JamiiForums
βœ”
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
#CORONAVIRUS KENYA: WIZARA YA AFYA YAONYA KUHUSU KUPULIZA KEMIKALI MITAANI

- Wizara ya Afya imeonya kemikali haziondoi Virusi hivyo, na ni hatari kiafya

- Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara hiyo, Dkt. Amoth amesema inaweza kuleta matatizo ya upumuaji

Soma https://jamii.app/CoronaDisinfectantsKE
MAMLAKA YA POLISI KWA MUJIBU WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO

> Kifungu cha 31: Polisi au watekelezaji wa sheria wanaweza kutoa amri inayoruhusu kuingia, kupekua, au kutwaa vifaa na mifumo ya kompyuta, na kutwaa data au taarifa zilizohifadhiwa kwenye kompyuta

> Wanaweza kufanya hivyo iwapo watajiridhisha kwamba kuna sababu za msingi kuamini kwamba mfumo huo wa kompyuta unaweza kutumika kama sehemu ya ushahidi

Zaidi, soma > https://jamii.app/SheriaMtandaoPolisi

#UhuruWaKujieleza
MAUAJI YA MWANAMUZIKI ETHIOPIA: VIFO VYA WAANDAMANAJI VYAFIKIA 166

> Watu 166 wameuawa katika maandamano yanayofanyika kufuatia kifo cha Mwanamuziki Hachalu Hundessa (34) aliyefariki kwa kupigwa risasi

> Watu 167 wameachwa na majeraha makubwa huku wengine 1,084 wakikamatwa na Polisi

Soma - https://jamii.app/MaandamanoVifoEthiopia
WHO YAREKODI MAAMBUKIZI 212,326 YA #COVID19 NDANI YA SAA 24

> Shirika la afya Duniani limesema maambukizi 130,000 yanatokea Marekani, Brazil na Mexico huku Afrika Kusini ikirekodi maambukizi 10,000

> Mpaka sasa watu zaidi ya Milioni 11 wameambukizwa #Corona na zaidi ya laki 5 wamefariki

Soma - https://jamii.app/CoronaCasesRise
RAIS MAGUFULI ATEUA DC WA MVOMERO NA MKURUGENZI WA BIHARAMULO

- Amemtea Albinus Mgonya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero akichukua nafasi ya Mohamed Musa Utaly

- Waziri Khachi Kombo amekuwa Mkurugenzi wa Biharamulo akichukua nafasi ya Wendi Ng’ahala

Soma https://jamii.app/UteuziMagufuli
JE, DAWA YA #COVID19 YA MADAGASCAR IMEDUNDA? MJI MKUU WAWEKWA β€˜LOCKDOWN’

- Madagascar imeuweka Mji wake Mkuu, Antananarivo kwenye β€˜lockdown’ mpya kufuatia ongezeko jipya la maambukizi ya #CoronaVirus

- Mtu mmoja pekee kutoka katika kila Kaya ndio ataruhusiwa kutoka ndani kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa sita mchana

Soma https://jamii.app/AntananarivoLockdown
#JFCOVID19_Updates
MWANZA: AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI BAADA YA KUVUNJA BENKI

> Mtu huyo na wenzake walifanikiwa kuvunja na kuingia ndani ya benki ya CRDB tawi la Igoma

> Walifanikiwa kuvuruga droo za ofisi, hawakuweza kuiba fedha zilizokuwa sehemu maalumu

NB: Picha si ya tukio halisi
Soma https://jamii.app/MwanzaRisasi
MAAMBUKIZI YA #COVID19 YAFIKIA 11,562,878 DUNIANI

> Jumla ya vifo 536,841 vimeripotiwa huku watu 6,537,765 wakipona

> Barua ya wazi ya Wanasayansi inatarajiwa kupelekwa WHO kuonesha #COVID19 inaweza kusambazwa kwa hewa

Soma https://jamii.app/COVID19Updates
#JFCOVID9_Updates
MAREKANI: SANAMU YA CHRISTOPHER COLUMBUS YAANGUSHWA

- Waandamanaji wameangusha sanamu hiyo na kuitupa kwenye maji katika bandari ya mji wa Baltimore

- Wanahistoria wanasema Columbus aliyegundua bara la Amerika alihusika pia katika utumwa na unyonyaji

Angalia; https://youtu.be/7dBPx-hhSVE
#JFLeo
IKULU, DODOMA: RAIS MAGUFULI KUWAAPISHA WATEULE MBALIMBALI

- Leo, Rais Magufuli anatarajia kuwaapisha viongozi mbalimbali wa Mikoa na Wilaya aliowateua hivi karibuni

