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo ameomba nafasi hizo ili waende kuwatetea Wakulima

> Amesema katika Uchaguzi huu hawatakuwa na mgombea wa Urais bali wanamuunga mkono mgombea wa CCM

Soma https://jamii.app/DhifaCCM2020
#JFSiasa
COSOTA YAHAMISHIWA CHINI YA WIZARA YA HABARI KUTOKA WIZARA YA BIASHARA

- Rais Magufuli ameihamisha COSOTA kutoka kuwa chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

- Pia, amewashukuru Wasanii wote hususan wa muziki kwa kuitangaza Tanzania vizuri na kuwataka kuendelea kufanya hivyo

Soma https://jamii.app/DhifaCCM2020
NUSU FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

- Klabu ya Simba inapata goli la kuongoza dhidi ya Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho

- Goli la Simba limefungwa na Gerson Fraga katika dakika ya 21

#SimbaSC #YangaSC #Sports #JFMichezo
MICHEZO: NUSU FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

- Mpira umeenda mapumziko huku Simba SC ikiwa inaongoza kwa goli 1-0 dhidi ya Yanga SC

- Goli la Simba limefungwa na Gerson Fraga katika dakika 21 ya mchezo huo

#SimbaSC #YangaSC #Sports #JFMichezo
NUSU FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

- Klabu ya Simba inaongoza kwa 3-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho

- Goli la kwanza limefungwa na Gerson Fraga katika dakika ya 21

- Goli la pili limefungwa na Clatous Chama huku goli la tatu likifungwa na Josee Miquisson

#SimbaSC #YangaSC #Sports #JFMichezo
SIMBA SC YAIADHIBU YANGA SC. YATINGA FAINALI YA KOMBE LA SHIRIKISHO

- Simba imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga Yanga SC goli 4-1 katika mchezo wa nusu fainali

- Magoli ya Simba yamefungwa na Gerson Fraga, Clatous Chama, Luis Miquisson na Mzamiru Yassin huku goli la kufutia machozi la Yanga likifungwa na Feitoto

#SimbaSC #YangaSC #Sports #JFMichezo
SUDAN: SERIKALI KUONDOA SHERIA ZINAZOKIUKA HAKI ZA BINADAMU

- Nchi hiyo imefuta Sheria ya Uasi pamoja na adhabu ya viboko. Ukeketaji wa Wanawake umepigwa marufuku

- Pia, Wananchi wasio Waislamu wameruhusiwa kuagiza, kuuza na kunywa pombe

Soma https://jamii.app/HumanRightsSudan
IRAN YATAJA 'KOSA LA KIBINADAMU' KUWA CHANZO CHA KUDUNGULIWA KWA NDEGE YA UKRAINE

- Abiria 176 walipoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea Januari mwaka huu

- Mawasiliano mabovu yametajwa kuwa sababu mojawapo ya ndege kudunguliwa kimakosa

Soma https://jamii.app/UkraineCrashIran
AFRIKA KUSINI YAREJESHA MASHARTI YA KUTOTOKA NDANI. UUZAJI POMBE WAZUIWA

> Rais Cyril Ramaphosa ametangaza kurudisha marufuku iliyokuwepo ya uuzaji wa pombe na zuio la kutotoka ndani usiku

> Marufuku ya kutoka ndani usiku itaanza kutekelezwa leo na itakuwa ikianza saa 3 usiku hadi saa 10 alfajiri kila siku

Soma - https://jamii.app/AlcoholCurfewSA
#JFLeo
MALI: VIONGOZI WA UPINZANI WAMTAKA RAIS IBRAHIM KEITA KUJIUZULU

- Kumekuwa na maandamano baada ya Muungano wa upinzani kukataa makubaliano yaliyosainiwa kumaliza mgogoro wa kisiasa

- Watu 4 wamepoteza maisha katika maandamano hayo

Soma - https://jamii.app/UpinzaniMaandamanoMali
RC HAPI: SIWEZI KUWA MBUNGE ILI NIPELEKE SHIDA ZA WANANCHI KWA RC

> Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema hana mpango wa kugombea Ubunge kwani itamlazimu kupeleka shida za wananchi wake kwa Mkuu wa Mkoa ili amtatulie, kitendo ambacho hayuko tayari kukifanya

> Pia, amewataka wanasiasa kuwa na heshima badala ya kulaumu kwa kila kitu na kufuata sheria na taratibu hususan ktk ufanyaji wa mikutano

Soma - https://jamii.app/HapiUbunge2020
MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA FEDHA NCHI ZA SADC KUANZA LEO

> Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango anatarajiwa kuongoza Mkutano huo utakaofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia leo hadi Julai 15, 2020

> Utajadili masuala ya Fedha na Uwekezaji na kutoa maamuzi ya kisera kuhusu athari za Kiuchumi na Kijamii za COVID-19

Soma - https://jamii.app/MkutanoWaziriSADC
AFRIKA KUSINI: MTOTO WA NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA

- Zindzi Mandela (59) amefariki asubuhi ya leo akiwa Hospitali Jijini Johannesburg. Chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi

- Amefariki akiwa ni Balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark

Soma - https://jamii.app/ZindziMandelaDies
#CORONAVIRUS: MEXICO INAKUWA NCHI YA 4 KWA VIFO DUNIANI

- Mexico imerekodi vifo 276 ndani ya saa 24 zilizopita, idadi ya vifo imefikia 35,006

- Nchi hiyo ina visa 299,750 vya #COVID19 na hadi sasa wagonjwa waliopona ni 184,764

Soma - https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID19_Updates