- Baadhi ya viongozi ni Thobias Andengenye aliyeteuliwa kuwa RC wa Kigoma

Fuatilia https://jamii.app/UapishajiDodoma
RAIS MAGUFULI AMUAGIZA IGP KUWAONDOA OCD, OCCID, NA AFISA USALAMA MERU

> Ni baada ya Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya #DawaZaKulevya kwenda Meru na kukamata magunia ya Bangi

> Amesema kuna kasoro kwani haiwezekani waliopo huko hawakuyakamata hadi mtu atoke Dodoma Makao Makuu kukamata

Soma https://jamii.app/JPMJulai2020
DAR: POLISI WATOA ONYO KUHUSU MAANDAMANO YA JULAI 7, 2020

> Polisi Kanda Maalum Dar wamesema maandamano ya #77Nyeupe ni batili, watakaoshiriki watachukuliwa hatua za kisheria

> Maandamano hayo yanahamasishwa mitandaoni ili kudai Tume Huru ya Uchaguzi

Soma https://jamii.app/77NyeupeOnyo
DAR: WATU 32 MBARONI KWA TUHUMA ZA WIZI WA TSH. BILIONI 2.082 ZA NMB

> Watu hao ni pamoja na Wafanyakazi 5 wa kampuni ya Ulinzi ya SGA waliopewa Tsh. 2,082,000,000 kuzitoa NMB-Mbezi Beach ili kuzipeleka NMB Benki House na kisha kuchukua Tsh. 780,000,000 na kutokomea nazo

Angalia Video; https://youtu.be/iKmqnYD9UP4
TCRA YAIFUNGIA KWANZA TV KWA MIEZI 11

> Ni kwa kukiuka Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta 2018 kwa kuchapisha taarifa ya Ubalozi wa Marekani

> TCRA imesema taarifa hiyo ilijaa upotoshaji na Kwanza TV waliichapisha bila kuzingatia mizania

Soma https://jamii.app/KwanzaTVBan
#JFLeo
MEMBE NA MKEWE WARUDISHA KADI YA CCM

> Bernard Membe na mkewe wamerudisha kadi na kuwashukuru CCM kwa mema yote waliyomtendea akiwa Mwanachama wa CCM

> Julai 2, kupitia BBC-Swahili, Membe alisema atagombea Urais kupitia upinzani kama wakimpa nafasi

Soma https://jamii.app/MembeArudishaKadi
#JFSiasa
KENYA: RAIS KENYATTA AFUNGUA MIJI YA NAIROBI, MOMBASA NA MANDERA

> Pia, ameongeza kwa siku 30 zuio la kutotoka ndani linaloanza saa 3 usiku hadi saa 10 alfajiri

> Ameruhusu ibada kurejea kwa waumini kutozidi 100 kwenye ibada na ibada isizidi saa 1

Soma https://jamii.app/CurfewKECOVID19
#JFCOVID19_Updates
RUKWA: WATU 380 WAMENUSURIKA KUFA BAADA YA MAJI YA KISIMA KUWEKEWA SUMU

> Waombolezaji waliokuwa karibu na kisima ambacho wangechota maji ya kunywa na kupikia wamenusurika kufa baada ya maji hayo kuwekewa sumu

> Maji yalijulikana kuwa na sumu baada ya mifugo wakiwemo ng’ombe 16 kufa baada ya kunywa maji hayo

Soma https://jamii.app/380Wanusurika
MAKATIBU TAWALA WA WILAYA 6 WATEULIWA AKIWEMO HASSAN NGOMA

- Waziri wa Utumishi, George Mkuchika amemteua Hassan Ngoma kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Singida

- Makatibu Tawala wengine ni wa Wilaya za Longido, Karatu, Malinyi, Gairo na Bunda

Soma https://jamii.app/UteuziDAS-6
RAIS MAGUFULI AKIZUNGUMZIA SUALA LA KUTOA RUHUSA KWA ALIOWATEUA

> Rais Magufuli amesema Viongozi aliowateua wakiomba ruhusa kwenda kwenye majukumu mengine anatoa haraka ruhusa hiyo

> Amesema viongozi wengine wameteuliwa baada ya waliokuwepo kuomba ruhusa. Hivyo mtu akiomba ruhusa yeye anakubali na kuteua mwingine

Angalia; https://youtu.be/X4oKDG-24XQ
#JFSiasa #Siasa #JamiiForums
MWANZA: RAIA WA CHINA AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUTOA RUSHWA

> TAKUKURU imemkamata Sheng Bing Lin (40) kwa tuhuma za kutoa Rushwa ya Tsh. 100,000 ili arudishiwe mashine ya 'betting' iliyokamatwa kwa kukosa kibali na kuchezeshwa muda usioruhusiwa

Soma https://jamii.app/MchinaMbaroni